bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 2
Exodus 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 3 →
1
Mtu wa mlango wa Lawi akaenda, akaoa mwanamke wa Kilawi.
2
Huyo mwanamke akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume; naye alipomwona kuwa mtoto mzuri, akamficha miezi mitatu.
3
Asipoweza kumficha tena, akamchukulia sanduku ya mafunjo, akayaziba kwa udongo wenye utomvu mweusi na kuyapata lami, akamweka mtoto humo ndani; kisha akaiweka hiyo sanduku katika manyasi kando ya mto mkubwa.
4
Umbu lake mtoto akasimama mbali, aone yatakayompata.
5
Mara akatelemka binti Farao, aoge mtoni, vijakazi wake wakitembea kando ya jito. Yeye alipoiona hiyo sanduku katikati ya manyasi akatuma kijakazi wake mmoja kuichukua.
6
Alipoifunua akamwona mtoto, naye huyu kitoto alikuwa akilia; naye akamhurumia, akasema: Ni mtoto wa Waebureo huyu.
7
Ndipo, umbu lake mtoto alipomwuliza binti Farao: Niende kukuitia mnyonyeshaji wa Kiebureo, akunyonyeshee mtoto?
8
Binti Farao akamwambia: Nenda! Ndipo, yule kijana wa kike alipokwenda, akamwita mamake mtoto.
9
Naye binti Farao akamwambia: Mchukue huyu mtoto, uninyonyeshee! Nami nitakupa msahahara wako. Kisha huyo mwanamke akamchukua mtoto, akamnyonyesha.
10
Mtoto alipokuwa mkubwa, akampeleka kwa binti Farao, naye akamwia mwanawe, akamwita jina lake Mose akisema: Kwani nilimtoa majini.
11
Siku zile Mose alipokwisha kukua akatoka kwenda kwa ndugu zake; alipovitazama, walivyofanyishwa kazi ngumu, akaona Mmisri mmoja, akimpiga mmoja wao ndugu zake wa Kiebureo.
12
Ndipo, alipogeuka huko na huko, tena alipoona, ya kama hakuna mtu, akampiga yule Mmisri na kumwua, kisha akamfukia mchangani.
13
Kesho yake alipotoka akaona, wawili wa Kiebureo wakipigana, akamwambia aliye mkorofi: Mbona unampiga mwenzako?
14
Naye akajibu: Yuko nani aliyekuweka kuwa mkuu wa mwamuzi kwetu? Je? Wewe unataka kuniua nami, kama ulivyomwua yule Mmisri? Ndipo, Mose aliposhikwa na woga, akasema: Kumbe lile jambo limejulikana.
15
Farao alipolisikia neno hilo, akamtafuta Mose, amwue; lakini Mose akamkimbia Farao, asimwone, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani, akakaa kwenye kisima.
16
Naye mtambikaji wa Midiani alikuwa na wana wa kike saba; hao walipokuja kuchota maji na kupajaza maji hapo, walipopatengeneza pa kunyweshea mbuzi na kondoo wa baba yao,
17
wakaja wachungaji wengine na kuwafukuza. Ndipo, Mose alipoinuka, akawasaidia akiwanywesha mbuzi na kondoo wao.
18
Walipofika kwa baba yao Reueli, akawauliza: Inakuwaje, mkifika leo, kukiwa mchana bado?
19
Wakasema: Mtu wa Kimisri ametuponya mikononi mwa wale wachungaji, kisha akatuchotea maji, akawanywesha mbuzi na kondoo.
20
Akawauliza wanawe: Yuko wapi? Mbona mmemwacha huko? Mwalikeni, ale nasi!
21
Kisha Mose akapatana kukaa kwake yule mtu, akampa Mose mwanawe Sipora kuwa mkewe.
22
Alipomzalia mtoto wa kiume, akamwita jina lake Gersomu (Mgeni wa Huku), kwani alisema: Nimekuwa mgeni katika nchi isiyo ya kwetu.
23
Siku zilipopita nyingi, yule mfalme wa Misri akafa. Nao wana wa Isiraeli wakapiga kite pamoja na kulia kwa ajili ya utumwa wao, nayo hayo malalamiko yao yakapanda, yakafika kwake Mungu kwa ajili ya huo utumwa wao.
24
Mungu alipoyasikia hayo mauguzi yao, yeye Mungu akalikumbuka Agano lake, alilomwekea Aburahamu na Isaka na Yakobo.
25
Ndipo, Mungu alipowaonea machngu wana wa Isiraeli, kwani yeye Mungu aliwajua, walivyo.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40