bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 37
Exodus 37
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 38 →
1
Kisha Besaleli akalitengeneza Sanduku la mbao za migunga, urefu wake ulikuwa mikono miwili na nusu, nao upana wake ulikuwa mkono mmoja na nusu, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mkono mmoja na nusu.
2
Akalifunikiza lote dhahabu tupu, upande wa ndani na upande wa nje, kisha akazungusha juu yake taji ya dhahabu.
3
Kisha akatengeneza mapete manne kwa kuyeyusha dhahabu, akayatia penye pembe zake nne, mapete mawili upande wake mmoja, tena mapete mawili upande wake wa pili.
4
Kisha akatengeneza mipiko ya migunga, nayo akaifunikiza dhahabu.
5
Kisha akaitia mipiko hiyo katika yale mapete pande zote mbili za Sanduku, iwe ya kulichukulia Sanduku.
6
Kisha akakitengeneza kifuniko kuwa Kiti cha Upozi cha dhahabu tupu, urefu wake ulikuwa mikono miwili na nusu, nao upana wake ulikuwa mkono mmoja na nusu.
7
Kisha akatengeneza Makerubi mawili ya dhahabu, nayo yalitengenezwa kwa kuzifuafua hizo dhahabu, akayaweka pande zote mbili za mwisho wa Kiti cha Upozi:
8
Kerubi moja akaliweka upande wa mwisho wa huku, nalo la pili upande wa mwisho wa huko. Ndivyo, alivyoyaweka hayo Makerubi pande zake zote mbili za mwisho wa Kiti cha Upozi.
9
Nayo Makerubi yalikuwa yameyakunjua mabawa juu yakikifunika Kiti cha Upozi kwa mabawa yao, nazo nyuso zao zilikuwa zimeelekeana, hayo Makerubi yakikitazama Kiti cha Upozi kwa nyuso zao.
10
Kisha akatengeneza meza kwa mbao za migunga, urefu wake ulikuwa mikono miwili, nao upana wake ulikuwa mkono mmoja, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mkono mmoja na nusu;
11
akaifunikiza dhahabu tupu, kisha akazungusha juu yake taji ya dhahabu.
12
Kisha akazungusha kando yake kibao cha kukingia chenye upana wa shibiri, nacho hicho kikingio akakizungushia taji ya dhahabu.
13
Kisha akaitengenezea mapete manne kwa kuyeyusha dhahabu, nayo hayo mapete akayatia penye pembe zake nne zilizokuwa penye miguu yake minne.
14
Hayo mapete yalikuwa papo hapo chini ya kikingio, wapate kutia humo mipiko ya kuichukulia hiyo meza.
15
Kisha akatengeneza mipiko kwa migunga na kuifunikiza dhahabu, itumike ya kuichukulia hiyo meza.
16
Kisha akatengeneza vyombo vya kuweka hapo mezani: vyano vyake na vijiko vyake na vikombe vyake na vitungi vyake vinavyotumikia vinywaji vya tambiko; vyote vilikuwa dhahabu tu.
17
Kisha akatengeneza kinara cha dhahabu tupu; hicho kinara nacho akakitengeneza kwa kufuafua dhahabu, ikapata kukitoka chote kizima: shina lake na mti wake navyo vikombe vyake na vifundo vyake na maua yake, vyote pia vilikuwa vimetoka dhahabu iyo hiyo moja.
18
Matawi sita yalitoka penye mbavu zake, matawi matatu ya kinara yalitoka penye ubavu mmoja, tena matawi matatu ya kinara yalitoka penye ubavu wa pili.
19
Vikombe vitatu vilivyofanana na maua yao. Vivyo hivyo vilikuwa katika matawi yote sita yaliyotoka katika mti wa kinara.
20
Lakini katika mti wa kinara vilikuwa vikombe vinne vilivyofanana na maua ya mlozi, yaani vifundo pamoja na maua yao.
21
Tena kila mahali matawi mawili yalipotoka katika huo mti wake, chini yake kilikuwa kifundo kimoja; vilikuwa vivyo hivyo kila mahali, yalipotoka matawi mawili, nayo matawi yaliyotoka katika kinara yalikuwa sita.
22
Vifundo na matawi yao yote ilikuwa kazi moja iliyoyatokeza yote pamoja kwa kuifua dhahabu iyo hiyo moja, nayo yalikuwa dhahabu tupu.
23
Kisha akatengeneza taa zake saba; nazo koleo zake na makato yake yote yalikuwa dhahabu tupu.
24
Alikitengeneza kinara pamoja na vyombo vyake kwa kipande cha dhahabu chenye uzito wa mizigo miwili.
25
Kisha akatengeneza kwa migunga meza ya kuvukizia; urefu wake ulikuwa mkono mmoja, nao upana wake ulikuwa mkono mmoja, pande zote nne zilikuwa sawa, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mikono miwili.
26
Akaifunikiza dhahabu tupu juu yake na kando yake pande zote na pembe zake, akazungusha juu yake taji ya dhahabu pande zote.
27
Kisha akaitengenezea mapete mawili ya dhahabu, akayatia chini ya taji pande zake mbili penye mbavu zake mbili, yawe ya kutilia mipiko ya kuichukulia.
28
Kisha akatengeneza mipiko kwa migunga, akaifunikiza dhahabu.
29
Kisha akatengeneza mafuta matakatifu ya kupaka na mavukizo yanukayo vizuri yasiyochanganyika na mengine, kama mafundi wa kutengeneza manukato wanavyojua kuyatengeneza.
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 38 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40