bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 29
Exodus 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 30 →
1
Hili ndilo jambo, utakalowafanyia, uwaeue kuwa watambikaji wangu: chukua dume la ng'ombe aliye kijana bado na madume mawili ya kondoo wasio na kilema,
2
na mikate isiyochachwa na maandazi yasiyochachwa yaliyotiwa mafuta na maandazi membamba yasiyochachwa, yaliyopakwa mafuta juu tu; haya yote uyatengeneze kwa unga mwembamba wa ngano.
3
Kisha yote uyatie katika kikapu kimoja, uyapeleke humo kikapuni pamoja na yule dume la ng'ombe na wale madume mawili ya kondoo.
4
Kisha umfikishe Haroni pamoja na wanawe hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, uwaoshe kwa maji.
5
Kisha yachukue hayo mavazi, umvike Haroni shati na kanzu na kisibau na kibati cha kifuani, kisha umfunge kisibau kwa masombo ya kisibau.
6
Kisha umvike kilemba kichwani pake na kulitia lile bamba takatifu katika kilemba chake.
7
Kisha chukua mafuta ya kumpaka, umpake na kuyamimina kichwani pake.
8
Kisha nao wanawe uwafikishe, uwavike shati;
9
kisha uwafunge mishipi, yeye Haroni na wanawe, uwafunge vilemba virefu; ndipo, utambikaji utakapokuwa wao kwa hayo maongozi ya kale na kale. Kisha umjaze Haroni gao lake, nao wanawe uwajaze magao yao.
10
Kisha umlete dume la ng'ombe, afike hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; ndipo Haroni na wanawe wambandikie huyo dume la ng'ombe mikono yao kichwani pake.
11
Kisha umchinje huyo dume la ng'ombe mbele ya Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
12
Kisha uchukue damu kidogo ya huyo dume la ng'ombe, uzipake pembe za meza ya kutambikia kwa kidole chako, nayo damu yote nyingine umwagie msingi wa meza ya kutambikia.
13
Kisha yachukue mafuta yote yanayoufunika utumbo na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo yake mawili nayo mafuta yanayoshikamana nayo, uyachome moto hapo mezani pa kutambikia.
14
Lakini nyama zake huyo dume la ng'ombe na ngozi yake na mavi yake uyateketeze kwa moto nje ya makambi, maana ni ng'ombe ya tambiko ya weuo.
15
Kisha wale madume ya kondoo chukua mmoja, naye Haroni na wanawe na wambandikie huyo dume la kondoo mikono yao kichwani pake
16
Kisha umchinje huyo dume la kondoo, nayo damu yake ichukue, uinyunyizie meza ya kutambikia pande zote.
17
Kisha huyo dume la kondoo umchangue kuwa vipande viwili, kisha uuoshe utumbo wake na miguu yake, upate kuviweka juu y vile vipande vyake na juu ya kichwa chake.
18
Huyo dume la kondoo wote umchome moto hapo mezani pa kutambikia kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima, ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
19
Kisha mchukue yule dume la kondoo wa pili, naye Haroni na wanawe na wambadikie huyo dume la kondoo mikono yao kichwani pake.
20
Kisha umchinje huyo dume la kondoo, uchukue damu yake kidogo, uwapake Haroni na wanawe pembe za chini za masikio yao ya kuume na vidole gumba vya mikono yao ya kuume na vidole gumba vya miguu yao ya kuume, nayo damu nyingine uinyunyizie meza ya kutambikia pande zote.
21
Kisha uchukue damu kidogo iliyoko mezani pa kutambikia na mafuta ya kupaka kidogo umnyunyizie Haroni na mavazi yake, kisha uwanyunyizie nao wanawe na mavazi ya wanawe; ndivyo, anavyoeuliwa yeye pamoja na mavazi yake, tena ndivyo, nao wanawe wanavyoeuliwa pamoja na mavazi yao.
22
Kisha uyachukue mafuta ya huyo dume la kondoo ni mkia na mafuta yaliyoufunika utumbo na kile kipande cha ini na mafigo yake mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo na paja la kuume, maana ni dume la kondoo apasaye siku ya kujazwa gao.
23
Uchukue tena katika kikapu cha mikate isiyochachwa kilichowekwa mbele ya Bwana mkate mmoja na andazi moja lililotiwa mafuta na andazi jembamba moja.
24
Haya yote uyaweke mikononi mwa Haroni namo mikononi mwa wanawe, uyapitishe motoni mbele ya Bwana.
25
Kisha uyachukue mikoni mwao uyachome moto mezani pa kutambikia kuwa moshi juu ya ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa, hivyo yatakuwa mbele ya Bwana mnuko wa moto wa kumpendeza Bwana.
26
Kisha uchukue kidari cha dume la kondoo la Haroni la kulijaza gao lake, ukipitishe mbele ya Bwana; kisha kitakuwa fungu lako.
27
Ndivyo, utakavyokitakasa kidari kuwa kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni, hata paja kuwa kipaji cha tambiko cha kunyanyuliwa, maana kidari kilipitishwa motoni, nalo paja lilinyanyuliwa kuwa lake Bwana; nacho hicho kidari pamoja na hilo paja yalitoka kwa dume la kondoo wa Haroni na wa wanawe aliyetolewa kuyajaza magao yao.
28
Hii na iwe haki yao Haroni na wanawe ya kale na kale kuyapata kwa wana wa Isiraeli, kwani ndio vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa, na viwe vyao, wana wa Isiraeli watakapotoa ng'ombe za tambiko za shukrani, maana vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa ni vyake Bwana.
29
Nayo mavazi matakatifu ya Haroni na yawe ya wwanawe, watakapomfuata, wayavae watakapopakwa mafuta ya kujazwa magao yao.
30
Mwanawe atakayepata utambikaji sharti ayavae siku saba, apate kuingia katika Hema la Mkutano na kutumikia Patakatifu.
31
Lakini huyo dume la kondoo aliyetolewa kuwajaza magao sharti umchukue, uzitokose nyama zake mahali patakatifu.
32
Naye Haroni na wanawe na wazile nyama zake huyu dume la kondoo pamoja na mikate iliyomo katika kikapu hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
33
Na wazile, kwa kuwa ndizo, walizopatiwa upozi nazo, wapate kujazwa magao pamoja na kueuliwa; lakini mgeni hana ruhusa kuzila, kwani ni takatifu.
34
Kama ziko nyama zitakazosalia zilizokuwa za kuwajaza magao, au kama iko mikate itakayosalia mpaka kesho, sharti uyateketeze hayo masao kwa moto, yasiliwe na mtu, kwani ni matakatifu nayo.
35
Sharti uwafanyizie Haroni na wanawe hivyo vyote, nilivyokuagiza, ukiwajaza magao yao siku saba.
36
Kila siku utatoa dume la ng'ombe aliye kijana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kumpatia upozi, uieue nayo meza ya kutambikia kwa kuwapatia upozi hapo; kisha umpake mafuta ya kumfanya kuwa mtakatifu.
37
Siku saba nayo meza ya kutambikia uipatie upozi na kuitakasa, ndipo, meza ya kutambikia itakapokuwa takatifu yenyewe, naye kila atakayeigusa sharti awe ametolewa kuwa mtakatifu.
38
Nayo haya ndiyo, utolee mezani pa kutambikia: wana kondoo wawili wa mwaka mmoja kila siku pasipo kukoma.
39
Mwana kondoo mmoja umtoe asubuhi, naye mwana kondoo wa pili umtoe saa za jioni.
40
Tena pamoja na kila mwana kondoo utoe vibaba vitatu vya unga mwembamba uliochanganywa na kibaba kimoja cha mafuta yaliyotwangwa vema, tena kibaba kimoja cha mvinyo kuwa kinywaji cha tambiko.
41
Naye mwana kondoo wa pili na umtoe saa za jioni pamoja na kilaji cha tambiko kama asubuhi; huo utakuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
42
Hizi na ziwe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wao wa vizazi vyenu watakazozitoa siku zote mbele ya Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; hapo ndipo, nitakapokutana nanyi, napo ndipo, nitakaposema na wewe.
43
Hapo ndipo, nitakapokutana kweli na wana wa Isiraeli, nalo Hema litapata kuwa takatifu kwa ajili ya utukufu wangu.
44
Mimi nitalitakasa Hema la Mkutano na meza ya kutambikia, naye Haroni na wanawe nitawatakasa, wapate kuwa watambikaji wangu.
45
Nami nitakaa katikati ya wana wa Isiraeli, niwe Mungu wao.
46
Nao watajua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wao aliyewatoa katika nchi ya Misri, nikae katikati yao, mimi Bwana niliye Mungu wao.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40