bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 20
Exodus 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 21 →
1
Mungu akayasema maneno haya yote kwamba:
2
Mimi ndimi Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa.
3
usiwe na miungu mingine ila mimi!
4
Usijifanyie kinyago wala mfano wo wote wa vitu vilivyoko mbinguni juu, wala vilivyoko nchini chini, wala vilivyomo majini chini ya nchi!
5
Usivitambikie, wala usivitumikie! Kwani mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; manza za baba nitazipatilizia wana, nikifikishe kizazi cha tatu na cha nne, kwao wanichukiao.
6
Lakini nitawafanyizia mema, nikifikishe hata kizazi cha maelfu, kwao wanipendao na kuyashika maagizo yangu.
7
Usilitaje Jina la Bwana Mungu wako bure! Kwani Bwana hatamwachilia alitajaye Jina lake bure.
8
Ikumbuke siku ya mapumziko kuitakasa!
9
Siku sita sharti ufanye kazi, uyamalize mambo yako yote!
10
Lakini siku ya saba ndiyo ya kumpumzikia Bwana Mungu wako. Hapo usifanye kazi yo yote, wala wewe, wala mwanao wa kiume, wala wa kike, wala mtumishi wako wa kiume, wala wa kike, wala nyama wako wa kufuga, wala mgeni wako aliomo malangoni mwako.
11
Kwani siku sita Bwana alizifanya mbingu na nchi na bahari navyo vyote vilivyomo, akapumzika siku ya saba; kwa hiyo Bwana aliibariki siku ya saba, akaitakasa.
12
Mheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!
13
Usiue!
14
Usizini!
15
Usiibe!
16
Usimshuhudie mwenzio uwongo!
17
Usiitamani nyumba ya mwenzio! Usimtamani mke wa mwenzio, wala mtumishi wake wa kiume wala wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote, mwenzio alicho nacho!
18
Nao watu wote walipoziona zile ngurumo na umeme na mlio wa baragumu nao mlima uliotoka moshi, walipoviona hivi vyote wakakimbia, wakasimama mbali,
19
wakamwambia Mose: Sema wewe na sisi, nasi tutasikia! Lakini Mungu asiseme nasi, tusife.
20
Naye Mose akawaambia: Msiogope! Kwani Mungu amekuja kuwajaribu ninyi, kusudi mwone na macho yenu, anavyoogopesha, mwache kumkosea.
21
Kwa hiyo watu wakasimama mbali, lakini Mose akalikaribia lile wingu jeusi, Mungu alimokuwa.
22
Bwana akamwambia Mose: Hivi ndivyo, uwaambie wana wa Isiraeli: Ninyi mmeona, ya kuwa nimesema nanyi toka mbinguni.
23
Kwa hiyo msifanye vyo vyote kuwa Mungu kama mimi, msijifanyizie miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu!
24
Unijengee kwa udongo pa kunitambikia, upate pa kunitolea ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukruni za kondoo wako na za ng'ombe wako! Napo po pote, nitakapokukumbusha Jina langu, nitakuja kwako, nikubariki.
25
Nawe utakaponijengea kwa mawe pa kunitambikia, usitumie mawe ya kuchonga. Kwani ukiyapiga tu kwa chuma chako cho chote umekwisha kuyatia uchafu.
26
Tena usitumie ngazi ya kupapandia hapo pa kunitambikia, ni kwamba vyako vyenye soni visifunuliwe hapo pake.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40