bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 22
Exodus 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 23 →
1
Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, akimchinja au akimwuza, kwa ng'ombe mmoja sharti alipe ng'ombe watano, na kwa kondoo mmoja sharti alipe kondoo wanne.
2
Mwizi akikamatwa papo hapo, anapovunjia nyumba, akipigwa, afe, basi, siko kukora manza za damu.
3
Lakini kama jua lilikuwa limekwisha kucha tangu hapo, mwenye kumwua atakuwa amekora manza za damu. Mwizi hana budi kuyalipa aliyokwiba; akiwa hanayo malipo, na auzwe kwa ajili ya wizi wake.
4
Kama nyama, aliyemwiba, anapatikana mkononi mwake angali mzima, kama ni ng'ombe au punda au kondoo, sharti alipe wawili.
5
Mtu akilisha shamba au mizabibu, akiliacha kundi lake, lijiendee kulisha shambani kwa mwingine, sharti amlipe na kuyatoa mazao ya shamba lake yeye na ya mizabibu yake yeye yaliyo mema.
6
Moto ukitoka kwenye kuchoma miiba, ukala miganda iliyokwisha kufungwa au mabua yenye ngano au shamba lo lote, basi, mwenye kuuwasha huo moto sharti ayalipe yaliyoharibika.
7
Mtu akimpa mwenzake fedha au vyombo, amwekee, navyo vikiibiwa nyumbani mwa mwenzake, mwizi akionekana, sharti avilipe mara mbili.
8
Lakini mwizi asipoonekana, mwenye nyumba na apelekwe kwa Mungu, waone, kama siye mwenyewe aliyevichukua vyombo vya mwenzake kwa mkono wake.
9
Shauri lo lote, mtu atakalomshtakia mwenzake, kama ni la ng'ombe au la punda au la kondoo au la nguo au la cho chote kilichopotea, mmoja akisema, ni mali yake yeye, basi, shauri lao hao wawili lipelekwe kwa Mungu; naye, Mungu atakayemtokeza kuwa mwenye kukosa, sharti amlipe mwenzake mara mbili kilichompotea.
10
Mtu akimpa mwenzake ng'ombe au punda au kondoo au nyama wo wote wa kufuga, amtunzie, naye akafa au akaumia au akachukuliwa, mtu asione,
11
mwenyewe na amwapishe mwenzake, amtaje Bwana kwamba hakuchukua mali ya mwenzake kwa mkono wake, kisha yule, mwenzake hana budi kumwitikia, asilipe.
12
Lakini mwizi akimwiba kwake, sharti amlipe yule mwenyewe.
13
Akiraruliwa na nyama, sharti amlete huyo nyama aliyeraruliwa kuwa ushahidi; basi, hivyo hatamlipa aliyeraruliwa.
14
Mtu akikopa nyama kwa mwenzake, naye huyo nyama akiumia au akifa, bwana wake akiwa hayuko, yule hana budi kumlipa.
15
Kama bwana wake yuko hapo, halipi; kama alimkodisha huyo nyama, malipo yamo katika hizo fedha za kukodisha.
16
Mtu akimdanganya mwanamwali asiyeposwa, alale naye, sharti amlipie mali za ukwe, awe mkewe.
17
Baba yake akikataa kabisa kumpa kuwa mkewe, bsi, atatoa fedha zimpasazo mwanamwali za posa.
18
Mwanamke mlozi usimwache, awepo!
19
Kila atakayelala na nyama sharti auawe kabisa.
20
Mtu atakayetambikia miungu mingine, isipokuwa Bwana peke yake, sharti atiwe mwiko wa kuwapo.
21
Mgeni usimwonee wala usimkorofishe! Kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
22
Mjane au mtoto aliyefiwa na wazazi usimtese!
23
Utakapomtesa atanililia mimi, mimi nami nitakisikia vema kilio chake.
24
Ndipo, makali yangu yatakapowaka moto, niwaue ninyi kwa upanga, wake zenu wawe wajane, nao watoto wenu wasiwe na baba tena.
25
Ukiwakopesha fedha watu wa ukoo wangu, wakikaa kwako wenye ukosefu, usiwawie kama wakopeshaji wengine, ni kwamba: Msiwatoze faida kubwa za kukopesha!
26
Ukimtoza mwenzako blanketi lake kuwa rehani, sharti umrudishie, mpaka jua likichwa.
27
Kwani hulitumia la kujifunika, hili peke yake ni nguo yake ya kuufunika mwili wake; asipokuwa nalo atalalia nini? Naye atakaponililia, mimi nitamsikia, kwani mimi ni mwenye huruma.
28
Mungu usimtukane! Wala mtawala ukoo wako usimwambie maovu!
29
Usikawilie kutoa malimbuko ya vilaji vyako vingi na ya vinywaji vyako! Naye mwanao wa kwanza unipe, awe wangu!
30
vivyo hivyo sharti uvifanye hata kwa ng'ombe wako na kwa mbuzi na kondoo wako: wana wao wa kwanza na wakae na mama zao siku saba, siku ya nane uwatoe kunipa mimi!
31
Nanyi sharti mwe watu wangu watakatifu, msile nyama aliyeraruliwa porini, nyama zake sharti mwatupie mbwa.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40