bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 30
Exodus 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 31 →
1
Tengeneza nayo meza ya kuvukizia mavukizo, uitengeneze nayo kwa migunga.
2
Urefu wake uwe mkono mmoja, nao upana wake uwe mkono mmoja, pande zote nne ziwe sawa, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mikono miwili.
3
Uifunikize dhahabu tupu juu yake na kando yake pande zote na pembe zake, kisha uzungushe juu yake taji la dhahabu pande zote.
4
Kisha uitengenezee mapete mawili ya dhahabu, uyatie chini ya taji pande zake mbili penye mbavu zake mbili, yawe ya kutilia mipiko ya kuichukulia.
5
Nayo mipiko uitengeneze kwa migunga, kisha nayo uifunikize dhahabu.
6
Kisha uiweke upande wa huku wa pazia linaloning'inia na kulielekea Sanduku la ushahidi, mbele ya kiti cha upozi kilichoko juu yake Sanduku la Ushahidi nitakapokutana na wewe.
7
Naye Haroni na avukize juu yake mavukizo yanukayo vizuri; kila kunapokucha akizitengeneza taa za kinara na ayavukize.
8
Hata Haroni atakapoziwasha hizo taa saa za jioni na ayavukize tena, mavukizo yavukizwe mbele ya Bwana siku zote nao walio wa vizazi vyenu.
9
Msivukize juu yake manukato mageni, wala msitoe juu yake ng'ombe za tambiko za kuteketezwa wala kipaji cha tambiko.
10
Kila mwaka mara moja Haroni na azipatie upozi pembe zake kwa damu ya ng'ombe ya tambiko ya weuo; mara moja tu kila mwaka na aipatie upozi kwao walio wa vizazi vyenu, maana ni takatifu yenyewe kwa kuwa yake Bwana.
11
Bwana akamwambia Mose kwamba:
12
Ukivihesabu vichwa vyao wana wa Isiraeli, watakapokaguliwa, na wamtolee Bwana makombozi ya kuzikomboa roho zao, kila mtu yake kwa kukaguliwa, wasipatwe na pigo lo lote kwa kukaguliwa.
13
Kwa hiyo kila atakayefika kukaguliwa sharti atoe nusu ya sekeli, ndio fedha zitumikazo Patakatifu, ambazo sekeli moja ni gera ishirini, ndio fedha moja ya thumuni nane. Nusu ya fedha hiyo iwe kipaji cha tambiko cha kumnyanyulia Bwana.
14
Kila atakayefika kukaguliwa mwenye miaka ishirini na zaidi sharti mnyanyulie Bwana hicho kipaji cha tambiko.
15
Mwenye mali asilipe zaidi, wala mnyonge asiipunguze hiyo nusu ya fedha kuwa kipaji cha tambiko cha kumnyanyulia Bwana, wajipatie upozi.
16
Kisha uzichukue hizo fedha za mapoza, utakazowatoza wana wa Isiraeli, uzitumie za utumishi wa hema la Mkutano; ndivyo, zitakavyokuwa za kumkumbusha Bwana, awakumbuke wana wa Isiraeli, azipatie roho zenu upozi.
17
Bwana akamwambia Mose kwamba:
18
Tengeneza birika la shaba lenye wekeo lake la shaba, liwe la kuogea, uliweke katikati ya Hema la Mkutano na meza ya kutambikia, kisha ulitie maji.
19
Haroni na wanawe waoshe humo mikono na miguu yao.
20
Watakapoingia katika Hema la Mkutano wajiogeshe majini, wasife! Au watakapoikaribia meza ya Bwana, watumikie hapo na kumchomea Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa,
21
na waioshe mikono na miguu yao, wasife! Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwake na kwa wazao wake na kwa vizazi vyao.
22
Bwana akamwambia Mose kwamba:
23
Jichukulie manukato yaliyo mazuri mno: manemane mabichi sekeli 500, ndio ratli 20, tena nusu yao dalasini zinukazo vizuri sekeli 250, ndio ratli 10, tena vichiri vinukavyo vizuri sekeli 250, ndio ratli 10,
24
na karafuu sekeli 500, ndio ratli 20 zilizopimwa kwa mizani ya Patakatifu, tena pishi moja ya mafuta ya chekele.
25
Kisha uyatengeneze kuwa mafuta matakatifu ya kupaka kwa kuchanganya mafuta na manukato, kama mtengeneza manukato aliye fundi anavyojua kuyatengeneza, yapate kuwa kweli mafuta matakatifu ya kupaka.
26
Kisha kwa hayo mafuta ulipake Hema la Mkutano na Sanduku la Ushahidi,
27
na meza na vyombo vyake vyote na kinara na vyombo vyake na meza ya kuvukizia,
28
na meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko na vyombo vyake vyote na birika na wekeo lake,
29
uvitakase hivyo, vipate kuwa vitakatifu vyenyewe. Kisha kila atakayevigusa sharti awe ametolewa kuwa mtakatifu.
30
Naye Haroni na wanawe uwapake mafuta, uwatakase, wapate kuwa watambikaji wangu.
31
Nao wana wa Isiraeli uwaambie kwamba: Hayo mafuta ya kupaka sharti yawe matakatifu kwa vizazi vyenu, kwa kuwa ni yangu.
32
Msiyamiminie mwilini mwa mtu, wala msitengeneze yaliyo sawa kama hayo, kwani ndiyo matakatifu, nayo sharti yawe matakatifu kwenu.
33
Mtu atakayechanganya mafuta kuwa kama hayo au atakayeyapaka mtu mgeni sharti ang'olewe kwao walio ukoo wake.
34
Bwana akamwambia Mose: Chukua viungo vinukavyo vizuri: liwa na udi na sandarusi, ndio viungo vinukavyo vizuri, tena uvumba ulio safi, vyote viwe kipimo kimoja tu.
35
Uvitengeneze kuwa mavukizo, kama mtengeneza manukato aliye fundi anavyojua kuyatengeneza na kutia chumvi humo, yapate kutakata na kuwa matakatifu.
36
Kisha uchukue humo kidogo, uyaponde sana, yawe kama uvumbi, kisha uchukue humo kidogo kuyaweka mbele ya Sanduku la Ushahidi katika Hema la Mkutano, nitakamokutana na wewe. Hayo mavukizo sharti yawe kwenu matakatifu yenyewe.
37
Mavukizo mengine mtakayoyatengeneza, msiyatengeneze kuwa kama hayo, ila hayo sharti yawe matakatifu kwenu kwa kuwa yake Bwana.
38
Mtu atakayetengeneza mavukizo kama hayo ya kuyavukiza sharti ang'olewe kwao walio wa ukoo wake.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40