bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 15
Exodus 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 16 →
1
Hapo ndipo, Mose na wana wana Isiraeli walipomwimbia Bwana wimbo huu, wakasema kwamba: Na nimwimbie Bwana! Kwani ni mtukufu mno, Farasi pamoja nao waliowapanda amewatosa baharini.
2
Bwana ni uwezo wangu na wimbo wangu, hunipatia wokovu. Yeye ni Mungu wangu, kwa hiyo na nimsifu, ni Mungu wa baba yangu, kwa hiyo na nimtukuze!
3
Bwana ni mpiga vita, Bwana ni Jina lake.
4
Magari ya Farao na vikosi vyake amewabwaga baharini, wateule wake wakuu wametoswa katika Bahari Nyekundu;
5
vilindi vikawafunika, wakazama chini kama mawe.
6
Mkono wako wa kuume, Bwana, hutukuka kwa nguvu, unazozifanya, mkono wako wa kuume, Bwana, huwaponda adui.
7
Kwa wingi wa ukuu wako unawaangamiza wao wakuinukiao; ukiyafungua makali yako; huwateketeza kama majani makavu.
8
Kwa kufoka kwa pua yako maji yakakwezwa juu, mawimbi yakasimama, kama yamo chunguni. vilindi vikaganda moyoni mwa bahari.
9
Adui aliposema: Nijihimize kufuata! Nitafika, roho yangu itapata kushiba, nikigawanya nyara; nitauchomoa upanga wangu, mkono wangu uwaangamize:
10
ndipo, ulipouvumisha upepo wako, nayo bahari ikawafunikiza, wakazama kama risasi katika maji makuu.
11
Miongoni mwa miungu yuko nani anayefanana na wewe, Bwana? Yuko nani anayefanana na wewe kwa utukufu na kwa utakatifu? Anayetisha kwa matendo yanayoshangiliwa, naye akifanya vioja?
12
Ulipoukunjua mkono wako wa kuume, nchi ikawameza.
13
Umewaongoza kwa huruma yako hao watu, uliowakomboa, ukawafikisha kwa nguvu zako huko, utukufu wako unakokaa.
14
Makabila ya watu walipovisikia wakatetemeka; uchungu ukawapata wenyeji wa Ufilisti.
15
Ndipo, wakuu wa Edomu walipostuka nao, nao madume wa Moabu wakapigwa bumbuazi, nao wenyeji wa Kanaani wakayeyuka wote. Mastuko na maogofyo yakawaangukia,
16
wakanyamaza kimya kama mawe kwa ukuu wa mkono wako, mpaka wapite wao walio ukoo wako, Bwana, mpaka wapite wao wa ukoo huo, uliowakomboa.
17
Waingize na kuwapanda kwenye milima iliyo fungu lako, ulikotengeneza Kao la kukalia wewe Bwana, ililolisimika mikono yako, Bwana, kuwa Patakatifu.
18
Bwana atakuwa mfalme kale na kale.
19
Kwani farasi wa Farao na magari yake pamoja nao walioyapanda walipoingia baharini, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao, wana wa Isiraeli walipokwisha kupita pakavu katikati ya bahari.
20
Ndipo, mfumbuaji wa kike Miriamu, umbu lake Haroni, alipochukua patu mkononi mwake, nao wanawake wote wakatoka, wamfuate na kupiga patu na kucheza ngoma.
21
Naye Miriamu akawaitikia kwamba: Mwimbieni Bwana! Kwani ni mtukufu mno, Farasi pamoja nao waliowapanda amewatosa baharini!
22
Kisha Mose akawasafirisha Waisiraeli na kuwaondoa kwenye Bahari Nyekundu, wakatoka hapo, wakaingia katika nyika ya Suri, wakaenda siku tatu pasipo kuona maji.
23
Kisha wakafika Mara, lakini hawakuweza kuyanywa yale maji ya Mara, kwani yalikuwa machungu; kwa hiyo wakapaita mahali pale Mara (Uchungu).
24
Ndipo, watu walipomnung'unikia Mose kwamba: Tunywe nini?
25
Naye alipomlilia Bwana, Bwana akamwonyesha mti; alipoutupa mti huo majini, maji yakawa matamu. Hapo Bwana akawatolea maongozi yapasayo, akawajaribu hapo
26
akiwaambia: Kama utaisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yanyokayo machoni pake na kuyategea maagizo yake masiko yako na kuyaangalia maongozi yake yote, ndipo, utakapoona, ya kuwa sikutii yale magonjwa yote, niliyowatia Wamisri, kwani mimi Bwana ni mponya wako.
27
Kisha wakafika Elimu palipokuwa visima vya maji 12 na mitende 70, wakapiga makambi hapo penye maji.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40