bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 40
Exodus 40
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ulisimamishe Kao la Hema la Mkutano.
3
Humo ndani uliweke Sanduku la Ushahidi, kisha ulitungike pazia mbele ya Sanduku.
4
Kisha iingize meza na kuyatandika juu yake yanayopasa kuwekwa hapo, kisha kiingize kinara na kuziweka taa zake juu yake.
5
Kisha iweke meza ya dhahabu ya kuvukizia mbele ya Sanduku la Ushahidi na kulitungika pazia pa kuliingilia Kao.
6
Kisha iweke meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko mbele ya hapo pa kuliingilia Kao la Hema la Mkutano.
7
Kisha uliweke birika katikati ya hema la Mkutano na meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko na kulitia maji.
8
Kisha Kao ulizungushie ua na kulitungika guo la pazia la langoni kwa ua.
9
Kisha yachukue mafuta ya kupaka, ulipake Kao lenyewe nayo yote yaliyomo; ndivyo, ulieue pamoja na vyombo vyake vyote kuwa vitakatifu.
10
Kisha ipake mafuta meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, uieue, hiyo meza ya kutambikia ipate kuwa takatifu yenyewe.
11
Kisha birika lipake mafuta nalo wekeo lake, ulieue.
12
Kisha mwite Haroni nao wanawe, wafike hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, kisha waambie wajiogeshe majini.
13
Kisha umvike Haroni mavazi matakatifu na kumpaka mafuta; hivi ndivyo, utakavyomweua, apate kuwa mtambikaji wangu.
14
Kisha wafikishe wanawe karibu, uwavike shati,
15
kisha wapake nao mafuta, kama ulivyompaka baba yao mafuta, wapate kuwa watambikaji wangu. Huko kuwapaka mafuta kutawapatia utambikaji wa kale na kale kwa vizazi vyao.
16
Mose akayafanya yote; kama Bwana alivyomwagiza, ndivyo, alivyoyafanya yote sawasawa.
17
Ikawa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, ndipo, Kao liliposimamishwa.
18
Mose alipolisimamisha Kao akaiweka miguu yake, akatia humo mbao zake, akazitia misunguo yake na kuzisimamisha nguzo zake.
19
Kisha akaweka juu ya Hema chandalua chake, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
20
Kisha akauchukua ushahidi, akauweka Sandukuni, akatia nayo mipiko penye Sanduku, akakiweka Kiti cha Upozi juu ya Sanduku.
21
Kisha akaliingiza Sanduku Kaoni ndani, akalitungika lile guo kubwa la pazia, lilifiche Sanduku la Ushahidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
22
Kisha akapeleka meza ndani ya Hema la Mkutano, akaiweka upande wa kaskazini wa Kao nje ya pazia,
23
kisha akamwekea Bwana juu yake mikate na kuitandika mistari mistari, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
24
Kisha akakiweka kinara Hemani mwa Mkutano upande wa kusini wa Kao, kuielekea meza.
25
Kisha akaziweka taa zake juu yake mbele ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
26
Kisha akaiweka meza ya dhahabu ya kuvukizia katika Hema la Mkutano mbele ya pazia.
27
Akavukizia juu yake mavukizo yanukayo vizuri, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
28
Kisha akalitungika pazia hapo pa kuliingilia Kao.
29
Kisha akaiweka meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko penye kuliingilia Kao la Hema la Mkutano, akatoa juu yake ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
30
Kisha akaliweka birika katikati ya Hema la Mkutano na meza ya kutambikia na kutia humo maji ya kujioshea.
31
Kisha Mose na Haroni na wanawe wakajiosha humo mikono yao na miguu yao.
32
Kila walipoliingia Hema la Mkutano, napo kila walipoikaribia meza ya kutambikia wakajiosha, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
33
Kisha akausimamisha ua wa kulizunguka Kao na meza ya kutambikia, kisha akalitungika pazia langoni kwa ua. Ndivyo, Mose alivyozimaliza hizi kazi.
34
Kisha lile wingu likalifunika Hema la Mkutano, nao utukufu wa Bwana ukajaa Kaoni.
35
Naye Mose hakuweza kuliingia Hema la Mkutano, kwa kuwa wingu lililikalia, nao utukufu wa Bwana ulijaa Hemani.
36
Hilo wingu lilipoondoka penye Kao, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka kwenda safari yao; ndivyo, vilivyokuwa katika hizo safari zao zote.
37
Lakini wingu lisipoondoka, hawakuondoka nao kwenda safari mpaka siku hiyo, lilipoondoka tena.
38
Kwani wingu la Bwana lililikalia Kao mchana, lakini usiku ulikuwamo moto, nao wote walio wa mlango wa Isiraeli wakauona katika safari zao zote.
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40