bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 1
Numbers 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
1
Siku ya kwanza ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri Bwana akamwambia Mose katika nyika ya Sinai Hemani mwa Mkutano kwamba:
2
Toeni jumla yao wote walio mkutano wa wana wa Isiraeli kwa ndugu zao na kwa milango ya baba zao, mkiyahesabu majina ya wana waume wote kichwa kwa kichwa.
3
Kuanzia kwao wenye miaka ishirini na zaidi wewe na Haroni mwakague wote pia wanaoweza kwenda vitani kwao Waisiraeli, kikosi kwa kikosi.
4
Tena mchukue kuwa nanyi kwa kila shina moja mtu mmoja aliye kichwa chao walio wa mlango wa baba yake.
5
Nayo haya ndiyo majina yao, ninaowataka, wasimame pamoja nanyi: wa Rubeni Elisuri, mwana wa Sedeuri;
6
wa Simeoni Selumieli, mwana wa Surisadai;
7
wa Yuda Nasoni, mwana wa Aminadabu;
8
wa Isakari Netaneli, mwana wa Suari;
9
wa Zebuluni Eliabu, mwana wa Heloni;
10
wa wana wa Yosefu: wa Efuraimu Elisama, mwana wa Amihudi, wa Manase Gamulieli, mwana wa Pedasuri;
11
wa Benyamini Abidani, mwana wa Gideoni;
12
wa Dani Ahiezeri, mwana wa Amisadai;
13
wa Aseri Pagieli, mwana wa Okrani;
14
wa Gadi Eliasafu, mwana wa Deueli;
15
wa Nafutali Ahira, mwana wa Enani.
16
Hawa ndio wateule wa mkutano walio wakuu wa mashina ya baba zao, nao ndio waliokuwa vichwa vya maelfu ya Waisiraeli.
17
Mose na Haroni wakawachukua watu hawa waliotajwa majina yao,
18
wakaukusanya mkutano wote siku ya kwanza ya mwezi wa pili; ndipo, walipoandikwa katika vitabu vya vizazi kwa ndugu zao na kwa milango ya baba zao; yakahesabiwa kichwa kwa kichwa majina yao waliokuwa wenye miaka ishirini na zaidi;
19
kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, alivyowakagua nyikani kwa Sinai.
20
Wana wa Rubeni, mwanawe wa kwanza wa Isiraeli, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina kichwa kwa kichwa, waume wote wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
21
jumla yao wa shina la Rubeni walikuwa watu 46500.
22
Wana wa Simeoni, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, walipokaguliwa na kuhesabiwa majina kichwa kwa kichwa, waume wote wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
23
jumla yao wa shina la Simeoni walikuwa watu 59300.
24
Wana wa Gadi, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
25
jumla yao wa shina la Gadi walikuwa watu 45650.
26
Wana wa Yuda, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwanda vitani,
27
jumla yao wa shina la Yuda walikuwa watu 74600.
28
Wana wa Isakari, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
29
jumla yao wa shina la Isakari walikuwa watu 54400.
30
Wana wa Zebuluni, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
31
jumla yao wa shina la Zebuluni walikuwa watu 57400.
32
Wanawe Yosefu wana wa Efuraimu, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
33
jumla yao wa shina la Efuraimu walikuwa watu 40500.
34
Wana wa manase, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
35
jumla yao wa shina la Manase walikuwa watu 32200.
36
Wana wa Benyamini, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
37
jumla yao wa shina la Benyamini walikuwa watu 35400.
38
Wana wa Dani, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
39
jumla yao wa shina la Dani walikuwa watu 62700.
40
Wana wa Aseri, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
41
jumla yao wa shina la Aseri walikuwa watu 41500.
42
Wana wa Nafutali, vizazi vyao vya udugu wao na vya milango ya baba zao, yalipohesabiwa majina yao wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani,
43
jumla yao wa shina la Nafutali walikuwa watu 53400.
44
Hizi ndizo jumla zao, nao waliowakagua ni Mose na Haroni na wale wakuu kumi na wawili wa Waisiraeli waliokuwa kila mmoja wa milango ya baba zao.
45
Nao wana wa Isiraeli wote wa milango ya baba zao waliokaguliwa kuwa wenye miaka ishirini na zaidi, wao wote walioweza kwenda vitani kwao Waisiraeli,
46
jumla yao yote walikuwa watu 603550.
47
Lakini Walawi hawakuhesabiwa katikati yao kwa hivyo, shina la baba zao lilivyokuwa.
48
Bwana akamwambia Mose kwamba:
49
Wao wa shina la Lawi usiwakague, wala jumla yao usiitie katika hiyo ya wana wa Isiraeli.
50
Ila utawaweka Walawi kuliangalia Kao l Ushahidi na vyombo vyake vyote nayo yote yaliyomo. Wao ndio watakaolichukua kao na vyombo vyake vyote, nao ndio watakaolitumikia, nao wakipiga makambi yao, hayo na yalizunguke.
51
Kao litakapoondoka, wao Walawi ndio watakaolishusha chini; tena Kao litakapofika makambini, Walawi ndio watakaolisimamisha; lakini mgeni atakayelikaribia hana budi kuuawa.
52
Wana wa Isiraeli watakapopiga makambi, kila mtu na apige hema katika kambi lake penye bendera ya kikosi cha kwao.
53
Lakini Walawi na wapige makambi kulizunguka Kao la Ushahidi, makali yangu yasiwajie wao wa mkutano wa wana wa Isiraeli; kwa hiyo Walawi na wangoje zamu ya kuliangalia Kao la Ushahidi.
54
Wana wa Isiraeli wakayafanya yote; kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, walivyofanya kuwa sawasawa.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36