bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 19
Numbers 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 20 →
1
Bwana akawambia Mose na Haroni kwamba:
2
Haya ndiyo maongozi ya mafunzo, Bwana aliyoyaagiza kwamba: Waambie wana wa Isiraeli, wakupatie ng'ombe mwekundu jike asiye na kilema wala doadoa lo lote, asiyefungwa bado kuvuta gari.
3
Kisha mpe mtambikaji Elazari, ampeleke kufika nje ya makambi, ndipo wamchinje machoni pake.
4
Kisha mtambikaji Elazari achukue kwa kidole chake damu yake kidogo, ainyunyizie mara saba hapo panapolielekea Hema la Mkutano.
5
Kisha wamteketeze machoni pake, nao sharti wateketeze ngozi yake na nyama zake na damu yake pamoja na mavi yake.
6
Naye mtambikaji na achukue kipande cha mwangati na kivumbasi na nyuzi nyekundu, azitupe katika huo moto unaomteketeza huyo ng'ombe.
7
Kisha mtambikaji na azifue nguo zake pamoja na kuuogesha mwili wake majini, kisha aingie makambini, lakini atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
8
Naye aliyemteketeza sharti azifue nguo zake majini na kuuogesha mwili wake majini, lakini naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
9
Kisha mtu mwenye kutakata na ayazoe majivu yake huyo ng'ombe, ayaweke nje ya makambi mahali palipo penye kutakata, yakae hapo hapo na kuangaliwa, yawe tayari, mkutano wa wana wa Isiraeli watakapoyatumia ya kutengeneza maji ya kunyunyiza, kwani ni ng'ombe ya tambiko ya weuo.
10
Naye aliyeyazoa hayo majivu ya huyo ng'ombe sharti azifue nguo zake, lakini atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni. Haya yawe maongozi ya kale na kale kwa wana wa Isiraeli na kwa wageni watakaokaa ugenini katikati yao.
11
Atakayegusa mfu wa mtu ye yote atakuwa mwenye uchafu siku saba.
12
Naye ajieue kwa yale maji ya kunyunyiza siku ya tatu, ndipo, atakapokuwa siku ya saba mwenye kutakata; lakini asipojieua siku ya tatu wala siku ya saba hatakuwa mwenye kutakata.
13
Kila mtu atakayegusa mfu, ni kwamba maiti ya mtu ye yote aliyekufa, asipojieua hulichafua Kao la Bwana; mtu aliye hivyo sharti ang'olewe kwao Waisiraeli. Kwa kuwa hakunyunyiziwa hayo maji ya kunyunyiza, ni mwenye uchafu, nao huo uchafu wake utamkalia vivyo hivyo.
14
Nayo haya maonyo sharti yaangaliwe, mtu akifa hemani: kila atakayeingia humo hemani naye kila atakayekuwamo humo hemani atakuwa mwenye uchafu siku saba.
15
Nacho kila chombo kilicho wazi kisichofunikwa na kifuniko cha kukifungia kabisa ni chenye uchafu.
16
Hata kila mtu atakayegusa porini mtu aliyeuawa kwa upanga au mfu au mfupa wa mtu au kaburi atakuwa mwenye uchafu siku saba.
17
Mtu akiwa mwenye uchafu hivyo, na wachukue majivu machache ya hiyo ng'ombe ya weuo iliyoteketezwa, wayatie chomboni, kisha watie humo maji ya mtoni.
18
Kisha mtu mwenye kutakata na achukue kivumbasi, akichovye katika hayo maji, ayanyunyizie lile hema na vyombo vyote vilivyomo nao watu wote waliokuwamo naye yule mtu aliyegusa mfupa wa mzoga wa mtu aliyeuawa kwa upanga au mfu au kaburi.
19
Ndivyo, mwenye kutakata atakavyomnyunyizia mwenye uchafu siku ya tatu na siku ya saba; akiisha kumweua hiyo siku ya saba sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, ndivyo, atakavyokuwa jioni mwenye kutakata.
20
Lakini mtu akiwa mwenye uchafu pasipo kujieua, basi, aliye hivyo hana budi kung'olewa katika mkutano huu, kwani hupachafua Patakatifu pa Bwana, kwani asiponyunyiziwa hayo maji ya kunyunyiza, ni mwenye uchafu vivyo hivyo.
21
Haya yawe kwao maongozi ya kale na kale. Naye yule aliyemnyunyizia mwenzake hayo maji ya kunyunyiza sharti azifue nguo zake. Naye atakayeyagusa hayo maji ya kunyunyiza atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
22
Navyo vyote, mwenye uchafu atakavyovigusa, vitakuwa vyenye uchafu, naye kila mtu, atakayemgusa, atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36