bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 13
Numbers 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 14 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Tuma watu kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani, mimi ninayotaka kuwapa wana wa Isiraeli. Kila shina la baba zao na litoe mtu mmoja, mtakayemtuma, nao wote wawe wakuu kwao.
3
Kwa kuagizwa na Bwana Mose akawatuma kutoka kule nyikani kwa Parani, nao watu hao wote walikuwa vichwa vya wana wa Isiraeli.
4
Nayo haya ndiyo majina yao: wa shina la Rubeni Samua, mwana wa Zakuri,
5
wa shina la Simeoni Safati, mwana wa Hori,
6
wa shina la Yuda Kalebu, mwana wa Yefune,
7
wa shina la Isakari Igali, mwana wa Yosefu,
8
wa shina la Efuraimu Hosea, mwana wa Nuni,
9
wa shina la Benyamini Palti, mwana wa Rafu,
10
wa shina la Zebuluni Gadieli, mwana wa Sodi,
11
wa shina la Yosefu wa shina la Manase Gadi, mwana wa Susi,
12
wa shina la Dani Amieli, mwana wa Gemali,
13
wa shina la Aseri Seturi, mwana wa Mikaeli,
14
wa shina la Nafutali Nabi, mwana wa Wofusi,
15
wa shina la Gadi Gueli, mwana wa Maki.
16
Haya ndiyo majina ya wale watu, Mose aliowatuma kuipeleleza nchi. Lakini Hosea, mwana wa Nuni, Mose akamwita Yosua.
17
Mose alipowatuma kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani akawaambia: Pandeni huku kusini, kisha mpande milimani.
18
Mwitazame hiyo nchi, ilivyo, nao watu wanaokaa huko, kama ni wanguvu, au kama ni wanyonge, kama ni wachache, au kama ni wengi.
19
Itazameni hiyo nchi, wale watu wanayoikaa, kama ni jema, au kama ni mbaya, nayo miji, wale watu wanayoikaa, itazameni, itazameni, kama ni makambikambi tu, au kama ni miji yenye maboma.
20
Nchi itazameni, kama ni yenye wiva, au kama haizai, kama iko miti, au kama hakuna. Tena jipeni mioyo, mchukue matunda ya nchi hiyo! Nazo siku zile zilikuwa siku za malimbuko ya mizabibu.
21
Kisha wakaenda kupanda huko, wakaipeleleza nchi toka nyika ya Sini mpaka Rehobu kwenye njia ya kwenda Hamati.
22
Kisha wakapanda upande wa nchi ya kusini, wakafika Heburoni; ndiko, walikokaa Ahimani, Sesai na Talmai, wana wa Anaki. Nao Heburoni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.
23
Walipofika penye kijito cha Eskoli, wakakata huko tawi la mzabibu lenye kichala, wakalichukua mpikoni watu wawili, wakachukua hata komamanga na kuyu.
24
Mahali pale wakapaita Kijito cha Eskoli (Kichala) kwa ajili ya hicho kichala, wana wa Isiraeli walichokikata huko.
25
siku 40 zilipopita, wakarudi, kwa kuwa walikwisha kuipeleleza hiyo nchi.
26
Wakaja, wakafika kwa Mose na Haroni na kwa mkutano wote wa wana wa Isiraeli katika nyika ya Parani kule Kadesi, wakawasimulia wao nao mkutano wote waliyoyaona, wakawaonyesha nayo yale matunda ya hiyo nchi.
27
Wakawasimulia kwamba: Tumeiingia nchi, mliyotutuma, ichuruzikayo maziwa na asali, nayo haya ni matunda yake.
28
Lakini wale wanaokaa katika hiyo nchi wako na nguvu, nayo miji yao ni mikubwa sana yenye maboma magumu; nao wana wa Anaki tumewaona huko.
29
Waamaleki wanakaa katika nchi ya kusini; nao Wahiti na Wayebusi na Waamori wanakaa milimani, nao Wakanaani wanakaa upande wa baharini na kando ya Yordani.
30
Naye Kalebu akawatuliza mioyo wale watu mbele ya Mose akisema: Haya! Na tupande, tuichukue hiyo nchi! Kwani tutaweza kuishinda kabisa.
31
Lakini wale watu wengine waliopanda naye wakasema: Hatuwezi kupanda, tupigane na hao watu, kwani ndio wenye nguvu kuliko sisi.
32
Wakazidi kuisingizia nchi ile, waliyoipeleleza, wakiwaambia wana wa Isiraeli: Hiyo nchi, tuliyoipita kuipeleleza, ndiyo nchi inayowala wenyeji wake, nao watu wote, tuliowaona huko, ni watu warefu mno.
33
Huko tumeona hata wale Majitu, ni wana wa Anaki wa mlango wa hao Majitu, nasi tukawa machoni petu kama panzi, tena ndivyo, tulivyokuwa machoni pao.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36