bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 33
Numbers 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 34 →
1
Hizi ndizo safari za wana wa Isiraeli, vikosi vyao vilipotoka katika nchi ya Misri, wakiongozwa na Mose na Haroni.
2
Mose akaziandika hizo safari zao, kama walivyotoka na kuondoka kwa kuagizwa na Bwana, nayo haya ndiyo matuo yao, walipoondoka kwendelea katika safari zao:
3
siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, ndiyo siku ya pili ya Pasaka, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi machoni pao Wamisri wote kwa nguvu za mkono uliotoka juu.
4
Nao Wamisri walikuwa wakiwazika wana wao wote wa kwanza, Bwana aliowapiga kwao, kwani Bwana aliihukumu miungu yao.
5
Wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi wakapiga makambi Sukoti.
6
Walipoondoka sukoti wakapiga makambi Etamu ulioko kwenye mapeo ya nyika.
7
Walipoondoka Etamu wakarudi Pi-Hahiroti unaoelekea Baali-Sefoni, wakapiga makambi mbele ya Migidoli.
8
Walipoondoka mbele yake Hahiroti wakapita katikati ya bahari, wakaingia nyikani; walipokwenda safari ya siku tatu katika nyika ya Etamu wakapiga makambi Mara.
9
Walipoondoka Mara wakafika Elimu; nako huko Elimu kulikuwa na visima vya maji 12 na mitende 70; kwa hiyo walipiga makambi huko.
10
Waalipondoka Elimu wakapiga makambi kwenye Bahari Nyekundu.
11
Walipoondoka kwenye Bahari Nyekundu wakapiga makambi nyikani kwa Sini.
12
Walipoondoka nyikani kwa Sini wakapiga makambi Dofuka.
13
Walipoondoka Dofuka wakapiga makambi Alusi.
14
Walipoondoka Alusi wakapiga makambi Refidimu; huko ndiko, watu walikokosa maji ya kunywa.
15
Walipoondoka Refidumu wakapiga makambi nyikani kwa Sinai.
16
Walipoondoka nyikani kwa Sinai wakapiga makambi kwenye Makaburi ya Uchu.
17
Walipoondoka kwenye Makaburi ya Uchu, wakapiga makambi Haseroti.
18
Walipoondoka Haseroti wakapiga makambi Ritima.
19
Walipoondoka Ritima wakapiga makambi Rimoni-Peresi.
20
Walipoondoka Rimoni-Peresi wakapiga makambi Libuna.
21
Walipoondoka Libuna wakapiga makambi Risa.
22
Walipoondoka Risa wakapiga makambi Kehelata.
23
Walipoondoka Kehelata wakapiga makambi mlimani kwa Seferi.
24
Walipoondoka mlimani kwa Seferi wakapiga makambi Harada.
25
Walipoondoka harada wakapiga makambi Makeloti.
26
Walipoondoka Makeloti wakapiga makambi Tahati.
27
Walipoondoka Tahati wakapiga makambi Tara.
28
Walipoondoka Tara wakapiga makambi Mitika.
29
Walipoondoka Mitika wakapiga makambi Hasimona.
30
Walipoondoka Hasimona wakapiga makambi Moseroti.
31
Walipoondoka Moseroti wakapiga makambi kwa wana wa Yakani.
32
Walipoondoka kwa wana wa Yakani wakapiga makambi Hori-Hagidigadi.
33
Walipoondoka Hori-Hagidigadi wakapiga makambi Yotibata.
34
Walipoondoka Yotibata wakapiga makambi Aburona.
35
Walipoondoka Aburona wakapiga makambi Esioni-Geberi.
36
Walipoondoka Esioni-Geberi wakapiga makambi nyikani kwa Sini, ndio Kadesi.
37
Walipoondoka Kadesi wakapiga makambi mlimani kwa Hori kwenye mwisho wa nchi ya Edomu.
38
Ndipo, mtambikaji Haroni alipopanda mlimani kwa Hori kwa kuagizwa na Bwana, akafa huko siku ya kwanza ya mwezi wa tano katika mwaka wa arobaini tangu hapo, wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri;
39
naye alikuwa mwenye miaka 123, alipokufa mlimani kwa Hori.
40
Ndipo, Aradi, mfalme wa Kanaani, aliposikia, ya kuwa wana wa Isiraeli wanakuja; maana alikaa upande wa kusini wa nchi ya Kanaani.
41
Walipoondoka mlimani kwa Hori wakapiga makambi Salmona.
42
Walipoondoka Salmona wakapiga makambi Punoni.
43
Walipoondoka Punoni wakapiga makambi Oboti.
44
Walipoondoka Oboti wakapiga makambi Iye-Abarimu mpakani kwa Moabu.
45
Walipoondoka huko Iyimu wakapiga makambi Diboni wa Gadi.
46
Walipoondoka Diboni wa Gadi wakapiga makambi Almoni-Dibulataimu.
47
Walipoondoka Almoni-Dibulataimu wakapiga makambi milimani kwa Abarimu kunakoelekea Nebo.
48
Walipoondoka milimani kwa Abarimu wakapiga makambi kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
49
Huko Yordani ndiko, walikopiga makambi kutoka Beti-Yesimoti mpaka Abeli-Sitimu kwenye mbuga za Moabu.
50
Bwana akamwambia Mose huko kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba:
51
Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapouvuka Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani.
52
sharti mwafukuze mbele yenu wenyeji wote wa nchi hiyo, kisha myaharibu mawe yao yote yenye machorochoro ya kuyaangukia, navyo vinyago vyao vyote vilivyoyeyushwa sharti mviharibu, napo pao pote pa kutambikia vilimani sharti mpabomoe.
53
Kisha mtaichukua hiyo nchi, mkae huko, kwani nimewapa ninyi nchi hiyo, mwichukue, iwe yenu.
54
Nayo nchi mtaigawanyia ndugu zenu kwa kupiga kura; ndugu walio wengi mwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache mwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao. Huko, kura itakakomwangukia kila mtu, kutakuwa kwake; sharti mgawiane mafungu yenu kwa mashina ya baba zao.
55
Lakini msipowafukuza mbele yenu wenyeji wa nchi hiyo, basi, hao mtakaowasaza watakuwa miiba machoni penu na machomo mbavuni penu, wawasonge ninyi katika nchi, mtakayoikaa ninyi.
56
Mwisho utakuwa, niwafanyizie ninyi yaleyale, niliyoyawaza kuwafanyizia wao.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36