bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 9
Numbers 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 10 →
1
Bwana akamwambia Mose nyikani kwa Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili tangu hapo, walipotoka katika nchi ya Misri kwamba:
2
Wana wa Isiraeli na waitengeneze kondoo ya Pasaka, siku zake zilizowekwa zitakapotimia.
3
Siku ya kumi na nne ya huu mwezi wakati wa jioni mwitengeneze saa zizo hizo zilizowekwa, myafuate maongozi yake yote na desturi zake zote zipasazo. Mwitengeneze vivyo hivyo.
4
Kwa hiyo Mose akawaambia wana wa Isiraeli, waitengeneze kondoo ya Pasaka.
5
Nao wakaitengeneza kondoo ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wakati wa jioni kule nyikani kwa Sinai; yote, Bwana aliyomwagiza Mose, wana wa Isiraeli wakayafanya vivyo hivyo sawasawa.
6
Wakawako watu waliokuwa wenye uchafu kwa ajili ya kufiwa; kwa hiyo hawakuweza kuitengeneza kondoo ya Pasaka siku hiyo, wakamtokea Mose na Haroni siku hiyo.
7
Hao watu wakawaambia: Sisi tu wenye uchafu kwa ajili ya kufiwa; mbona tunakatazwa kumtolea Bwana matoleo katikati ya wana wa Isiraeli siku hiyo iliyowekwa?
8
Mose akawaambia: Ngojeni, nisikie, Bwana atakayoyaagiza kwa ajili yenu.
9
Bwana akamwambia Mose kwamba:
10
Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Kila mtu wa kwenu au wa vizazi vyenu, kama ni mwenye uchafu kwa kufiwa au kama yuko mbali safarini, naye ataweza kuitengeneza kondoo ya Pasaka ya Bwana.
11
Na aitengeneze siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili wakati wa jioni, tena na waile pamoja na mikate isiyochachwa na mboga zenye uchungu.
12
Lakini wasisaze nyama mpaka kesho, tena watu wasivunje mifupa, ila waile na kuyafuata maongozi yote ya Pasaka.
13
Lakini mtu asipokuwa mwenye uchafu, wala asipokuwa safarini, akiacha tu kuitengeneza kondoo ya Pasaka, mtu aliye hivyo sharti ang'olewe kwao walio ukoo wake, kwani hakumtolea Bwana matoleo siku hiyo iliyowekwa. Mtu aliye hivyo sharti atwikwe kosa lake.
14
Kama kwenu atakuwako mgeni, naye akitaka kuitengeneza kondoo ya Pasaka ya Bwana, basi, na aitengeneze na kuyafuata maongozi ya Pasaka na desturi zake ziipasazo; maongozi ya kwenu yawe yaleyale, nayo huwapasa wageni na wenyeji wa nchi hiyo.
15
Siku hiyo, walipolisimamisha Kao, lile wingu likalifunika Kao kuwa juu yake Hema la Ushahidi; lakini jioni likaonekana juu ya Kao kuwa kama moto mpaka asubui.
16
Vikawa hivyo siku zote: hilo wingu lililifunika Kao, tena usiku likaonekana kuwa kama moto.
17
Napo, hilo wingu lilipoondoka penye Hema, likiisha, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka kwenda safari yao; napo mahali, hilo wingu lilipotua, ndipo, wana wa Isiraeli walipopiga makambi.
18
Hivyo wana wa Isiraeli waliondoka kusafiri kwa kuagizwa na Bwana, tena kwa kuagizwa na Bwana walipiga makambi. Siku zote, hilo wingu lilipokaa juu ya Kao, nao walikaa makambini.
19
Napo hapo, wingu lilipokawilia na kukaa siku nyingi juu ya Kao, wana wa Isiraeli wakamwangalia Bwana, kama ilivyowapasa kumwangalia, lakini hawakuondoka kwenda safari yao.
20
Wingu lilipokuwa juu ya Kao siku chache tu, walikaa makambini kwa kuagizwa na Bwana; tena kwa kuagizwa na Bwana waliondoka kwenda safari yao.
21
Wingu lilipokaa tu toka jioni hata asubuhi, kisha wingu lilipoondoka asubuhi, nao waliondoka kwenda safari yao; au lilipokaa tu mchana na usiku pamoja, basi, hapo wingu lilipoondoka, nao waliondoka kwenda safari yao.
22
Lakini wingu lilipokaa juu ya Kao siku mbili au mwezi au siku nyingi zaidi, nao wana wa Isiraeli walikaa makambini, hawakuondoka kwenda safari yao; lakini lilipoondoka, nao waliondoka kwenda safari yao.
23
Hivyo walikaa makambini kwa kuagizwa na Bwana, tena waliondoka kwenda safari yao kwa kuagizwa na Bwana. Ndivyo, walivyomwangalia Bwana, kama ilivyowapasa kuyaangalia, Bwana atakayoyaagiza kinywani mwa Mose.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36