bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 10
Numbers 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 11 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Jifanyizie matarumbeta mawili ya fedha, nayo uyatengeneze kwa kufuafua fedha, uyatumie kuwa ya kuwaitia wao wa mkutano, tena ya kuwatangazia, wavunje makambi.
3
Yatakapopigwa yote mawili, watu wote wakusanyike kwako hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
4
Lakini litakapopigwa moja tu, na wakusanyike kwako wakuu tu walio vichwa vyao maelfu ya Waisiraeli.
5
Lakini mtakapoyapiga kwa sauti kuu za kushangilia, makambi yaliyoko upande wa maawioni kwa jua na yavunjwe.
6
Mtakapoyapiga mara ya pili kwa sauti kuu za kushangilia, makambi yaliyoko upande wa kusini na yavunjwe. Yatakapopigwa kwa sauti kuu za kushangilia yatakuwa ya kuvunjia makambi.
7
Lakini kwa kuukusanya mkutano mtayapiga tu pasipo kuzitumia sauti kuu za kushangilia.
8
Nao wana wa Haroni walio watambikaji ndio watakaoyapiga hayo matarumbeta. Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwenu na kwa vizazi vyenu.
9
Napo hapo, mtakapokwenda vitani katika nchi yenu kupigana na adui watakaowasonga, na mshangilie na kuyapiga hayo matarumbeta; ndipo, mtakapokumbukwa mbele ya Bwana Mungu wenu, mwokolewe katika adui zenu.
10
Nazo siku za furaha zenu na za sikukuu zenu na za miandamo ya mwezi na myapige, mkizitoa ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukrani; ndipo, yatakaposaidia, mkumbukwe mbele ya Mungu wenu. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
11
Ikawa siku ya ishirini ya mwezi wa pili katika mwaka wa pili, ndipo, lile wingu lilipoondoka penye Kao la Ushahidi.
12
Nao wana wa isiraeli wakaondoka kwenda safari yao na kutoka nyikani kwa Sinai, nalo wingu likatua tena katika nyika ya Parani.
13
Kama Bwana alivyoviagiza kinywani mwa Mose, ndivyo, wa kwanza walivyoondoka.
14
Kwanza ikaondoka bendera ya makambi ya wana wa Yuda, vikosi kwa vikosi, naye mkuu wa vikosi vyao alikuwa Nasoni, mwana wa Aminadabu.
15
Naye mkuu wa shina la wana wa Isakari alikuwa Netaneli, mwana wa Suari.
16
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Zebuluni alikuwa Eliabu, mwana wa Heloni.
17
Kisha Kao likashushwa, nao wana wa Gersoni na wana wa Merari wakaondoka na kulichukua Kao.
18
Kisha bendera ya makambi ya Rubeni ikaondoka, vikosi kwa vikosi, naye mkuu wa vikosi vyao alikuwa Elisuri, mwana wa Sedeuri.
19
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Simeoni alikuwa Selumieli, mwana wa Surisadai.
20
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Gadi alikuwa Eliasafu, mwana wa Deueli.
21
Kisha wakaondoka Wakehati wakivichukua vyombo vitakatifu; hao walipofika, wale walikuwa wamekwisha kulisimamisha Kao.
22
Kisha bendera ya makambi ya wana wa Efuraimu ikaondoka, vikosi kwa vikosi, naye mkuu wa vikosi vyao alikuwa Elisama, mwana wa Amihudi.
23
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Manase alikuwa Gamulieli, mwana wa Pedasuri.
24
Nye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Benyamini alikuwa Abidani, mwana wa Gideoni.
25
Kisha bendera ya makambi ya wana wa Dani ikaondoka, vikosi kwa vikosi; nao walikuwa wanyuma wa makambi yote, naye mkuu wa vikosi vyao alikuwa Ahiezeri, mwana wa Amisadai.
26
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Aseri alikuwa Pagieli, mwana wa Okrani.
27
Naye mkuu wa vikosi vya shina la wana wa Nafutali alikuwa Ahira, mwana wa Enani.
28
Hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyokwenda safarini, vikosi kwa vikosi, walipoondoka kwenda safari yao.
29
Mose akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli wa Midiani, mkwewe Mose: Sisi tunaondoka kwenda mahali, Bwana aliposema: Hapo ndipo, nitakapowapa ninyi; nenda pamoja nasi, tutakufanyizia mema, kwani Bwana amewaambia wana wa Isiraeli, ya kuwa atawapa mema.
30
Lakini akamwambia: Sitakwenda, ila nitarudi kwetu kwa ndugu zangu wa kuzaliwa nao.
31
Akamjibu: Usituache! Kwa kuwa unajua mahali, tunapoweza kupiga makambi nyikani, kwa hiyo utakuwa kama macho yetu sisi.
32
Ukienda na sisi, tutakufanyizia mema yote, Bwana atakayotufanyizia sisi.
33
Walipoondoka mlimani kwa Bwana, wakasafiri siku tatu, nalo Sanduku la Agano la Bwana likawatangulia safari ya hizo siku tatu, liwatafutie mahali pa kupumzikia.
34
Nalo wingu la Bwana lilikuwa juu yao mchana, walipoondoka makambini.
35
Kila mara Sanduku lilipoondoka, Mose akasema: Inuka, Bwana, adui zako watawanyike, nao wachukivu wako waukimbie uso wako!
36
Tena lilipotua husema: Rudi, Bwana, kwenye maelfu na maelfu ya Isiraeli!
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36