bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 31
Numbers 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Walipizie wana wa Isiraeli kwa Wamidiani! Kisha utachukuliwa kwenda kwao walio ukoo wako.
3
Ndipo, Mose alipowaambia watu kwamba: Tengenezeni watu wa kwenu kwenda vitani, wawaendee Wamidiani kumpatia Bwana lipizo kwao Wamidiani!
4
Kwao mashina ya Waisiraeli kila shina moja litoe watu elfu moja na kuwatuama kwenda vitani.
5
Kwa hiyo wakatolewa katika maelfu ya Waisiraeli elfu moja katika kila shina, wakawa watu maelfu kumi na mawili waliotengenezwa kwenda vitani.
6
Hayo maelfu, elfu moja la kila shina, Mose akawatuma kwenda vitani pamoja na Pinehasi, mwana wa mtambikaji Elazari; huyu alishika mkononi mwake vyombo vya Patakatifu nayo yale matarumbeta ya shangwe.
7
Wakaenda vitani kupigana na adui, kama Bwana alivyomwagiza Mose, wakawaua wa kiume wote.
8
Nao wafalme wa Wamidiani wakawaua pamoja na watu wao waliouawa: Ewi na Rekemu na Suri na Huri na Reba; hao watano ndio waliokuwa wafalme wao Wamidiani. Naye Bileamu, mwana wa Beori, wakamwua kwa upanga.
9
Kisha wana wa Isiraeli wakawateka wanawake wa Midiani na watoto wao, nao ng'ombe wao wote na mbuzi na kondoo wao wote na mali zao zote pia wakazichukua kuwa nyara zao.
10
Lakini miji yao yote, walimokaa, na makambi yenye mahema yao wakayateketeza kwa moto.
11
Kisha wakawachukua nyama wote na mateka yote, watu pamoja na nyama,
12
wote pia wakawapeleka kwa Mose na kwa mtambikaji Elazari na kwao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli; mateka na mapato ndiyo, waliyoyapeleka pamoja na nyara makambini kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani; ndipo hapo, Yeriko ulipokuwa ng'ambo ya pili.
13
Ndipo, Mose na mtambikaji Elazari na wakuu wote wa mkutano walipotoka kwenda kukutana nao huko nje ya makambi.
14
Lakini Mose akawakasirikia waliowekwa kuvisimamia vikosi, wale wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia waliotoka kwa kupiga vita;
15
kwa hiyo Mose akawaambia: Kumbe mmewaponya wanawake wote!
16
Nao ndio walioongozwa na Bileamu, wakawakosesha wana wa Isiraeli, wamvunjie Bwana maagano kwa ajili ya Peori, nao wa mkutano wa Bwana wakapatwa na pigo kwa sababu hiyo.
17
Sasa waueni watoto wa kiume wote! Nao wanawake wote wanaojua waume kwa kulala nao wa kiume waueni nao!
18
Lakini watoto wa kike wote wasiojua bado kulala nao wa kiume waponyeni, wakae kwenu!
19
Kisha ninyi laleni nje ya makambi siku saba, ninyi nyote mlioua mtu nanyi mliogusa tu mtu aliyeuawa, mjieue siku ya tatu na siku ya saba, ninyi wenyewe pamoja na mateka yenu.
20
Nazo nguo zote navyo vyombo vyote vya ngozi navyo vyote vilivyotengenezwa kwa manyoya ya singa za mbuzi navyo vyombo vyote vya mti sharti mvieue.
21
Naye mtambikaji Elazari akawaambia askari waliotoka kwa kupiga vita: Haya ndiyo maongozi ya maonyo, Bwana aliyomwagiza Mose:
22
vilivyo dhahabu na fedha na shaba na vyuma na mabati na risasi,
23
navyo vyote vinavyoweza kuingia motoni sharti mvipitishe motoni, vipate kutakata, kisha mvieue kwa yale maji ya kunyunyiza; lakini vyote visivyopatana na moto na mvipitishe majini.
24
Kisha sharti mzifue nguo zenu siku ya saba; ndipo, mtakapokuwa wenye kutakata, baadaye mtaingia makambini.
25
Bwana akamwambia Mose kwamba:
26
Toa jumla yao mateka, waliyoyapata ya watu na ya nyama, wewe pamoja na mtambikaji Elazari nao wakuu wa milango ya mkutano!
27
Kisha hayo mapato uyatoe mafungu mawili, moja liwe lao walioshika kazi ya mapigano na kwenda vitani, la pili liwe lao wengine wote wa mkutano.
28
Kisha wao waliokwenda kupiga vita uwatoze toleo limpasalo Bwana: kwa kila mia tano mmoja, kama ni watu au ng'ombe au punda au mbuzi au kondoo.
29
Hivyo ndivyo, utakavyowatoza katika nusu yao, umpe mtambikaji Elazari kuwa vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana.
30
Lakini katika nusu yao wana wa Isiraeli uchukue mmoja na kumtoa katika kila hamsini, kama ni watu au ng'ombe au punda au mbuzi au kondoo; katika nyama wote utoe hivyo, uwape Walawi wanaongoja zamu ya kuliangalia Kao la Bwana.
31
Ndipo, Mose na mtambikaji Elazari walipofanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
32
Masao ya nyara, watu wa vita walizozichukua, mapato hayo yalikuwa mbuzi na kondoo pamoja 675000,
33
na ng'ombe 72000,
34
na punda 61000.
35
Nao wana wa kike wasiojua bado kulala na mtu wa kiume wote pamoja walikuwa 32000.
36
kwa hiyo ile nusu iliyokuwa fungu lao waliokwenda vitani, hesabu ya mbuzi na kondoo ilikuwa 337500.
37
Nalo toleo lililompasa Bwana la hao mbuzi na kondoo lilikuwa 675.
38
Nao ng'ombe wao walkuwa 36000, nalo toleo lao lililompasa Bwana lilikuwa ng'ombe 72.
39
Nao punda walikuwa 30500, nalo toleo lao lililompasa Bwana lilikuwa 61.
40
Nao watu wao walikuwa 16000, nalo toleo lao lililompasa Bwana lilikuwa watu 32.
41
Hayo matoleo Mose akampa mtambikaji Elazari kuwa vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
42
Nayo nusu nyingine ya wana wa Isiraeli, Mose aliyoiondoa kwao waliokwenda kuvipiga hivyo vita,
43
hiyo nusu iliyokuwa yao wa mkutano ilikuwa nayo mbuzi na kondoo 337500,
44
nao ng'ombe walikuwa 36000,
45
nao punda walikuwa 30500,
46
nao watu walikuwa 16000.
47
Katika nusu hii ya wana wa Isiraeli Mose akachukua mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, kama ni watu au nyama, akawapa Walawi waliongoja zamu ya kuliangalia Kao la Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
48
Kisha waliowekwa kuyasimamia maelfu ya vikosi, wale wakuu wa maelfu na wa mamia wakamkaribia Mose,
49
wakamwambia Mose: Sisi watumishi wako tumetoa jumla ya watu wa vita, tuliowashika mikononi mwetu, namo miongoni mwao hakukoseka hata mmoja.
50
Kwa hiyo tunamtolea Bwana vyombo vya dhahabu, kila mtu alivyoviona kuwa matoleo: vikuku na vitimbi na pete za vidoleni na mapete ya masikioni na mapambo yo yote, tujipatie upozi mbele ya Bwana.
51
Mose na mtambikaji Elazari wakachukua kwao hizo dhahabu zilizotengenezwa kuwa hivyo vyombo vyote.
52
Nazo dhahabu zote, walizomtolea Bwana kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa zilikuwa frasila kumi na saba, ndizo zilizotoka kwa wakuu wa maelfu na kwa wakuu wa mamia.
53
Nao waliokuwa askari tu walijichukulia kila mtu nyara zake.
54
Mose na mtambikaji Elazari walipokwisha kuzichukua hizo dhahabu kwao wakuu wa maelfu na wa mamia wakazipeleka Hemani wa Mkutano, ziwe za kumkumbusha Bwana, asikoe kuwatazama wana wa Iiraeli.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36