bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 30
Numbers 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
1
Mose akawaambia wakuu wa mashia ya wana wa Isiraeli kwamba: Hili ndilo neno, Bwana aliloliagiza:
2
Mtu akimwapia Bwana kumtolea cho chote au kiapo cha kujifungia kifungo cho chote, asilitangue neno lake, ila sharti ayafanye yote, kama kinywa chake kilivyoyasema.
3
Mwanamke akimwapia Bwana kumtolea cho chote, au akijifungia kiungo, akingali nyumbani mwa baba yake, au akingali kijana bado,
4
naye baba yake akipata habari ya kule kuapa kwake au ya kujifungia kifungo cho chote, basi, baba yake akimnyamazia kimya, yote aliyoyaapa yatakuwapo, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, vitakuwa vimemfunga.
5
Lakini baba yake akimkataza siku hiyo, anapopata habari, basi, yote aliyoyaapa navyo vifungo vyote, alivyojifungia, havitakuwapo, naye Bwana atamwondolea jambo hilo, kwa kuwa baba yake amemkataza.
6
Lakini atakapoolewa akiwa mwenye mambo, aliyoyaapa, au midomo yake iliyojisemea tu ya kjifungia kifungo,
7
basi, mumewe akipata habari na kumnyamazia kimya siku hiyo, anapopata habari, yatakuwapo aliyoyaapa, navyo vifungo, alivyojifungia, vitakuwapo.
8
Lakini mumewe akimkataza siku hiyo, anapopata habari, basi, yeye atakuwa ameyatangua hayo mambo, aliyokuwa nayo kwa kuapa, nayo yale, midomo yake iliyojisemea tu ya kujifungia kifungo, naye Bwana atamwondolea jambo hilo.
9
Lakini mjane au mwanamke aliyeachana na mumewe atakayoyaapa navyo vifungo vyote, atakavyojifungia, vitakuwapo, vimfunge.
10
Mwanamke akijiapia mambo yo yote nyumbani mwa mumewe au akijifungia kifungo cho chote kwa kiapo,
11
basi, mumewe akipata habari yake na kumnyamazia kimya, asimkataze, yote aliyoyaapa yatakuwapo, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, vitakuwapo.
12
Lakini mumewe akivitangua kabisa siku hiyo, anapopata habari, basi, yote yaliyotoka midomoni mwa mkewe ya kiapo nayo ya kujifungia kifungo hayatakuwapo, kwa kuwa mumewe ameyatangua, naye Bwana atamwondolea jambo hilo.
13
Yote, mwanamke aliyoyaapa, navyo vifungo vyote, alivyojifungia kwa kiapo vya kujiumiza mwenyewe, mumewe anaweza kuyatia nguvu, yawepo, tena mumewe anaweza kuyatangua.
14
Mumewe akimnyamazia kimya tangu leo hata kesho, basi, amekwisha kuyatia nguvu, yawepo yote, aliyoyaapa, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, amekwisha kuvitia nguvu navyo, viwepo, kwani amemnyamazia kimya siku hiyo, alipopata habari.
15
Naye akiisha kupata habari, tena akivitangua siku za nyuma hana budi kujitwika manza za mkewe.
16
Haya ndiyo maongozi, Bwana aliyomwagiza Mose ya kuwaongoza mtu na mkewe, hata baba na mwanawe wa kike, akiwa angaliko kijana na kukaa nyumbani mwa baba yake.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36