bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 4
Numbers 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 5 →
1
Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
2
Fanyeni hesabu ya wana wa Kehati na kuwatoa kwao wana wa Lawi walio wa udugu wao wa milango ya baba zao.
3
Wao wa miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini ndio wanaofaa wote kuuingia utumishi huo, wafanye kazi za humo Hemani mwa Mkutano.
4
Nazo kazi za utumishi za wana wa Kehati za humo Hemani mwa Mkutano ziwe za Patakatifu Penyewe.
5
Makambi yatakapovunjwa, Haroni na wanawe na waingie Hemani, walishushe lile guo kubwa la pazia, wafunike nalo Sanduku la Ushahidi.
6
Kisha waweke juu yake blanketi la ngozi za pomboo, juu yake tena watandaze nguo nyeusi iliyo ya kifalme yote nzima, kisha na walitie mipiko yake.
7
Hata meza yenye mikate ya kuwa usoni pa Bwana na waifunike kwa nguo nyeusi ya kifalme na kuweka juu yake vyano na vijiko na vikombe na madumu ya vinywaji vya tambiko, nayo mikate, wasiyokoma kumwekea Bwana, sharti iwe juu yake.
8
Kisha na watandaze nguo nyekundu ya kifalme, kisha waifunike kwa blanketi la ngozi za pomboo, kisha na waitie mipiko yake.
9
Kisha na wachukue nguo nyeusi ya kifalme, wakifunike kinara kiangazacho pamoja na taa zake na koleo zake na makato yake na vyombo vyake vyote vya mafuta, wanavyovitumia vya kazi yake.
10
Kisha na wakifunike pamoja na vyombo vyake vyote kwa blanketi la ngozi za pomboo, kisha na wakiweke juu ya miti ya kukichukulia.
11
Kisha watandaze nguo nyeusi ya kifalme juu ya meza ya dhahabu ya kuvukizia, kisha waifunike kwa blanketi la ngozi za pomboo na kuitia mipiko yake.
12
Kisha na wachukue vyombo vyote, wanavyovitumia Patakatifu, wavifunge katika nguo nyeusi ya kifalme na kuvifunika tena kwa blanketi la ngozi za pomboo, kisha waviweke juu ya miti ya kuvichukulia.
13
Kisha na wazoe majivu mezani pa kuteketezea ng'ombe za tambiko, kisha watandaze juu yake nguo nyekundu ya kifalme.
14
Kisha na waweke juu yake vyombo vyake vyote, wanavyovitumia wakifanya kazi za hapo, sinia na nyuma na majembe na vyano na vyombo vyote vya meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, wavifunike juu kwa blanketi la ngozi za pomboo, kisha na waitie mipiko yake.
15
Haroni na wanawe watakapokwisha kupafunika Patakatifu na vyombo vyake vyote wakitaka kuvunja makambi, ndipo, wana wa Kehati watakapoingia kuvichukua, lakini wasiguse vitu vitakatifu, wasife. Hii ndiyo mizigo yao wana wa Kehati, watakayoichukua Hemani mwa Mkutano.
16
Tena kazi yake Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, ni kuyaangalia mafuta ya kinara na mavukizo yanukayo vizuri na vilaji vya tambiko vya kila siku na mafuta ya kupaka, tena kuliangalia Kao lote zima na vyote vilivyomo ndani ya Patakatifu, maana ndivyo vyombo vyake.
17
Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
18
Angalieni, shina la udugu wa Wakehati lisitoweke kwao Walawi!
19
Ila yafanyeni haya, wapate kuwapo, wasife, watakapopakaribia Patakatifu Penyewe: Kwanza Haroni na wanawe na waingie, kisha wawaweke kila mtu penye kazi yake na kumpa mzigo wake.
20
Lakini wasiingie kamwe kupatazama tu Patakatifu, ijapo iwe kitambo kidogo kabisa, wsife.
21
Bwana akamwambia Mose kwamba:
22
Fanya hesabu ya wana wa Gersoni nao walio wa milango ya baba zao na wa udugu wao.
23
Uwakague walio wenye miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, ndio wanaofaa wote kuuingia utumishi, wafanye kazi za kutumikia Hemani mwa Mkutano.
24
Hizi ndizo kazi zao walio wa udugu wa Gersoni za kutumika na za kuchukua mizigo:
25
na wayachukue mazulia ya Kao, na Hema la Mkutano na chandalua chake na chandalua cha ngozi za pomboo kilichoko juu yake na pazia la hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano,
26
na nguo za uani na pazia la hapo pa kuingia langoni kwa ua, unaolizunguka Kao na meza ya kuteketezea ng'ombe ya tambiko, na kamba zao na vyombo vyote vya utumishi wao, nayo yote yapasayo kufanywa nao na wayafanye.
27
Utumishi wote wa wana wa Gersoni, kama ni kuichukua mizigo iwapasayo yote, au kama ni kuzifanya kazi ziwapasazo zote, ufanyike kwa kuagizwa na Haroni na wanawe; ninyi mwaweke kwa kuzignlia kazi za mizigo yao yote.
28
Hizi ndizo kazi za utumishi wao walio wa udugu wa wana wa Gersoni wa kutumikia Hemani mwa Mkutano, naye atakayewaangalia ni Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni.
29
Uwakague nao wana wa Merari walio wa udugu wao wa milango ya baba zao:
30
uwakague walio wa miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, ndio wanaofaa wote kuuingia utumishi, wafanye kazi za kutumikia Hemani mwa Mkutano.
31
Hizi ndizo kazi zao za kuiangalia mizigo yao, nao huo ndio utumishi wao wote wa kufanya Hemani mwa Mkutano: kuzichukua mbao za Kao na misunguo yake na nguzo zake na miguu yake,
32
na nguzo zinazouzunguka au na miguu yao na mambo zao na kamba zao na vyombo vyao vyote, wafanye yote yaupasayo utumishi wao. Navyo vyombo vya kuviangalia, wakivichukua, mwape na kuvitaja kila kimoja jina lake.
33
Hizi ndizo kazi za utumishi wao walio wa udugu wa wana wa Merari, wazifanye za kutumikia Hemani mwa Mkutano, naye mkuu wao awe Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni.
34
Kwa hiyo Mose na Haroni na wakuu wa mkutano wakawakagua wana wa Kehati walio wa udugu wao na wa milango ya baba zao;
35
waliokuwa wenye miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, ndio waliofaa wote kuuingia utumishi, wafanye kazi za kutumikia Hemani mwa Mkutano.
36
Jumla yao walio wa udugu wao walikuwa watu 2750.
37
Hii ndiyo jumla yao wote wa udugu wa Wakehati waliotumikia Hemani mwa Mkutano, Mose na Haroni waliowakagua kwa amri, Bwana aliyompa Mose.
38
Wana wa Gersoni wakakaguliwa nao walio wa udugu wao na wa milango ya baba zao,
39
waliokuwa wenye miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, ndio waliofaa wote kuuingia utumishi, wafanye kazi za kutumikia Hemani mwa Mkutano.
40
Jumla yao walio wa udugu wao na wa milango ya baba zao walikuwa watu 2630.
41
Hii ndiyo jumla yao wote wa udugu wa wana wa Gersoni waliotumikia Hemani mwa Mkutano, Mose na Haroni waliowakagua kwa amri ya Bwana.
42
Ndugu za wana wa Merari wakakagulia nao walio wa udugu wao na wa milango ya baba zao,
43
waliokuwa wenye miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, ndio waliofaa wote kuuingia utumishi, wafanye kazi za kutumikia Hemani mwa Mkutano.
44
Jumla yao walio wa udugu wao walikuwa watu 3200.
45
Hii ndiyo jumla yao walio wa udugu wa wana wa Merari, Mose na Haroni waliowakagua kwa amri, Bwana aliyompa Mose.
46
Hawa ndio Walawi wote waliokaguliwa, Mose na Haroni na wakuu wa Waisiraeli waliowakagua, waliokuwa wa udugu wao na wa milango ya baba zao,
47
ndio waliokuwa wenye miaka thelathini na zaidi mpaka miaka hamsini, nao ndio wote waliofaa kufanya kazi za kuutumikia huo utumishi nao utumishi wa kuchukua mizigo Hemani mwa Mkutano.
48
Jumla yao walikuwa watu 8580.
49
Kwa amri, Bwana aliyompa Mose, aliwakagua na kumweka kila mtu mmoja penye kazi yake ya utumishi na penye mzigo wake wa kuuchukua; nao wakawekwa vivyo hivyo, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36