bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 7

← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 8 →
1
Ikawa siku hiyo, Mose alipokwisha kulisimamisha Kao na kulipaka mafuta na kulieua kuwa takatifu pamoja na vyombo vyake vyote na kuipaka mafuta nayo meza ya kutambikia pamoja na vyombo vyake vyote na kuvieua kuwa vitakatifu,
2
ndipo, wakuu wa Waisiraeli waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao walipovitoa vipaji vyao vya tambiko, kwa kuwa wakuu wa mashina waliowasimamia wale waliokaguliwa.
3
Wakayaleta hayo matoleo yao, wakatoa mbele ya Bwana magari sita yenye mafuniko na ng'ombe kumi na wawili, kila wakuu wawili wakitoa gari moja, na kila mkuu mmoja akitoa ng'ombe mmoja; hapo mbele ya Kao ndipo, walipoyatoa.
4
Bwana akamwambia Mose kwamba:
5
Yachukue kwao, nayo yatumiwe kuusaidia utumishi wa Hema la Mkutano. Uwape Walawi, kila mtu kama kazi ya utumishi wake ilivyo.
6
Mose akayachukua hayo magari pamoja na ng'ombe, akawapa Walawi.
7
Magari mawili na ng'ombe wanne akawapa wana wa Gersoni kwa hivyo, utumishi wao ulivyokuwa.
8
Magari manne na ng'ombe wanane akawapa wana wa Merari kwa hivyo, utumishi wao ulivyokuwa, Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni, aliousimamia.
9
Lakini wana wa Kehati hakuwapa, kwani utumishi wao ulikuwa wa Pataktifu, hawakuwa na budi kuvichukua vyombo vyake mabegani.
10
Kisha wakuu wakatoa vipaji vya weuo wa meza ya kutambikia siku hiyo, ilipopakwa mafuta; ndipo, wakuu walipoyatoa matoleo yao mbele ya meza ya kutambikia.
11
Bwana akamwambia Mose: Kila mkuu mmoja awe na siku yake, nayo hiyo siku yake ndipo kila mkuu mmoja ayatoe matoleo yake ya weuo wa meza ya kutambikia.
12
Aliyeyatoa matoleo yake siku ya kwanza alikuwa Nasoni, mwana wa Aminadabu, wa shina la Yuda.
13
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
14
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho ilikuwa kimejaa mavukizo;
15
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
16
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
17
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Nasoni, mwana wa Aminadabu.
18
Siku ya pili Netaneli, mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, akaleta vipaji vyake.
19
Matoleo yake, aliyoyatoa, yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwambamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
20
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
21
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
22
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
23
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Netaneli, mwana wa Suari.
24
Siku ya tatu Eliabu, mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zebuluni, akaleta vipaji vyake.
25
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilukuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
26
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
27
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
28
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
29
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Eliabu, mwana wa Heloni.
30
Siku ya nne Elisuri, mwana wa Sedeuri, mkuu wa wana wa Rubeni, akaleta vipaji vyake.
31
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
32
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
33
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
34
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
35
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Elisuri, mwana wa Sedeuri.
36
Siku ya tano Selumieli, mwana wa Surisadai, mkuu wa wana wa Simeoni akaleta vipaji vyake.
37
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
38
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
39
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
40
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
41
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Selumieli, mwana wa Surisadai.
42
Siku ya sita Eliasafu, mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi, akaleta vipaji vyake.
43
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
44
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
45
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
46
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
47
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Eliasafu, mwana wa Deueli.
48
Siku ya saba Elisama, mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efuraimu, akaleta vipaji vyake.
49
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
50
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
51
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
52
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
53
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Elisama, mwana wa Amihudi.
54
Siku ya nane Gamulieli, mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase, akaleta vipaji vyake.
55
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
56
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
57
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima;
58
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo;
59
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Gamulieli, mwana wa Pedasuri.
60
Siku ya tisa Abidani, mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini, akaleta vipaji vyake.
61
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
62
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikukwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
63
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
64
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
65
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Abidani, mwana wa Gideoni.
66
Siku ya kumi Ahiezeri, mwana wa Amisadai, mkuu wa wana wana wa Dani, akaleta vipaji vyake.
67
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
68
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
69
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
70
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo;
71
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Ahiezeri mwana wa Amisadai.
72
Siku ya kumi na moja Pagieli, mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Aseri, akaleta vipaji vyake.
73
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
74
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
75
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
76
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
77
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo wa mwaka mmoja na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Pagieli, mwana wa Okrani.
78
Siku ya kumi na mbili Ahira, mwana wa Enani, mkuu wa wana wa Nafutali, akaleta vipaji vyake.
79
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
80
tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;
81
tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,
82
tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,
83
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Ahira, mwana wa Enani.
84
Hivi vilikuwa vipaji, wakuu wa Waisiraeli walivyovitoa vya weuo wa meza ya kutambikia siku hiyo, ilipopakwa mafuta: mabakuli yaa fedha 12 na vyano vya fedha 12 na vijiko vya dhahabu 12.
85
Kila bakuli moja kiasi chake kilikuwa fedha 130, kila chano kimoja kiasi chake kilikuwa fedha 70; jumla ya fedha za hivi vyombo ilikuwa fedha 2400, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu.
86
Vijiko vya dhahabu vilivyojaa mavukizo vilikuwa 12, kila kijiko kimoja kiasi chake kilikuwa vipande kumi vya dhahabu, ndio fedha 180; dhahabu zote za hivyo vijiko vilikuwa vipande 120, ndio fedha 2160.
87
Jumla ya ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima ilikuwa: madume 12 ya ng'ombe, mmadume 12 ya kondoo, wana kondoo wa mwaka mmoja 12 pamoja na vilaji vyao vya tambiko; tena madume 12 ya mbuzi kuwa ng'ombe za tambiko za weuo.
88
Nayo jumla ya ng'ombe za tambiko za shukrani ilikuwa: Ng'ombe 24, madume 60 ya kondoo, wana mbuzi 60, wana kondoo 60 wa mwaka mmoja; hivi vilikuwa vipaji vya weuo wa meza ya kutambikia, ilipokwisha kupakwa mafuta.
89
Kisha kila mara Mose alipoingia Hemani mwa Mkutano kusema na Bwana alisikia, sauti yake ikisema naye toka hapo penye Kiti cha Upozi kilicholifunika Sanduku la Ushahidi, nayo ilitoka katikati ya Makerubi, ikasema naye.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36