bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 20
Numbers 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 21 →
1
Mkutano wote wa wana wa Isiraeli walipofika katika nyika ya Sini katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadesi. Ndiko, Miriamu alikokufa; kisha akazikwa huko.
2
Wao wa mkutano wasipoona maji huko, wakamkusanyikia Mose na Haroni,
3
wakamgombeza Mose wakimwambia kwamba: Afadhali tungalizimia roho pamoja na ndugu zetu waliozimia roho mbele ya Bwana!
4
Kwa nini mmelileta kundi lake Bwana katika nyika hii, tujifie pamoja na nyama wetu wa kufuga?
5
Kwa nini mlitutoa Misri, mkatuleta mahali hapa pabaya? Huku hatuwezi kupanda mbegu, tena hakuna mikuyu wala mizabibu wala mikomamanga, wala maji tu ya kunywa hayako huku.
6
Mose na Haroni wakatoka hapo, walipokusanyika, wakaenda hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; napo hapo, walipoanguka kifudifudi, utukufu wa Bwana ukawatokea.
7
Bwana akamwambia Mose kwamba:
8
Ichukue ile fimbo! Kisha wewe na kaka yako Haroni wakusanyeni wao wote wa mkutano, mseme na mwamba huu machoni pao wote, ndipo, utakapowapa maji yake. Ndivyo, utakavyowatolea maji humu mwambani, uwanyweshe wao wa mkutano pamoja na nyama wao wa kufuga.
9
Mose akaichukua fimbo iliyokuwa mbele ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.
10
Kisha Mose na Haroni wakalikusanya kundi la watu mbele ya mwamba, akawaambia: Sikieni, ninyi msiotii! Itakuwaje? Tutaweza kuwatolea ninyi maji humu mwambani?
11
Kisha Mose akauinua mkono wake, akaupiga mwamba kwa fimbo yake mara mbili; ndipo, maji yalipotoka mengi, wao wa mkutano wakanywa wenyewe nao nyama wao wa kufuga.
12
lakini Bwana akamwambia Mose naye Haroni: Kwa kuwa hamkunitegemea na kunitakasa machoni pao wana wa Isiraeli, kwa hiyo hamtaliingiza kundi hili katika ile nchi, nitakayowapa.
13
Maji yale yakaitwa Meriba (Magomvi), kwa kuwa wana wa Isiraeli waligombana na Bwana, naye akajitokeza kwao kuwa mtakatifu.
14
Kule Kadesi Mose akatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu kwamba: Hivi ndivyo, ndugu yako Isiraeli anavyosema: Wewe unayajua masumbuko yote yaliyotupata:
15
baba zetu walishuka Misri, wakakaa huko siku nyingi, nao Wamisri wakatufanyizia mabaya sisi na baba zetu.
16
Tulipomlilia Bwana, akatusikia, akatuma malaika, akatutoa Misri. Tazama, sisi tumo humo Kadesi, ndio mji wa mpakani kwenye nchi yako.
17
Sasa tunataka kupita katika nchi yako, lakini hatutaki kupita mashambani wala mizabibuni, wala hatutakunywa maji ya visimani, ila tunataka kuishika njia ya mfalme tu, tusiiache kwenda kuumeni wala kushotoni, hata tuupite mpaka wako mwingine.
18
Lakini Mwedomu akamwambia: Hutapita kwangu. Ila nitatoka mwenye upanga, nipigane na wewe.
19
Wana wa Isiraeli wakamwambia: Tunataka kushika njia tu, tena tukinywa maji yako sisi na nyama wetu wa kufuga tutakulipa; hakuna jingine, tunalolitaka, ila kupita tu kwa miguu yetu.
20
Lakini akasema: Huna ruhusa kupita. Kisha Waedomu wakatoka wenye watu wengi na wenye mikono ya nguvu, wawazuie.
21
Ndivyo, Waedomu walivyowakataza Waisiraeli kupita mipakani kwao; ndipo, Waisiraeli walipogeuka, washike njia ya kupitia kando yao.
22
Kisha wana wa Isiraeli wakaondoka Kadesi, wakafika mkutano wao wote kwenye mlima wa Hori.
23
Huko kwenye mlima wa Hori kwenye mipaka ya nchi ya Edomu Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
24
Sasa Haroni atachukuliwa, awe pamoja nao walio wa ukoo wake, kwani hataingia katika nchi ile, nitakayowapa wana wa Isiraeli, kwa kuwa mlikibishia kinywa changu kwenye Maji ya Magomvi.
25
Mchukue Haroni pamoja na mwanawe Elazari, uwapeleke mlimani kwa Hori juu.
26
Huko umvue Haroni mavazi yake, umvike mwanawe Elazari! Kisha Haroni atachukuliwa, afe huko.
27
Mose akafanya, kama Bwana alivyomwagiza, wakaupanda mlima wa Hori machoni pao wote walio wa mkutano.
28
Kisha Mose akamvua Haroni mavazi yake, akamvika mwanawe Elazari; ndipo, Haroni alipokufa huko juu mlimani, kisha Mose na Elazari wakashuka mlimani.
29
Wote wa mkutano walipoona, ya kuwa Haroni amekwisha kufa, wakamwombolezea Haroni siku thelathini wao wote wa mlango wa Isiraeli.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36