bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 27
Numbers 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 28 →
1
Wakaja wana wa kike wa Selofuhadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, waliokuwa wa ndugu za Manase, mwana wa Yosefu, majina yao hawa wanawe wa kike ndiyo haya: Mala na Noa na Hogla na Milka na Tirsa.
2
Hao wakamtokea Mose na mtambikaji Elazari na wakuu wa mkutano wote hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, wakasema:
3
Baba yetu alikufa nyikani, naye hakuwa katika mkutano wao waliofanya shauri la kumpingia Bwana katika mkutano wao Wakora, ila alikufa kwa ukosaji wake yeye, lakini hakuwa na wana wa kiume.
4
Mbona jina la baba yetu litoweke katika ndugu zake, kwa kuwa hakuwa na mwana wa kiume? Tupe sisi fungu katikati ya ndugu za baba yetu, tulichukue!
5
Mose akalitokeza hilo shauri lao mbele ya Bwana.
6
Naye Bwana akamwambia Mose kwamba:
7
Haya, wana wa kike wa Selofuhadi waliyoyasema, ndiyo ya kweli. Uwape katikati ya ndugu za baba yao fungu, walichukue, liwe lao, ukiagiza, fungu la baba yao walipate wao.
8
Nao wana wa Isiraeli waambie kwamba: Mtu akifa pasipo kuwa na mwana wa kiume, fungu lake huyu sharti mmwachie mwanawe wa kike.
9
Kama hata mwana wa kike hakuwa naye, mtawapa ndugu zake fungu lake.
10
Kama hata ndugu hakuwa nao, mtawapa ndugu za baba yake fungu lake.
11
Kama baba yake hakuwa na ndugu, basi, hilo fungu lake mtampa ye yote aliye ndugu yake wa kuzaliwa naye wa mlango wake, alichukue. Haya na yawe kwao wana wa Isiraeli maongozi yenye haki, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
12
Bwana akamwambia Mose: Panda huku juu mlimani kwa Abarimu, uitazame hiyo nchi, nitakayowapa wana wa Isiraeli.
13
Ukiisha kuiona utachukuliwa nawe kwenda kwao walio ukoo wako, kama kaka yako Haroni alivyochukuliwa naye kwenda huko.
14
Ni kwa kuwa nyikani kwa Sini hamkukitii vema kinywa changu cha kwamba: Mnitakase kwa kutoa maji machoni pao, mkutano huu uliponigombeza; hayo yalikuwa penye Maji ya Magomvi kule Kadesi nyikani kwa Sini.
15
Naye Mose akamwambia Bwana kwamba:
16
Bwana wangu aliye mwenye roho zao wote walio wenye miili na aweke mtu kuwa mkuu wa mkutano huu,
17
atakayewatangulia kwa kutoka na kuingia kwake, atakayewaongoza wao, wapate kutoka na kuingia tena, watu wa mkutano huu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.
18
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Mchukue Yosua, mwana wa Nuni, aliye mtu mwenye Roho yangu moyoni mwake, umbandikie mkono kichwani pake!
19
Kisha msimamishe mbele ya mtambikaji Elazari machoni pao walio wa mkutano huu, umwagizie mambo yako machoni pao
20
na kumgawia utukufu wako, umkalie naye, watu wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wamsikie.
21
Itakapotukia, na amtokee mtambikaji Elazari, ampigie bao na kuutumia Urimu mbele ya Bwana, kama desturi; utakaposema, watoke, sharti watoke, tena utakaposema, waingie, sharti waingie, yeye na wana wote wa Isiraeli pamoja naye, huo mkutano wote pia.
22
Mose akafanya, kama Bwana alivyomwagiza: akamchukua Yosua, akamsimamisha mbele ya mtambikaji Elazari na mbele ya mkutano wote.
23
Kisha akambandikia mikono yake kichwani pake, akamwagizia mambo yake, kama Bwana alivyosema kinywani mwa Mose.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36