bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 3
Numbers 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
1
Hivi ndivyo vizazi vya Haroni na vya Mose vya siku zile, Bwana aliposema na Mose mlimani kwa Sinai.
2
Haya ndiyo majina ya wanawe Haroni: wa kwanza ni Nadabu, tena Abihu na Elazari na Itamari.
3
Haya ndiyo majina ya wanawe Haroni waliopakwa mafuta kuwa watambikaji na kujazwa magao yao, wapate kufanya kazi ya utambikaji.
4
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Bwana walipomtolea Bwana moto mgeni wa mavukizo nyikani kwa Sinai, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo Elazari na Itamari walifanya kazi ya utambikaji na kuangaliwa na baba yao Haroni.
5
Bwana akamwambia Mose kwamba:
6
Wafikishe hawa wana wa shina la Lawi, uwasimamishe mbele ya mtambikaji Haroni, wamtumikie.
7
Tena na waziangalie hizo kazi zinazompasa yeye kuziangalia, nazo kazi zinazoupasa mkutano wote kuziangalia mbele ya hema la Mkutano na kuutumikia utumishi wa Kaoni.
8
Na waviangalie vyombo vyote vya Hema la Mkutano na kuziangalia kazi zinazowapasa wana wa Isiraeli kuziangalia na kuutumikia utumishi wa kaoni.
9
Hawa Walawi umpe Haroni na wanawe, wawe vipaji vyao walivyopewa na wana wa Isiraeli.
10
Nao akina Haroni na wanawe uwaweke kuuangalia utambikaji wao. Lakini mgeni atakayejitia humo hana budi kuuawa.
11
Bwana akasema na Mose kwamba:
12
Tazama, mimi nimewachagua Walawi na kuwatoa katikati ya wana wa Isiraeli kuwa makombozi ya wana watakaozaliwa wa kwanza na mama zao kwa wana wa Isiraeli, kwa hiyo Walawi watakuwa wangu.
13
Kwani wana wa kwanza wote ni wangu, kwani siku hiyo, nilipompiga kila mwana wa kwanza katika nchi ya Misri, nilijitakasia kila mwana wa kwanza kwa Waisiraeli, kama ni wa mtu au kama ni wa nyama wa kufuga, wawe wangu mimi Bwana.
14
Bwana akamwambia Mose nyikani kwa Sinai kwamba:
15
Wakague wana wa Lawi milango ya baba zao mlango kwa mlango na udugu kwa udugu ukiwahesabu waume wote walio wenye mwezi mmoja na zaidi.
16
Kisha Mose akawakagua kwa hiyo amri ya bwana, kama alivyoagizwa.
17
Nao wana wa lawi walikuwa hawa kwa majina yao: Gersoni na Kehati na Merari.
18
Nayo haya ndiyo majina ya wanawe Gersoni wenye udugu wao: Libuni na Simei.
19
Nao wanawe Kehati wenye udugu wao ni Amuramu na Isihari, Heburoni na Uzieli.
20
Nao wanawe Merari wenye udugu wao ni Mahali na Musi. Hawa ndio ndugu za Lawi za milango ya baba zao.
21
Wa Gersoni walikuwa wao wa udugu wa Libuni nao wa udugu wa Simei; hawa ndio ndugu zao wa Gersoni.
22
Walipohesabiwa waume wote wenye mwezi mmoja na zaidi jumla yao walikuwa watu 7500.
23
Hawa ndugu zao wa Gersoni wakaambiwa, wapige makambi nyuma ya Kao upande wa baharini.
24
Naye mkuu wao wa mlango wa baba yao Gersoni awe Eliasafu, mwana wa Laeli.
25
Nazo kazi zao wana wa Gersoni za kuziangalia Hemani mwa Mkutano ziwe kuliangalia Kao lenyewe na Hema na chandalua chake na lile guo kubwa la pazia lililoko pa kuliingilia Hema la Mkutano,
26
nazo nguo za uani na lile guo kubwa la pazia lililoko pa kuuingilia ua, unaolizunguka Kao na meza ya kutambikia, tena kamba zake nayo yote yanyoupasa utumishi huu.
27
Wa Kehati walikuwa wao wa udugu wa Amuramu nao wa udugu wa Isihari nao wa udugu wa Heburoni nao wa udugu wa Uzieli. Hawa ndio ndugu zao wa Kehati.
28
Walipohesabiwa waume wote wenye mwezi mmoja na zaidi jumla yao walikuwa watu 8600 wa kuziangalia kazi za kupaangalia Patakatifu.
29
Hawa ndugu zao wa Kehati wakaambiwa, wapige makambi upande wa kusini wa Kao.
30
Naye mkuu wao wa mlango wa baba yao Kehati awe Elisafani, mwana wa Uzieli.
31
Nazo kazi zake ziwe kuliangalia Sanduku na meza ya mikate na kinara na meza ya kuvukizia nayo ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, navyo vyombo vya Patakatifu, watakavyovitumia, na pazia la Hemani, tena wafanye kazi zote za utumishi uwapasao.
32
Naye mkuu wa wakuu wa Walawi alikuwa Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, awakague wote wanaoangalia kazi za Patakatifu.
33
Wa Merari walikuwa wao wa udugu wa Mahali nao wa udugu wa Musi. Hawa ndio ndugu zao wa Merari.
34
Walipohesabiwa waume wote wenye mwezi mmoja na zaidi jumla yao walikuwa watu 6200.
35
Nao wakaambiwa, mkuu wao wa mlango wa baba yao Merari awe Surieli, mwana wa Abihaili, nao wapige makambi upande wa kaskazini wa Kao.
36
Nazo kazi zao wana wa Merari za kuangalia walizopewa ziwe hizo za mbao za Kao na misunguo yao na nguzo zao na miguu yao na vyombo vyao vyote, wafanye kazi zote za utumishi ziwapasazo,
37
tena kazi za kuziangalia nguzo zilizouzunguka ua na miguu yao na mambo zao na kamba zao.
38
Nao waliopiga makambi mbele ya Kao upande wa mashariki, ndio mbele ya Hema la Mkutano upande wa maawioni kwa jua walikuwa Mose na Haroni na wanawe waliongoja zamu za kupaangalia Patakatifu mahali pao wana wa Isiraeli. Lakini mgeni aliyejitia katika kazi hizi hakuwa na budi kuuawa.
39
Jumla yao Walawi wote, Mose na Haroni waliowakagua kwa amri ya Bwana, waume wote wenye mwezi mmoja na zaidi wa udugu wao walikuwa watu 22000.
40
Bwana akamwambia Mose: Wakague waume wote wa wana wa Isiraeli wenye mwezi mmoja na zaidi walio wana wa kwanza, ufanye hesabu ya majina yao.
41
Uwachukue Walawi kuwa wangu mimi Bwana, wakiwakomboa wana wote wa kwanza kwa wana wa Isiraeli, nao nyama wa kufuga wa Walawi na wawakomboe wana wa kwanza wa nyama wa kufuga wa wana wa Isiraeli.
42
Ndipo, Mose alipowakagua wana wote wa kwanza wa Waisiraeli, kama Bwana alivyomwagiza.
43
Nao waume wote waliokuwa wana wa kwanza wenye mwezi mmoja na zaidi walipohesabiwa majina, jumla yao walikuwa watu 22273.
44
Bwana akamwambia Mose kwamba:
45
Wachukue Walawi kuwa makombozi ya wana wote wa kwanza kwa wana wa Isiraeli, nao nyama wa kufuga wa Walawi kuwa makombozi ya nyama wao, Walawi wawe wangu mimi Bwana.
46
Nayo makombozi yao wale 273 waliozidi kwa wana wa kwanza wa wana wa Isiraeli kuwa wengi kuliko Walawi,
47
uwatoze kila mmoja fedha (sekeli) tano tano kichwa kwa kichwa, nazo hizi fedha, utakazowatoza, ziwe fedha zinazotumika Patakatifu, kila fedha moja iwe ya gera ishirini, ndio thumuni nane.
48
Hizi fedha mpe Haroni na wanawe kwa kuwa makombozi yao wale waliozidi kuwa wengi.
49
Ndipo, Mose alipowatoza fedha za makombozi wale waliozidi kuwa wengi kuliko wale waliokombolewa na Walawi.
50
Nazo hizi fedha, alizozitoza za kuwakomboa wana wa kwanza wa wana wa Isiraeli, zikawa 1365, zikipimwa kwa fedha za Patakatifu.
51
Kisha Mose akampa Haroni na wanawe hizo fedha kwa ile amri ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36