bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 26
Numbers 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 27 →
1
Lile pigo lilipokwisha kukoma, Bwana akamwambia Mose na Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, kwamba:
2
Toeni jumla yao wote walio mkutano wa wana wa Isiraeli kuanzia kwao walio wenye miaka ishirini na zaidi wa milango ya baba zao mkiwakagua wote wanaoweza kwenda vitani kwao Waisiraeli.
3
Kwa hiyo Mose na mtambikaji Elazari wakasema nao kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba:
4
Wahesabuni wao walio wenye miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose pamoja nao wana wa Isiraeli waliotoka katika nchi ya Misri.
5
Rubeni, mwana wa kwanza wa Isiraeli, wanawe Rubeni walikuwa: Henoki, baba ya ndugu zao Wahenoki, Palu, baba ya ndugu zao Wapalu;
6
Hesironi, baba ya ndugu zao Wahesironi, Karmi, baba ya ndugu zao Wakarmi.
7
Hizi ndizo ndugu zao Warubeni, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 43730.
8
Wana wa Palu walikuwa wa Eliabu;
9
nao hao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli na Datani na Abiramu; nao Datani na Abiramu walikuwa wale wateule wa mkutano walioshindana na Mose na Haroni katika mkutano wao wa Kora, wao waliposhindana na Bwana.
10
Ilikuwa hapo, nchi ilipoasama na kuwameza pamoja na Kora; wao wa mkutano wao walipokufa, moto ulikula watu 250, wakawa kielekezo cha kutisha.
11
Lakini wana wa Kora hawakufa hapo.
12
Wana wa Simeoni kwa ndugu zao walikuwa: Nemueli, baba ya ndugu zao Wanemueli, Yamini, baba ya ndugu zao Wayamini, Yakini, baba ya ndugu zao Wayakini,
13
Zera, baba ya ndugu zao Wazera, Sauli baba ya ndugu zao Wasauli.
14
Hizi ndizo ndugu zao Wasimeoni, watu 22200.
15
Wana wa Gadi kwa ndugu zao walikuwa: Sefoni, baba ya ndugu zao Wasefoni, Hagi, baba ya ndugu zao Wahagi, Suni, baba ya ndugu zao Wasuni;
16
Ozini, baba ya ndugu zao Waozini, Eri, baba ya ndugu zao Waeri;
17
Arodi, baba ya ndugu zao Waarodi, Areli, baba ya ndugu zao Waareli.
18
Hizi ndizo ndugu zao Wagadi; nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 40500.
19
Wana wa Yuda walikuwa: Eri na Onani, nao Eri na Onani walikuwa wamekufa katika nchi ya Kanaani.
20
Wana wa Yuda kwa ndugu zao walikuwa: Sela, baba ya ndugu zao Wasela, Peresi, baba ya ndugu zao Waperesi, Zera, baba ya ndugu zao Wazera.
21
Nao wana wa Peresi walikuwa: Hesironi, baba ya ndugu zao Wahesironi, Hamuli, baba ya ndugu zao Wahamuli.
22
Hizi ndizo ndugu zao Wayuda, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 76500.
23
Wana wa Isakari kwa ndugu zao walikuwa: Tola, baba ya ndugu zao Watola, Puwa, baba ya ndugu zao Wapuwa;
24
Yasubu, baba ya ndugu zao Wayasubu, Simuroni, baba ya ndugu zao Wasimuroni.
25
Hizi ndizo ndugu zao Waisakari, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 64300.
26
Wana wa Zebuluni kwa ndugu zao walikuwa: Seredi, baba ya ndugu zao Waseredi, Eloni, baba ya ndugu zao Waeloni, Yaleli, baba ya ndugu zao Wayaleli.
27
Hizi ndizo ndugu zao Wazebuluni, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 60500.
28
Wana wa Yosefu kwa ndugu zao walikuwa: Manase na Efuraimu.
29
Wana wa Manase walikuwa: Makiri, baba ya ndugu zao Wamakiri, naye Makiri akamzaa Gileadi, naye Gileadi alikuwa baba ya ndugu zao Wagileadi.
30
Nao wana wa Gileadi walikuwa: Iezeri, baba ya ndugu zao Waiezeri, Heleki, baba ya ndugu zao Waheleki,
31
na Asirieli, baba ya ndugu zao Waasirieli, na Sekemu, baba ya ndugu zao Wasekemu,
32
na Semida, baba ya ndugu zao Wasemida, na Heferi, baba ya ndugu zao Waheferi.
33
Lakini Selofuhadi, mwana wa Heferi, hakuwa na mwana wa kiume, walikuwa wa kike tu, nayo majina yao hao wana wa kike wa Selofuhadi yalikuwa Mala na Noa, Hogla, Milka na Tirsa.
34
Hizi ndizo ndugu zao Wamanase, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 52700.
35
Wana wa Efuraimu kwa ndugu zao walikuwa: Sutela, baba ya ndugu zao Wasutela, Bekeri, baba ya ndugu zao Wabekeri, Tahani, baba ya ndugu zao Watahani.
36
Nao hawa walikuwa wana wa Sutela: Erani, baba ya ndugu zao Waerani.
37
Hizi ndizo ndugu zao wana wa Efuraimu, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 32500. Hawa walikuwa wana wa Yosefu kwa ndugu zao.
38
Wana wa Benyamini kwa ndugu zao walikuwa: Bela, baba ya ndugu zao Wabela, Asibeli, baba ya ndugu zao Waasibeli, Ahiramu, baba ya ndugu zao Waahiramu,
39
Sufamu, baba ya ndugu zao Wasufamu, Hufamu, baba ya ndugu zao Wahufamu.
40
Nao wana wa Bela walikuwa Ardi na Namani, baba ya ndugu zao Waardi na baba ya ndugu zao Wanamani.
41
Hawa walikuwa wana wa Benyamini kwa ndugu zao, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 45600.
42
Hawa walikuwa wana wa Dani kwa ndugu zao: Suhamu, baba ya ndugu zao Wasuhamu; hizi ndizo ndugu zao Wadani kwa ndugu zao.
43
Nao wa kwao ndugu zao Wasuhamu waliokaguliwa walikuwa watu 64400.
44
Wana wa Aseri kwa ndugu zao walikuwa: Imuna, baba ya ndugu zao Waimuna, Iswi, baba ya ndugu zao Waiswi, Beria, baba ya ndugu zao Waberia.
45
Wana wa Beria walikuwa: Heberi, baba ya ndugu zao Waheberi, Malkieli, baba ya ndugu zao Wamalkieli.
46
Nalo jina la mwanawe wa kike wa Aseri alikuwa Sara.
47
Hizi ndizo ndugu zao wana wa Aseri, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 53400.
48
Wana wa Nafutali kwa ndugu zao walikuwa: Yaseli, baba ya ndugu zao Wayaseli, Guni, baba ya ndugu zao Waguni,
49
Yeseri, baba ya ndugu zao Wayeseri, Silemu, baba ya ndugu zao Wasilemu.
50
Hizi ndizo ndugu zao Wanafutali kwa ndugu zao; nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 45400.
51
Hii ilikuwa jumla ya wana wa Isiraeli waliokaguliwa watu 601730.
52
Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:
53
Hawa ndio watakaogawiwa nchi hiyo kwa hesabu ya majina.
54
Walio wengi uwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache uwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao; kila shina sharti lipate fungu lake kwa hesabu yao waliokaguliwa kwake.
55
Lakini nchi sharti igawanywe kwa kupiga kura, wapate mafungu yao kwa majina ya baba za mashina.
56
Wao walio wengi nao walio wachache sharti mafungu yao ya kuwa yao wenyewe wagawiwe kwa kupigiwa kura.
57
Nayo hii ndiyo jumla ya Walawi kwa ndugu zao: Gersoni, baba ya ndugu zao Wagersoni, Kehati, baba ya ndugu zao Wakehati, Merari baba ya ndugu zao Wamerari.
58
Hizi ndizo ndugu zao Walawi: Ndugu zao Walibuni, ndugu zao Waheburoni, ndugu zao Wamahali, ndugu zao Wamusi, ndugu zao Wakora. Naye Kehati alimzaa Amuramu.
59
Nalo jina lake mkewe Amuramu alikuwa Yokebedi, binti Lawi, huyu Lawi aliyezaliwa huko Misri, naye akamzalia Amuramu Haroni na Mose na umbu lao Miriamu.
60
Naye Haroni aliwazaa: Nadabu na Abihu na Elazari na Itamari.
61
Lakini Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa isiyopasa.
62
Jumla yao ilikuwa watu 23000, ndio wa kiume wote waliokuwa wenye mwezi mmoja na zaidi; kwani hawakukaguliwa katikati ya wana wa Isiraeli, kwa kuwa hawakupewa fungu lao wenyewe katikati ya wana wa Isiraeli.
63
Hii ndiyo jumla yao, Mose na mtambikaji Elazari waliowakagua, walipowakagua wana wa Isiraeli kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
64
Miongoni mwao hakuwamo mtu hata mmoja wao, Mose na mtambikaji Haroni waliowakagua walipowakagua wana wa Isiraeli nyikani kwa Sinai.
65
Kwani Bwana aliwaambia: Hamna budi kufa nyikani; kwa hiyo hakusalia mtu hata mmoja kwao, ni Kalebu tu, mwana wa Yefune, na Yosua, mwana wa Nuni.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36