bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 5
Numbers 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waagize wana wa Isiraeli, watoe makambini wote walio wenye ukoma nao wote walio wenye kisonono nao wote waliojipatia uchafu kwa kugusa mfu.
3
Sharti mwatoe, kama ni mume au kama ni mke, na kuwatuma kwenda nje ya makambi, wasiyachafue makambi, mimi ninamokaa katikati yao.
4
Wana wa Isiraeli wakayafanya na kuwatuma kwenda nje ya makambi; kama Bwana alivyomwambia Mose, ndivyo, wana wa Isiraeli walivyoyafanya.
5
Bwana akamwambia Mose kwamba:
6
Waambie wana wa Isiraeli: Mtu mume au mke akifanya kosa lo lote la kimtu na kumvunjia Bwana maagano, mtu huyo atakuwa amekora manza.
7
Hao sharti wayaungame makosa yao, waliyoyafanya, kisha wazilipe manza zao, walizozikora, na kumrudishia mwenyewe, waliyemkosea, mali zake sawasawa na kuongeza fungu la tano.
8
Kama mtu huyo hakuacha ndugu anayepasa kupewa hayo malipo ya manza, sharti Bwana apewe hayo malipo ya manza, yawe yake mtambikaji, wakiisha kutoa humo dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kumpatia upozi.
9
Navyo vipaji vyote vya tambiko, wana wa Isiraeli watakavyovitoa kuwa vitakatifu vya kumnyanyulia Bwana, na wampelekee mtambikaji, navyo vitakuwa vyake.
10
Vipaji vyo vyote, mtu atakavyovitoa kuwa vitakatifu, vitakuwa vyake mtambikaji, navyo vyote, mtu atakavyompa mtambikaji, vitakuwa vyake.
11
Bwana akamwambia Mose kwamba:
12
Sema na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Kama mke wa mtu anakosa na kumvunjia mumewe maagano yake,
13
mtu akilala naye kwa ugoni, vikafichika machoni pa mumewe, asijulikane, ya kuwa amejichafua, kwa kuwa hakuwako shahidi, wala hakufumaniwa,
14
lakini wivu ukiwaka moto rohoni mwake mumee, amwonee mkewe wivu kwa kwamba amejichafua, au pengine wivu ukiwaka moto rohoni mwake mumewe, amwonee mkewe wivu, naye haujichafua,
15
basi, vikiwa hivyo sharti mume ampeleke mkewe kwa mtambikaji pamoja na kumpelekea toleo lake, vibaba viwili vya unga wa mawele, lakini asiumiminie mafuta, wala asiweke uvumba juu yake, kwani ni kilaji cha tambiko cha wivu, tena ni kilaji cha tambiko cha ukumbusho cha kukumbushia manza, alizozikora.
16
Naye mtambikaji na ampeleke huyo mwanamke, amsimamishe mbele yake Bwana,
17
kisha mtambikaji achote maji matakatifu kwa chombo cha udongo, kisha achote hata vumbi kidogo lililoko chini Kaoni, alitie katika hayo maji.
18
Mtambikaji akiisha kumsimamisha huyo mwanamke mbele ya Bwana na kuzifungua nywele za kichwani pake, na ampe mkononi mwake hicho kilaji cha tambiko cha ukumbusho, nacho ni kilaji cha tambiko cha wivu, lakini yale maji machungu yenye maapizo mtambikaji sharti ayashike mkononi mwake.
19
Kisha mtambikaji na amwapishe na kumwambia huyo mwanamke: Kama mtu hakulala kwako, nawe hukukosa na kujichafua ukimtumia mwingine kuwa kama mumeo, hutapatwa na apizo lo lote la haya maji machungu yenye maapizo.
20
Lakini kama umekosa na kujichafua ukimtumia mwingine kuwa kama mumeo, mtu ye yote akilala kwako kwa ugoni asiye mumeo, basi, yatakupata.
21
Kisha mtambikaji na amwapishe huyo mwanamke kwa kiapo cha kuapiza, mtambikaji akimwambia huyo mwanamke: Bwana na akuweke kuwa kielekezo cha kuapizwa katikati yao walio ukoo wako akivipoozesha viuno vyako pamoja na kulivimbisha tumbo lako!
22
Nayo maji haya yenye maapizo na yaingie mwilini mwako, yalivimbishe tumbo lako pamoja na kuvipoozesha viuno vyako! Naye huyo mwanamke sharti aitikie na kusema: Amin. Amin.
23
Kisha mtambikaji na ayaandike haya maapizo chuoni na kuyafuta kwa yale maji machungu.
24
Kisha na amnyweshe huyo mwanamke hayo maji machungu yenye maapizo, yamwingie.
25
Kisha mtambikaji na akichukue kilaji cha tambiko cha wivu mkononi mwa mwanamke, akipitishe motoni mbele ya Bwana na kumtolea mezani pa kutambikia.
26
Hapo mtambikaji na achukue gao moja la kilaji cha tambiko kilicho cha ukumbusho wake mwanamke, akichome moto mezani pa kutambikia, kisha amnyweshe mwanamke yale maji.
27
Akiisha kumnywesha hayo maji, naye akiwa amejichafua na kumvunjia mumewe maagano yake, basi, hayo maji machungu yenye maapizo yatakapomwingia yatalivimbisha tumbo lake pamoja na kuvipoozesha viuno vyake; ndivyo, huyu mwanamke atakavyokuwa ameapizwa kwao walio ukoo wake.
28
Lakini kama mwanamke huyu hakujichafua, akiwa ametakata, hatapatwa na jambo lo lote, ila atazaa watoto tena.
29
Haya ndiyo maonyo yao wenye wivu, mwanamke akiwa amekosa na kujipatia uchafu kwa kutumia mwingine kuwa kama mumewe,
30
au wivu ukiwaka moto rohoni mwa mtu, amwonee mkewe wivu, amsimamishe huyo mwanamke mbele ya Bwana, mtambikaji amfanyizie mambo yote ya haya maonyo.
31
Hapo mumewe atakuwa hana manza zo zote tena, lakini mwanamke aliye hivyo hana budi kujitwika manza, alizozikora.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36