bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 34
Numbers 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 35 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waagize wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, basi, nchi itakayowaangukia kuwa fungu lenu itakuwa nchi ya Kanaani hivyo, ilivyo na mipaka yake.
3
Mpaka wenu wa kusini utoke nyikani kwa Sini, uendelee kando ya Edomu; hivyo mpaka wenu wa kusini utaanzia upande wa maawioni kwa jua kwenye mwisho wa Bahari ya Chumvi.
4
Kisha huo mpaka upazungukie hapo pa kukwelea Akarabimu upande wake wa kusini, kisha upitie sini, utokee upande wa kusini wa Kadesi-Barnea, kisha utokee kwenye ua wa Adari na kufikia Asimoni.
5
Kutoka Asimoni mpaka ukigeukie kijito cha Misri, upate kutokea baharini.
6
Mpaka wenu wa upande wa baharini utakuwa Bahari Kubwa; huu utakuwa mpaka wenu wa upande wa baharini.
7
Mpaka wenu wa kaskazini utoke kwenye Bahari Kubwa, mwufikishe mlimani kwa Hori;
8
toka mlimani kwa Hori mwufikishe mpaka Hamati, kisha mpaka huu tokee Sedadi.
9
Ukitoka hapo, mpaka uendelee kufika Zifuroni, kisha utokee kwenye ua wa Enani. Huu utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
10
Mpaka wenu wa upande wa maawioni kwa jua utoke kwenye ua wa Enani, mwufikishe Sefamu;
11
toka Sefamu mpaka na utelemkie Ribula na kupita Aini upande wa maawioni kwa jua; kisha mpaka uendelee kutelemka, hata ufike kando ya bahari ya Kinereti upande wake wa maawioni kwa jua.
12
Kisha mpaka wa utelemke na kuufuata mto na Yordani, hata utokee kwenye Bahari ya Chumvi. Hii itakuwa nchi yenu yenye hiyo mipaka yake inayoizunguka pande zote.
13
Kisha Mose akawaagiza wana wa Isiraeli kwamba: Hiyo ndiyo nchi, mtakayoipata kwa kupiga kura, mwichukue, iwe yenu, naye Bwana ameagiza kuipa yale mashina tisa na nusu ya Manase.
14
Kwani wao wa shina la Rubeni wamekwisha kuipatia milango ya baba zao, nao wa shina la wana wa Gadi wamekwisha kuipatia milango ya baba zao, nao walio nusu ya shina la Manase wamekwisha kujipatia mafungu yao.
15
Hayo mashina mawili na nusu ya shina la Manase wamekwisha kujipatia mafungu yao ng'ambo ya Yordani ya mashariki iliyo ya maawioni kwa jua, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
16
Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:
17
Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia ninyi nchi hiyo, iwe yenu: mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni.
18
Tena sharti mchukue mkuu mmoja mmoja wa kila shina moja wa kusaidia kuigawanya nchi hiyo.
19
Nayo haya ndiyo majina ya watu hao: wa shina la Yuda Kalebu, mwana wa Yefune.
20
Wa shina la wana wa Simeoni Samueli, mwana wa Amihudi.
21
Wa shina la Benyamini Elidadi, mwana wa Kisiloni.
22
Wa shina la wana wa Dani mkuu Buki, mwana wa Yogli.
23
Wa wana wa Yosefu: wa shina la wana wa Manase mkuu Hanieli, mwana wa Efodi.
24
Wa shina la wana wa Efuraimu mkuu Kemueli, mwana wa Sifutani.
25
Wa shina la wana wa Zebuluni mkuu Elisafani, mwana wa Parnaki.
26
Wa shina la wana wa Isakari mkuu Paltieli, mwana wa Azani.
27
Wa shina la wana wa Aseri mkuu Ahihudi, mwana wa Selomi.
28
Wa shina la wana wa Nafutali mkuu Pedaheli, mwana wa Amihudi.
29
Hawa ndio, Bwana aliowaagiza, kuwagawanyia wana wa Isiraeli mafungu yao katika nchi ya Kanaani.
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36