bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 14
Numbers 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 15 →
1
Ndipo, wao wote wa mkutano walipozipaza sana sauti zao, watu wakalia usiku kucha.
2
Wana wote wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni, nao wote walio wa mkutano wao wakawaambia: Afadhali tungalikufa katika nchi ya Misri au tungekufa huku nyikani!
3
Kwa nini Bwana anatupeleka katika nchi ile, tuuawe kwa panga, wake zetu nao watoto wetu watekwe? Haitatufalia zaidi kurudi Misri?
4
Wakasemezana wao kwa wao: Na tujipatie mkuu, turudi Misri?
5
Ndipo, Mose na Haroni walipojiangusha nyusoni pao mbele ya huo mkutano wote wa wana wa Isiraeli uliokusanyika.
6
Nao Yosua, mwana wa Nuni, na Kalebu, mwana wa Yefune, waliokuwa pamoja nao walioipeleleza hiyo nchi, wakayararua mavazi yao,
7
wakauambia mkutano wote wa wana wa Isiraeli kwamba; Ile nchi, tuliyoipita na kuipeleleza, ni nchi njema sanasana.
8
Bwana akipendezwa nasi, atatuingiza katika nchi hiyo, atupe, iwe yetu; nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali.
9
Ni hili tu, msimpingie Bwana! Tena wale watu wa nchi hiyo msiwaogope, kwani watakuwa kama chakula chetu, nacho kivuli, walichokikimbilia, kimeondoka kwao, naye Bwana yuko pamoja na sisi, kwa hiyo msiwaogope!
10
Wao wote wa huo mkutano walipotaka kuwaua na kuwatupia mawe, ndipo, utukufu wa Bwana ulipotokea penye Hema la Mkutano mbele ya wana wote wa Isiraeli.
11
Bwana akamwambia Mose: Watu hawa watanitukana mpaka lini? Watakataa mpaka lini kunitegemea? Nami nimevifanya hivyo vielekezo vyote kwao!
12
Nitawapiga kwa ugonjwa mbaya uuao, niwatoweshe, kisha nitakufanya wewe kuwa kabila kubwa lenye nguvu kuliko hawa.
13
Lakini Mose akamwambia Bwana: Wamisri watavisikia; kwani wewe umewatoa watu hawa kwa nguvu yako katikati yao, ukawaleta huku.
14
Nao wenyeji wa nchi hii watasimuliwa, kwani nao wamesikia, ya kuwa wewe Bwana uko katikati ya watu hawa, uliowatokea, wakuone macho kwa macho wewe Bwana, tena ya kuwa wingu lako huwasimamia, ukiwatangulia mchana kwa wingu linalofanana na nguzo, nao usiku kwa wingu le moto linalofanana na nguzo
15
Kama ungewaua watu hawa kama mtu mmoja, ndipo, wamizimu waliousikia uvumi wako watakaposema kwamba:
16
Kwa kuwa Bwana hakuweza kuwaingiza watu hawa katika nchi hiyo, aliyoiapia kuwapa, kwa hiyo amewachinja nyikani.
17
Sasa nguvu ya Bwana wangu na ionekane kuwa kuu, kama ulivyosema kwamba:
18
Bwana ni mwenye uvumilivu na upole mwingi, huondoa manza na mapotovu, lakini mbele yake hakuna asiye mkosaji; nazo manza, baba walizozikora, huzilipisha wtoto, akifikishe kizazi cha tatu na cha nne.
19
Waondolee watu hawa manza kwa ukubwa wa upole wako, kama ulivyowaondolea watu hawa makosa yao kutoka Misri mpaka hapa!
20
Ndipo, Bwana aliposema: Nimewaondolea makosa kwa hivyo, ulivyowaombea.
21
Kwa hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ulimwengu wote utaenezwa utukufu wangu.
22
Kwani watu hawa wote waliouona utukufu wangu na vielekezo vyangu, nilivyovifanya Misri na nyikani, wakanijaribu sana mara kumi wakikataa kuisikiliza sauti yangu,
23
hawa wote hawataiona nchi, niliyowaapia baba zao kuwapa, kweli wao wote walionitukana hawataiona kabisa.
24
Ni mtumishi wangu Kalebu tu aliye mwenye roho nyingine moyoni mwake, akanifuata kwa moyo wote, basi, yeye nitamwingiza katika nchi hiyo, aliyoiingia kwanza, nao wa uzao wake wataichukua kuwa yao,
25
lakini Waamaleki na Wakanaani watakaa bondeni. Kesho geukeni na kujiendea nyikani mkishika njia ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu.
26
Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
27
Itakuwa mpaka lini, watu wa mkutano huu mbaya wakininung'unikia? Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Isiraeli, wao waliponinung'unikia.
28
Waambie: Ndivyo, asemavyo Bwana: Kwa hivyo, nilivyo Mwenye uzima, nitawafanyizia yayo hayo, mliyoyasema masikioni mwangu:
29
Huku nyikani itaanguka mizoga yenu ninyi nyote mliokaguliwa na kuhesabiwa, mlio wenye miaka ishirini na zaidi, mlioninung'unikia.
30
Ninyi nyote hamtaiingia kabisa ile nchi, niliyoiapia na kuuinua mkono wangu, ya kwamba nitawakalisha huko. Kalebu, mwana wa Yefune, na Yosua, mwana wa Nuni, hawa tu wataiona.
31
Lakini watoto wenu, mliowasema, ya kama watakuwa mateka, nitawaingiza huko waijue nchi ile, mliyoikataa.
32
Lakini mizoga yenu ninyi itaanguka huku nyikani.
33
Lakini kwanza wana wenu watakuwa wachungaji nyikani miaka 40, watwikwe ugoni wenu, mpaka mizogo yenu imalizike nyikani.
34
Kwa hesabu ya zile siku 40, mlizoipeleleza ile nchi, kila siku moja itahesabiwa kuwa mwaka mmoja; hivyo ndivyo, watakavyotwikwa miaka 40 manza, mlizozikora, mpate kutambua, mambo yanavyoendelea, nikiondoka kwenu.
35
Mimi Bwana nimesema, nami nitawafanyizia haya wao wote walio wa mkutano huu mbaya waliokusanyika, wanipingie: huku nyikani watamalizika, kwani huku ndiko, watakakofia.
36
Kisha wale watu, Mose aliowatuma kuipeleleza nchi ile, ni wao waliounung'unisha mkutano wote waliporudi na kutoa habari za nchi ile,
37
hao watu waliozitoa zile habari mbaya za nchi ile wakafa kwa kupigwa na Bwana.
38
Lakini Yosua, mwana wa Nuni, na Kalebu, mwana wa Yefune, ndio waliokaa wenye uzima miongoni mwao waliokwenda kuipeleleza ile nchi.
39
Mose alipowaambia wana wote wa Isiraeli maneno haya, wakasikitika sana.
40
Kesho yake wakaamka na mapema, wakapanda mlimani juu kileleni na kusema: Basi, tumekwisha kufika huku, sasa twende kupanda mahali pale, Bwana alipotuelekeza! Kwani tumekosa.
41
Lakini Mose akasema: Mbona ninyi mwataka kuitangua amri ya Bwana? Hamtafanikiwa.
42
Msipande! Kwani Bwana hamnaye katikati yenu, msipigwe na adui zenu.
43
Kwani Waamaleki na Wakanaani wako mbele yenu, nanyi mtaangushwa kwa panga, kwa kuwa mmerudi nyuma na kumwacha Bwana; kwa hiyo Bwana hatakuwa nanyi.
44
Lakini kwa kujivuna wakapanda mlimani juu kileleni, lakini Sanduku la Agano la Bwana na Mose hawakutoka makambini.
45
Ndipo, Waamaleki na Wakanaani waliokaa huko mlimani walipotelemka, wakawapiga, wakawatawanya mpaka Horma.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36