bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 28
Numbers 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 29 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waagize wana wa Isiraeli, uwaambie: Jiangalieni, mnitolee wakati huo uliowekwa matoleo yanayonipasa, ndio chakula changu cha ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa kuwa mnuko wa kunipendeza.
3
Uwaambie: Nazo hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa, mtakazomtolea Bwana: Wana kondoo wa mwaka mmoja wasio na kilema, pasipo kukoma kila siku wawili kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
4
Mwana kondoo mmoja utamtoa asubuhi, naye mwana kondoo wa pili utamtoa saa za jioni.
5
Pamoja naye utoe vibaba vitatu vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na kibaba kimoja cha mafuta yaliyotwangwa vema kuwa kilaji cha tambiko.
6
Hii ndio ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima iliyotolewa kila siku mlimani kwa Sinai kuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
7
Tena utoe kinywaji chake cha tambiko, kibaba kimoja cha mvinyo kwa kila mwana kondoo, nacho hicho kinywaji cha tambiko cha mvinyo yenye nguvu ummiminie Bwana hapo Patakatifu.
8
Naye mwana kondoo wa pili na umtoe saa za jioni pamoja na kilaji cha tambiko na kinywaji chake cha tambiko kama asubuhi; ukifanya hivyo, vitakuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
9
Tena siku ya mapumziko mtoe wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na kilema na vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko, tena kinywaji chake cha tambiko.
10
Hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kila siku ya mapumziko, mtakazozitoa pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kila siku na kinywaji chake cha tambiko.
11
Tena siku za kwanza za miezi yenu na mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
12
Tena mtoe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha dume moja la kondoo.
13
Tena vibaba vitatutatu vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha kila mwana kondoo mmoja. Ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima itakayotolewa hivyo itakuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
14
Navyo vinywaji vyao vya tambiko na viwe vibaba viwili vya mvinyo vya dume moja la ng'ombe na kibaba kimoja na nusu cha mvinyo cha dume la kondoo na kibaba kimoja cha mvinyo cha mwana kondoo mmoja. Hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima za mwandamo wa mwezi, mtakazozitoa mwezi kwa mwezi mwaka mzima.
15
Tena pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku Bwana na atolewe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na kinywaji chake cha tambiko.
16
Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ni Pasaka ya Bwana.
17
Siku ya kumi na tano ya mwezi huo na mle sikukuu; ndipo iliwe mikate isiyochachwa siku saba.
18
Siku ya kwanza na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,
19
ila mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima motoni: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
20
Navyo vilaji vyao vya tambiko na mtoe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume la kondoo.
21
Tena na mtoe vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
22
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kuwapatia ninyi upozi.
23
Hao sharti mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya asubuhi inayotolewa kila siku.
24
Hao na mwatoe kila siku siku hizo saba kuwa chakula cha moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana; nao na watolewe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kinywaji chake cha tambiko.
25
Siku ya saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
26
Siku ya malimbuko, mtakapomtolea Bwana vilaji vipya vya tambiko, ndio sikukuu yenu ya majuma saba; hapo na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
27
Tena na mtoe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza Bwana: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja.
28
Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume moja la kondoo,
29
tena vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
30
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwapatia ninyi upozi.
31
Hao na mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kilaji chake cha tambiko; nao sharti wawe pasipo kilema, tena mtoe navyo vinywaji vyao vya tambiko.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36