bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 16
Numbers 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
1
Kora, mwana wa Isihari, mwana wa Kehati, mwana wa Lawi, akachukua watu, yeye na Datani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Peleti, waliokuwa wana wa Rubeni.
2
Hawa wakamwinukia Mose pamoja na wana wa Isiraeli 250 waliokuwa wakuu mashaurini na wateule wa mkutano wenye jina kuu.
3
Wakakusanyika kutetana na Mose na Haroni, wakawaambia: Maneno yenu ni mengi, kwani wao wote wa mkutano wetu mzima ni watakatifu, naye Bwana yuko katikati yao. Mbona mnajikweza kuwa wakuu wao wa mkutano wa Bwana?
4
Mose alipoyasikia akaanguka kifudifudi,
5
akamwambia Kora nao wenzake wote, aliowakusanya, kwamba: Kesho Bwana atamjulisha aliye wake naye aliye mtakatifu akimfikisha kwake; kwani atakayemchagua atamfikisha kwake.
6
Fanyeni haya: jichukulieni vyetezo, wewe Kora na wenzako wote, uliowakusanya!
7
Tieni moto humo, kisha wekeni kesho mavukizo juu yao mbele ya Bwana! Naye mtu, Bwana atakayemchagua, na awe mtakatifu. Maneno yenu ni mengi, ninyi wana wa Lawi.
8
Kisha Mose akamwambia Kora: Sikieni, ninyi wana wa Lawi!
9
Je? Ni kidogo kwenu, Mungu wa Isiraeli akiwatenga ninyi kwao wa mkutano wa Waisiraeli na kuwafikisha kwake, mwutumikie utumishi wa Kao lake Bwana na kusimama mbele ya mkutano kwa kuutumikia?
10
Wewe na ndugu zako wote walio wana wa Lawi amewafikisha kwake pamoja na wewe, tena mnautafutiaje utambikaji nao?
11
Kweli wewe pamoja na wenzako wote mnafanya shauri la kumpingia Bwana, kwani Haroni ni nani, mkimnung'unikia?
12
Kisha Mose akatuma kumwita Datani na Abiramu, wana wa Eliabu, lakini wakasema: Hatuji.
13
Ni kidogo, ukitutoa katika nchi ichuruzikayo maziwa na asali, utuue huku nyikani? Unajikuzaje tena kuwa mkuu wa kututawala?
14
Kweli umetuingiza katika nchi ichuruzikayo maziwa na asali! Kweli umetugawia mashamba na mizabibu kuwa yetu! Watu hawa unataka kuwachoma macho? Hatuji.
15
Ndipo, Mose alipokasirika sana, akamwambia Bwana: Usigeuke kuvitazama vilaji vyao vya tambiko! Sikuchukua kwao hata punda mmoja tu, wala mtu wa kwao sikumfanyizia mabaya hata mmoja tu.
16
Kisha Mose akamwambia Kora: Wewe na wenzako wote, uliowakusanya, sharti mwe kesho mbele ya Bwana, wewe nao wale na Haroni.
17
Mchukue kila mmoja chetezo chake, mtie humo mavukizo, kisha mmtokee Bwana kila mmoja na chetezo chake, vyote viwe vyetezo 250, wewe nawe na Haroni, kila na chake chetezo.
18
Wakachukua kila mtu chetezo chake, wakatia moto humo, juu ya moto wakaweka mavukizo, wakaja kusimama hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, hata Mose na Haroni walikuwako.
19
Lakini Kora alikuwa aliwakusanya hao wa mkutano wote hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; ndipo, utukufu wa Bwana ulipoutokea huo mkutano wote.
20
Naye Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
21
Jitengeni na kutoka katikati yao wa mkutano huu! Kwani nitawamaliza kwa mara moja.
22
Wakaanguka kifudifudi, wakasema: Mungu uliye Mungu wa roho zao wote walio wenye miili, mtu mmoja akikosa, utawachafukia wote wa mkutano huu?
23
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose kwamba:
24
Waambie wao wa mkutano huu kwamba: Epukeni kabisa po pote panapoyazunguka makao ya Kora na ya Datani na ya Abiramu!
25
Kisha Mose akainuka, akaenda kwao Datani na Abiramu, nao wazee wa Waisiraeli wakamfuata.
26
Akasema nao wa mkutano kwamba: Ondokeni penye mahema ya watu hawa wasiomcha Mungu! Wala msiguse cho chote kilicho chao, msiangamizwe kwa ajili ya makosa yao yote.
27
Ndipo, walipoepuka po pote palipoyazunguka makao ya Kora na ya Datani na ya Abiramu, lakini Datani na Abiramu wakatoka, wakasimama hapo pa kuyaingilia mahema yao pamoja na wake zao na wana wao na watoto wao wachanga.
28
Kisha Mose akasema: Hivi ndivyo, mtakavyotambua, kama Bwana alinituma, niyafanye hayo matendo yote, au kama ni moyo wangu ulionituma:
29
watu hawa watakapokufa, kama watu wote wanavyokufa, au watakapopatwa na mambo, watu wote wanayopatwa nayo, Bwana hakunituma.
30
Lakini Bwana akiumba jambo jipya, nchi ikiasama na kuwameza wao pamoja navyo vyote vilivyo vyao, washuke kuzimuni wakiwa wazima, ndipo, mtakapotambua, ya kuwa watu hao wamemtukana Bwana.
31
Ikawa, alipokwisha kuyasema maneno haya, ndipo, nchi ilipoatuka chini yao,
32
maana nchi ikaasama, ikawameza wao pamoja na nyumba zao, nao watu wote waliokuwa upande wa Kora, nazo mali zao zote.
33
Ndivyo, walivyoshuka kuzimuni pamoja navyo vyote vilivyokuwa vyao wakiwa wazima, kisha nchi ikawafunika, wakawa wametoweka katikati yao wa mkutano huu.
34
Nao Waisiraeli wote waliosimama hapo na kuwazunguka wakakimbia kwa makelele yao, kwani walisema: Nchi isitumeze na sisi!
35
Kisha moto ukatoka kwake Bwana, ukawala wale watu 250, walipokuwa wanavukiza.
36
Bwana akamwambia Mose kwamba:
37
Mwambie Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, aviokote vyetezo hapo, wale walipoteketezwa, kwani ni vitakatifu; nayo makaa ya moto uyamwage huko na huko.
38
Kisha hivyo vyetezo vya hao wakosaji waliojipatia kufa wenyewe vitengenezeni kuwa mabati mapana ya kuifunikiza meza ya kutambikia. Kwa kuwa walivitokeza mbele ya Bwana, ni vitakatifu, navyo sharti viwe kielekezo kwao wana wa Isiraeli.
39
Naye mtambikaji Elazari akavichukua hivyo vyetezo vya shaba, wao walioteketea walivyovitokeza mbele ya Bwana, wakavisana, viwe kifuniko cha meza ya kutambikia.
40
Hivyo vikawa ukumbusho wa wana wa Isiraeli, kwa kwamba mtu mgeni asiye wa uzao wa Haroni, asije kuvukiza mavukizo mbele ya Bwana, asipatwe na mambo kama Kora na wenzake, aliowakusanya, maana Bwana alivyomwambia kinywani mwa Mose yalimpata.
41
Kesho yake wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni kwamba: Mmewaua watu wa Mungu.
42
Ikawa, huo mkutano ulipokusanyika kutetana na Mose na Haroni, nao hao walipoligeukia Hema la Mkutano, mara lile wingu likalifunika, nao utukufu wa Bwana ukatokea.
43
Mose na Haroni walipokwenda kufika hapo mbele ya Hema la Mkutano,
44
Bwana akamwambia Mose kwamba:
45
Jiepusheni katikati ya mkutano huu, niwamalize kwa mara moja! Ndipo, walipoanguka kifudifudi,
46
naye Mose akamwambia Haroni: Chukua chetezo, utie humo moto wa mezani pa kutambikia, kisha weka mavukizo juu yake, uende upesi kwenye mkutano, uwapatie upozi, kwani makali yamekwisha kutoka kwake Bwana, nalo pigo limekwisha kuwaanzia.
47
Haroni akachukua chetezo, kama Mose alivyosema, akapiga mbio kufika katikati ya mkutano, akaona, ya kuwa pigo limeanza kweli kupiga watu; ndipo, alipotia mavukizo juu ya moto, awapatie watu upozi.
48
Aliposimama katikati yao waliokufa nao walio wazima bado, hilo pigo likakomeshwa.
49
Nao waliouawa na hilo pigo walikuwa watu 14700, wasipohesabiwa waliokufa kwa ajili ya Kora.
50
Kisha Haroni akarudi kwa Mose hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, hilo pigo lilipokuwa limekomeshwa.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36