bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 11
Numbers 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 12 →
1
Lakini watu wakanuna, vikawa vibaya masikioni mwa Bwana; naye Bwana alipovisikia, makali yake yakawaka moto, nao moto wa Bwana ukawawakia, ukayala makambi yaliyokuwa pembeni.
2
Ndipo, watu walipomlilia Mose; naye Mose alipomlalamikia Bwana, moto ukakoma.
3
Wakapaita mahali pale Tabera (Wakio la Moto), kwa kuwa moto wa Bwana uliwawakia hapo.
4
Wafuasi waliokuwa katikati yao wakaingiwa na tamaa kabisa; ndipo, nao wana wa Isiraeli walipolia tena na kusema: Yuko nani atakayetupa nyama, tule?
5
Tunazikumbuka samaki, tulizokula bure tu katika nchi ya Misri, nayo matango na matikiti na mabogaboga na vitunguu na vitunguu somu.
6
Lakini sasa roho zetu zimekauka, kwani hivyo vyote haviko, macho yetu huona Mana tu.
7
Nazo Mana zilikuwa kama punje za mtama mweupe, tena ukizitazama zilifanana na magwede.
8
Watu wakazungukazunguka na kuziokota, wakazisaga kwa mawe ya kusagia, au wakazitwanga katika vinu, kisha wakazipika katika nyungu au wakatengeneza mikate, nayo walipoila ilikuwa kama maandazi penye mafuta matamu.
9
Umande ulipoanguka usiku makambini, Mana nazo zikaanguka pamoja nao.
10
Mose alipowasikia watu, wakilia ndugu na ndugu pamoja, kila mtu pa kuliingilia hema lake, nayo makali ya Bwana yalipowaka sana, vikawa vibaya machoni pake Mose.
11
Kwa hiyo Mose akamwambia Bwana: Mbona unamfanyizia mtumishi wako vibaya? Mbona sioni upendeleo machoni pako? Mbona unanitwika mizigo ya watu hawa wote?
12
Je? Aliyewazaa watu hawa wote kwa kuwachukua mimba ni mimi? Unaniambiaje: Wachukue kifuani pako, kama mnyonyeshaji anavyobeba mtoto mchanga, uwapeleke katika nchi, uliyowaapia baba zao kuwapa?
13
Nitoe wapi nyama za kuwapa hao watu wote? Kwani wananililia kwamba: Tupe nyama, tule!
14
Mimi peke yangu siwezi kuwatunza watu hawa wote, ni mzigo unaonilemea na kunishinda.
15
Ukitaka kunifanyizia hivi, niue kabisa, kama nimeona upendeleo machoni pako, nisiendelee kuyaona haya mabaya yaliyonipata.
16
Bwana akamwambia Mose: Toa katika wazee wa Waisiraeli watu 70, uwakusanye kwangu, nao wawe watu, unaowajua, ya kuwa ndio wazee wa watu walio wenye amri, uwapeleke penye Hema la Mkutano, wajipange hapo pamoja na wewe.
17
Nami nitashuka, niseme hapo na wewe, nayo roho inayokukalia nitaichukua nusunusu na kuiweka juu yao, wajitwike pamoja na wewe mzigo wa kuwatunza watu hawa, usiuchukue peke yako tena.
18
Nao watu hawa waambie: Jitakaseni kuwa tayari kesho, mpate nyama! Kwani mmelia masikioni mwa Bwana kwamba: Yuko nani atakayetupa nyama, tule? kwani huko Misri tuliona mema. Bwana ndiye atakayewapa nyama, mle.
19
Nanyi hamtazila siku moja tu wala siku mbili wala siku tano wala siku kumi wala siku ishirini,
20
ila na mzile mwezi mzima, hata zitoke puani mwenu, hata ziwatapishe, kwa kuwa mmemkataa Bwana anayekaa katikati yenu, mlipomlilia kwamba: Kwa nini tumetoka Misri?
21
Mose akasema: Watu hawa, nilio nao hapa, ni watu 600000 wanaokwenda kwa miguu, nawe unasema: Nitawapa nyama, wale mwezi mzima!
22
Je? Itawezekana kuwachinjia kondoo na mbuzi na ng'ombe, wapate nyama za kutosha? Au inawezekana kuwakusanyia samaki wote wa baharini, wapate samaki nazo za kutosha?
23
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Je? Mkono wa Bwana umegeuka kuwa mfupi? Sasa utaona, kama neno langu linakupatia kitu, au kama ni la bure.
24
Kisha Mose akatoka, akawaambia watu hayo maneno ya Bwana; akatoa katika wazee wa Waisiraeli watu 70, akawakusanya, akawapanga, walizunguke Hema.
25
Ndipo, Bwana aliposhuka winguni kusema naye, nayo roho iliyomkalia akaichukua nusunusu, akawagawia hao wazee 70; ikawa, roho ilipotua juu yao, ndipo, walipofumbua mambo, lakini hawakuendelea.
26
Kulikuwa na watu wawili waliosalia makambini, mmoja jina lake Eldadi, wa pili jina lake Medadi, nao roho ikatua juu yao, kwani walikuwa wameandikwa, lakini hawakutokea Hemani, nao wakafumbua mambo makambini.
27
Ndipo, kijana alipopiga mbio kumpasha Mose habari kwamba: Eldadi na Medadi wamo makambini wakifumbua mambo.
28
Yosua, mwana wa Nuni, aliyekuwa mtumishi wake Mose tangu ujana wake, akajibu na kusema: Bwana wangu Mose, wakomeshe!
29
lakini Mose akamwambia: Wewe unaona wivu kwa ajili yangu mimi? Laiti watu wote wa Bwana wangekuwa wafumbuaji, Bwana akiwagawia roho yake!
30
Kisha Mose akarudi tena makambini yeye pamoja na hao wazee wa Waisiraeli.
31
Ndipo, upepo ulipotoka kwake Bwana, ukatoa tombo upande wa baharini, ukawatawanya po pote penye makambi, kupita katikati yao ulikuwa mwendo wa siku moja upande wa huku, nao upande wa huko ulikuwa mwendo wa siku moja, vivyo hivyo kuyazunguka makambi yote, tena juu ya nchi ilikuwa mikono miwili kuupima wingi wao.
32
Watu wakaondoka, wakawa wakiwaokota hao tombo mchana kutwa na usiku kucha, tena mchana wa kesho; aliyeokota machache aliokota frasila mia, wakawaanika pande zote za kuyazunguka makambi.
33
Lakini nyama zilipokuwa zingaliko vinywani mwao, zilipokuwa hazijaisha kutafunwa, ndipo, makali ya Bwana yalipowawakia hao watu, naye Bwana akawapiga hao watu pigo kubwa mno.
34
Kwa hiyo walipaita mahali pale Makaburi ya uchu, kwa kuwa walizika hapo watu waliouawa na Uchu mwingi.
35
Watu walipoondoka hapo penye Makaburi ya Uchu wakaenda Haseroti, wakakaa Haseroti.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36