bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 21
Numbers 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 22 →
1
Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyekaa upande wa kusini aliposikia, ya kuwa Waisiraeli wanakuja wakiifuata njia ya wapelelezi, akapigana nao Waisiraeli, akateka wengine wa kwao.
2
Ndipo, Waisiraeli walipomwapia Bwana kiapo cha kwamba: Ukiwatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo.
3
Bwana akazisikia sauti zao Waisiraeli, akawapa hao Wakanaani, nao wakawaangamiza wao pamoja na miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo; kwa hiyo wakapaita mahali pale Horma (Mwiko).
4
Kisha wakaondoka kwenye mlima wa Hori wakishika njia ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu, waizunguke nchi ya Edomu. Watu walipotaka kuzimia roho kwa kuchoka njiani,
5
wakamgombeza Mungu, hata Mose kwamba: Kwa nini mlitutoa Misri, tujifie huku nyikani? Kwani hakuna chakula wala maji, nazo roho zetu zinachukizwa na chakula hiki kikosacho nguvu.
6
Ndipo, Bwana alipotuma nyoka za moto kuwajia hao watu; nao walipowauma watu, wakafa watu wengi kwao Waisiraeli.
7
Ndipo, watu walipomjia Mose, wakasema: Tumekosa tulipomgombeza Bwana, hata wewe. Tuombee kwake Bwana, awaondoe hawa nyoka kwetu! Mose alipowaombea hao watu,
8
Bwana akamwambia Mose: Jitengenezee nyoka ya moto, uitungike kuwa kielekezo! Itakuwa, kila aliyeumwa na nyoka atakapoitazama atapona.
9
Mose akatengeneza nyoka ya shaba nyekundu, akaitungika kuwa kielekezo, ikawa hivyo: nyoka alipomwuma mtu, naye akaitazama hiyo nyoka ya shaba, akapona. Waisiraeli walipoondoka huko, wakapiga makambi Oboti.
10
Walipoondoka Oboti wakapiga makambi Iye-Abarimu katika nyika inayoelekea Moabu upande wa maawioni kwa jua.
11
Walipoondoka huko, wakapiga makambi kwenye kijito cha Zeredi.
12
Walipoondoka huko, wakapiga makambi kwenye kijito cha Zeredi.
13
Walipoondoka huko wakapiga makambi ng'ambo ya huko ya Arnoni ulioko nyikani, utokao mipakani kwa Waamori, kwani Arnoni ulikuwa mpaka wa Wamoabu kuwatenga Wamoabu na Waamori.
14
Kwa hiyo inasemwa katika kitabu cha vita vya Bwana:
15
Bonde la Sufa na vijito vya Arnoni, napo vijito vinaposhukia, panapopafikia napo mahali penye mji wa Ari ndipo panapouegemea mpaka wa Moabu.
16
Toka hapo wkafika Kisimani; ndiko kwenye kile kisima, Bwana alikomwambia Mose kwamba: Wakusanye watu, niwape maji!
17
siku zile Waisiraeli waliuimba wimbo huu:
18
Bubujika, kisima! Haya! Kiimbieni! Waliokichimba kisima hiki ndio wakuu; kweli majumbe wa watu ndio waliokifukua. kwa kutumia bakora na fimbo zao za kifalme. Toka huko nyikani wakaenda Matana.
19
Toka Matana wakaenda Nahalieli, toka Nahalieli wakaenda Bamoti,
20
toka Bamoti wakaenda bondeni kwenye mbuga za Moabu zilizoko kwenye mlima na Pisiga uelekeao jangwani.
21
Waisiraeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, kwamba:
22
Tunataka kupita katika nchi yako; hatutaondoka njiani kuingia mashambani au mizabibuni, wala hatutakunywa maji ya visimani, ila tunataka kuishika njia ya mfalme tu, hata tuupite mpaka wako mwingine.
23
Lakini Sihoni hakuwapa wana wa Isiraeli ruhusa kupita mipakani kwake, ila Sihoni akawakusanya watu wake wote, akatoka kwenda nyikani kuwazuia Waisiraeli. Alipofika Yasa akapigana nao Waisiraeli.
24
lakini Waisiraeli wakampiga kwa ukali wa panga, wakaichukua nchi yake toka mto wa Arnoni mpaka mto wa Yakobo, wana wa Amoni walikokaa, kwani mipaka yao wana wa Amoni ilikuwa yenye nguvu.
25
Waisiraeli wakaiteka hiyo miji yote, kisha Waisiraeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, namo Hesiboni na katika mitaa yake yote.
26
Kwani Hesiboni ulikuwa mji wa Sihoni, mfalme wa Waamori; naye aliupigania kale na mfalme wa Moabu, ndipo, alipoichukua hiyo nchi yake na kuitoa mkononi mwake mpaka mto wa Arnoni.
27
Kwa hiyo wenye kutunga mafumbo walisema: Njoni Hesiboni, mji wa Sihoni ujengwe na kutiwa nguvu!
28
Kwani moto umetoka Hesiboni, miali ya moto imetoka mjini mwa Sihoni, ikaula mji wa Ari wa Moabu nao wenyeji wa vilimani kwa Arnoni.
29
Umepatwa na mambo, wewe Moabu! Mmeangamia ninyi, watu wa Kemosi! Wamewakimbiza wana wenu wa kiume, nao wana wenu wa kike wamempa Sihoni, mfalme wa Waamori!
30
Tulipowapiga mishale, ndipo, Hesiboni ulipoangamia mpaka Diboni, tukaiharibu nchi mpaka Nofa, tukafika hata Medeba.
31
ndipo, Waisiraeli walipokaa katika nchi ya Waamori.
32
Kisha Mose akatuma watu kwenda Yazeri kupeleleza, nao wakaiteka mitaa yake na kuwafukuza Waamori waliokuwamo.
33
Kisha wakageuka, wakaishika njia ya kupanda Basani. Lakini Ogi, mfalme wa Basani, akatoka kuwazuia, yeye na watu wake wote, wakapigana huko Edirei.
34
Bwana akamwambia Mose: Usimwogope, kwani nimemtia mkononi mwako pamoja na watu wake wote, hata nchi yake, umfanyizie, kama ulivyomfanyizia Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni.
35
ndipo, walipompiga yeye na wanawe na watu wake wote, wasisaze kwake hata mmoja aliyeweza kukimbia, kisha wakaitwaa nchi yake.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36