bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 22
Numbers 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
1
Wana wa Isiraeli walipoondoka huko wakapiga makambi kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
2
Balaka, mwana wa Sipori, alipoyaona yote, Waisiraeli waliyowafanyizia Waamori,
3
Wamoabu wakaingiwa na woga mwingi sana wa hao watu kwa kuwa wengi sana, nao Wamoabu wakawastukia sana wana wa Isiraeli.
4
Ndipo, Wamoabu walipowaambia wazee wa Wamidiani: Makundi hayo yatameza yote yanayotuzunguka, kama ng'ombe anavyomeza majani ya porini. Ndipo, Balaka, mwana wa Sipori, aliyekuwa mfalme wa Wamoabu siku zile
5
alipotuma wajumbe kwenda Petori kwa Bileamu, mwana wa Beori, aliyekaa kwenye lile jito kubwa katika nchi yao walio ukoo wake, wamwite na kumwambia: Tazama, wako watu waliotoka Misri, nao wanaifunika nchi hii pote, unapotazama, tena wanakaa kunielekea mimi.
6
Sasa njoo, uniapizie watu hawa! Kwani wako na nguvu za kunishinda mimi. Hivyo labda nitaweza kuwapiga na kuwafukuza katika nchi hii, kwani ninajua: Utakayembariki atakuwa amebarikiwa, naye utakayemwapiza atakuwa ameapizwa.
7
Ndipo, wazee wa Wamoabu na wazee wa Wamidiani walipokwenda wakiushika mshahara wa uaguaji mikononi mwao; nao walipofika kwa Bileamu wakamwambia maneno ya Balaka.
8
Akawaambia: Laleni huku usiku huu! Nami na niwarudishie neno, kama Bwana atakavyoniambia. Kwa hiyo wale wakuu wa Wamoabu wakakaa kwake Bileamu.
9
Mungu akaja kwake Bileamu, akamwuliza: Watu hawa wanaokaa kwako ni watu gani?
10
Bileamu akamwambia Mungu: Balaka, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu
11
kwamba: Tazama, wako watu waliotoka Misri, nao wanaifunika nchi pote, unapotazama; sasa njoo, uniapizie watu hawa! Labda hivyo nitaweza kupigana nao na kuwafukuza.
12
Lakini Mungu akamwambia Bileamu: Usiende nao! Wala usiwaapize watu hao, kwani wamebarikiwa.
13
Bileamu alipoamka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaka: Nendeni zenu katika nchi yenu, kwani Bwana amekataa kunipa ruhusa kwenda nanyi.
14
Ndipo, wakuu wa Wamoabu walipoondoka; walipofika kwa Balaka wakamwambia: Bileamu amekataa kwenda na sisi.
15
Ndipo, Balaka alipotuma tena wakuu wengi wenye utukufu zaidi kuliko wale wa kwanza.
16
Walipofika kwa Bileamu wakamwambia: Hivi ndivyo, anavyosema Balaka, mwana wa Sipori: Usikatae kuja kwangu!
17
Kwani nitakuheshimu sanasana, nayo yote, utakayoniambia, nitayafanya; njoo tu, uniapizie hawa watu!
18
Bileamu akajibu, akawaambia watumishi wa Balaka: Ijapo Balaka anipe nyumba yake ijaayo fedha na dhahabu, sitaweza kukipita kinywa cha Bwana Mungu wangu, nifanye jambo dogo au kubwa.
19
Sasa nanyi kaeni hapa usiku huu, nijue, Bwana atakayoniambia tena!
20
Mungu akaja kwake Bileamu na usiku, akamwambia: Kama hawa watu wamekuja kukuita, inuka, uende nao! Lakini sharti ulifanye neno, nitakalokuambia.
21
Bileamu alipoondoka asubuhi akamtandika punda wake, akaenda nao wakuu wa Moabu.
22
Makali ya Mungu ayakawaka moto, kwa kuwa amekwenda; kwa hiyo malaika wa Bwana akaja, akajisimamisha njiani, ampinge; naye alikuwa amempanda punda wake, nao vijana wake wawili walikuwa naye.
23
Punda alipomwona malaika wa Bwana, akisimama njiani na kushika mkononi upanga uliochomolewa, punda akaondoka njiani na kuingia porini, naye Bileamu akampiga punda, amrudishe njiani.
24
Kisha malaika wa Bwana akasimama tena njiani penye mizabibu palipokuwa pembamba, kwa kuwa pande zote mbili palikuwa na kuta za mawe.
25
Punda alipomwona malaika wa Bwana akajisonga ukutani na kuuchubua mguu wa Bileamu; ndipo, alipompiga tena.
26
Naye malaika wa Bwana akapita tena, akaenda kusimama mahali pafinyu sana pasipowezekana kupitia wala kuumeni wala kushotoni.
27
Punda alipomwona malaika wa Bwana akalala chini, naye Bileamu alikuwa juu yake. Ndipo, makali ya Bileamu yalipomwakia, akampiga punda kwa fimbo.
28
Ndipo, Bwana alipokifumbua kinywa cha punda, akamwambia Bileamu: Nimekukosea nini, ukinipiga sasa mara ya tatu?
29
Bileamu akamwambia punda: Kumbe unanifyoza! Kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, ningekuua sasa hivi.
30
Naye punda akamwambia Bileamu: Je? Mimi si punda wako, uliyempanda siku zote za maisha yako hata siku hii ya leo? Nimezoa kukufanyizia hivyo? Akasema: La!
31
Ndipo, Bwana alipoyafumbua macho yake Bileamu, akamwona malaika wa Bwana, alivyosimama njiani na kushika mkononi upanga uliochomolewa; ndipo, alipomwinamia na kumwangukia kifudifudi.
32
Naye malaika wa Bwana akamwambia: Kwa nini umempiga punda wako sasa mara ya tatu? Tazama, mimi nimetoka, nikupinge. Kwani safari hii ni ya kuangamiza machoni pangu.
33
Punda aliponiona akaondoka njiani mbele yangu sasa mara ya tatu; kama asingaliondoka njiani mbele yangu, ningalikwisha kukuua wewe mwenyewe na kumponya yeye.
34
Ndipo, Bileamu alipomwambia malaika wa Bwana: Nimekosa, kwani sikujua, ya kuwa wewe umesimama njiani, unipinge; sasa kama safari hii ni mbaya machoni pako, nitarudi.
35
Naye malaika wa Bwana akamwambia Bileamu: Jiendee pamoja na watu hawa! Lakini sharti uliseme neno hilo tu, nitakalokuambia. Kisha Bileamu akaenda na wale wakuu wa Balaka.
36
Balaka aliposikia, ya kama Bileamu anakuja, akatoka kumwendea njiani mpaka kwenye mji wa Moabu ulioko mahali penye mto wa Arnoni ulioko kwenye mapeo ya mpaka.
37
Balaka akamwuliza Bileamu: Sikutuma kwako vizuri, nikuite? Mbona hukuja kwangu? Labda unaniwazia kuwa mtu asiyeweza kukupa macheo?
38
Naye Bileamu akamwambia Balaka: Tazama, nimefika kwako! Lakini sasa je? nitaweza kusema lo lote? Neno hilo tu, Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo, nitakalolisema.
39
Kisha Bileamu akaenda na Balaka, wakaingia Kiriati-Husoti (Mji wenye Mabarabara).
40
Balaka akachinja ng'ombe na kondoo kuwa ng'ombe za tambiko, akamgawia hata Bileamu nyama, hata wakuu waliokuwa naye.
41
Ilipokuwa asubuhi, Balaka akamchukua Bileamu, akampeleka juu vilimani kwa Baali; huko ndiko, alikowaona watu hao hata mwisho wa makambi yao.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36