bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 35
Numbers 35
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 36 →
1
Kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waagize wana wa Isiraeli, wawape Walawi katika mafungu yao, watakayoyachukua, miji ya kukaa, nayo malisho yanayoizunguka hiyo miji mwape Walawi!
3
Hiyo miji iwe yao ya kukaa, nayo malisho yawe ya ng'ombe wao na ya mbuzi na ya kondoo wao na ya nyama wao wengine wote.
4
Hayo malisho ya miji, mtakayowapa Walawi, upana wao kutoka penye boma la mji kwenda nje sharti uwe mikono elfu kuuzunguka mji.
5
Kwa hiyo na mpime huko nje ya mji upande wa maawioni kwa jua mikono 2000, nao upande wa kusini mikono 2000, nao upande wa baharini mikono 2000, nao upande wa kaskazini mikono 2000; nao mji uwe katikati; hayo na yawe malisho yao penye miji yao.
6
Katika hiyo miji, mtakayowapa Walawi, sharti mwape miji sita ya kuikimbilia; hiyo mwape kwamba: mwuaji apate kuikimbilia. Pasipo kuihesabu hiyo mwape miji 42.
7
Hivyo miji yote, mtakayowapa Walawi, itakuwa 48, ndiyo hiyo miji yenyewe pamoja na malisho yao.
8
Mtakapoitoa hiyo miji katika mafungu, wana wa Isiraeli watakayoyachukua, yawe yao, kwao walio wengi na mtoe mingi, nako kwao walio wachache na mtoe michache; kila shina na litoe kwa ukuu wa fungu lake, litakalolipata kuwa lake, liwagawie Walawi miji ya kwao.
9
Bwana akamwambia Mose kwamba:
10
Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Hapo, mtakapouvuka Yordani na kuingia katika nchi ya Kanaani,
11
jichagulieni miji itakayowafalia ninyi kuwa miji ya kuikimbilia, mwuaji apate kuikimbilia, kama hakumpiga mwenziwe na kumwua kwa kusudi.
12
Miji hiyo iwe kwenu ya kuikimbilia na kumkimbia mlipizi, mwuaji asife, mpaka asimamishwe mbele ya mkutano, ahukumiwe nao.
13
Nayo miji, mtakayoitoa kuwa miji ya kuikimbilia, sharti iwe sita kwenu.
14
Miji mitatu na mtoe ng'ambo ya huku ya Yordani, tena na mtoe miji mitatu katika nchi ya Kanaani, iwe miji ya kuikimbilia.
15
Miji hiyo sita iwe ya kuikimbilia wana wa Isiraeli, nao wageni, nao watakaokaa kwao, wapate kuikimbilia wote wasioua mtu kwa kusudi.
16
Lakini kama mtu amempiga mwenzake kwa chombo cha chuma, akafa, yule ni mwuaji, naye kwa kuwa ni mwuaji, hana budi kuuawa.
17
Kama amempiga kwa jiwe, alilolishika, linaloweza kuua mtu, yule akafa, basi, ni mwuaji, naye kwa kuwa ni mwuaji, hana budi kuuawa.
18
kama amempiga kwa chombo cha mti, alichokishika mkononi, kinachoweza kuua mtu, akafa, basi, ni mwuaji, naye kwa kuwa ni mwuaji, hana budi kuuawa.
19
Mwenye kuilipiza hiyo damu na amwue mwuaji; hapo, atakapomkuta yeye, na amwue.
20
Tena mtu akimkumba mwenzake kwa kumchukia, au akimtupia kitu kwa kumvizia, yule akafa,
21
au akimpiga kwa mkono wake kwa uadui, yule akafa, basi, yule aliyempiga hana budi kuuawa, kwa kuwa ni mwuaji; naye mwenye kuilipiza hiyo damu na amwue huyo mwuaji hapo, atakapomkuta.
22
Lakini kama amemkumba kwa mara moja tu pasipo kuvijua, isipokuwa kwa uadui, au kama amemtupia kitu cho chote pasipo kumvizia,
23
au kama ameacha pasipo kumwona, jiwe lo lote linaloweza kumwua mtu limwangukie, naye yule akafa asipokuwa wala adui wake wala mwenye kumtakia baya,
24
basi, wao wa mkutano watamwamulia yule aliyeua naye mwenye kuilipiza hiyo damu, wakiyafuata hayo maamuzi.
25
Nao wa mkutano watamponya huyo aliyeua mikononi mwake mwenye kuilipiza hiyo damu, kisha wao wa mkutano na wamrudishe katika mji wa kuukimbilia, alimokimbilia, naye atakaa humo, mpaka atakapokufa mtambikaji mkuu, waliyempaka mafuta matakatifu.
26
lakini kama yule mwuaji atatoka mipakani mwa mji wa kuukimbilia, alimokimbilia,
27
naye mwenye kuilipiza hiyo damu akamwona nje ya mipaka ya huo mji, alimokimbilia, basi, mwenye kuilipiza hiyo damu atamwua huyo mwuaji pasipo kukora manza za damu.
28
Kwani ilimpasa kukaa mle mjini, alimokimbilia, mpaka mtambikaji mkuu atakapokufa. Mtambikaji mkuu atakapokwisha kufa, huyo mwuaji naye atarudi kwao kwenye fungu lake, alilolichukua, liwe lake.
29
Haya sharti yawe kwenu maongozi ya maamuzi ya vizazi vyenu po pote, mtakapokaa.
30
Kila atakayemwua mwenziwe sharti wamwue huyo mwuaji kwa ushahidi wao walioviona, lakini shahidi mmoja asitoshe wa kuua mtu.
31
Tena msichukue makombozi ya mtu mwuaji aliyekora manza za kufa, hana budi kuuawa.
32
Wala msichukue makombozi ya mtu aliyekimbilia mji wa kuukimbilia, kwamba apate kurudi na kukaa kwao, mtambikaji akiwa hajafa bado.
33
Wala msiipatie uchafu hiyo nchi, mtakayoiingia. Kwani damu huipatia nchi uchafu, tena haiwezekani kuipatia hiyo nchi upozi wa hiyo damu iliyomwagika kwake, isipokuwa kwa damu yake yeye aliyeimwaga hiyo damu.
34
Kwa hiyo msiichafue hiyo nchi, ninyi mtakayoikaa, mimi nami nitakakokaa; kwani mimi Bwana nitakaa katikati ya wana wa Isiraeli.
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 36 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36