bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 18
Numbers 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 19 →
1
Bwana akamwambia Haroni: Wewe na wanao na mlango wa baba yako pamoja na wewe mtatwikwa maovu yatakayoonekana Patakatifu; tena wewe pamoja na wanao mtatwikwa maovu ya utambikaji wenu.
2
Nao ndugu wa shina la Lawi lililo shina la baba yako uwachukue, waandamane na wewe na kukutumikia wewe pamoja na wanao, mkifanya kazi zenu mbele ya Hema la Ushahidi.
3
Kazi zao zinazowapasa kuziangalia ni kukuangalia wewe na kuliangalia Hema lote, wasikaribie tu vyombo vya Patakatifu na meza ya kutambikia, wasife wao nao pamoja nanyi.
4
Sharti waandamane na wewe, waziangalie kazi za Hema la Mkutano ziwapasazo kuziangalia za utumishi wote wa kulitumikia Hema, lakini mgeni asiwakaribie ninyi.
5
Kazi zenu zinazowapasa ninyi kuziangalia ni kupaangalia Patakatifu na kuiangalia meza ya kutambikia, makali yangu yasiwatokee tena wana wa Isiraeli.
6
Tazama, mimi nimewatoa ndugu zenu Walawi katikati yao wana wa Isiraeli, nikawapa ninyi kuwa vipaji vya Bwana kwa kuutumikia utumishi wote wa Hema la Mkutano.
7
Nawe wewe pamoja na wanao sharti mwuangalie utambikaji wenu, mfanye kazi zote za utumishi za meza ya kutambikia nazo za Chumbani mbele ya pazia, kwani ninawapa utambikaji wenu kuwa kipaji mlichopewa, lakini mgeni atakayeukaribia hana budi kuuawa.
8
Bwana akamwambia Haroni: Tazama, mimi nimekupa kuviangalia vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa, ninavyotolewa; kwa hiyo ninakupa vipaji vitakatifu vyote, wana wa Isiraeli wanavyovitoa, kuwa ujira wako wewe na wa wanao wa kupakwa mafuta. Hii na iwe haki yenu ya kale na kale.
9
Vitakavyokuwa vitakatifu vyenyewe vitakuwa vyako, visichomwe moto, navyo ni hivi: matoleo yao yote, vilaji vyao vya tambiko na ng'ombe zao za tambiko za weuo nazo za upozi, watakazonitolea mimi, ni matakatifu yenyewe kuwa yako na ya wanao.
10
Na myale mahali palipo patakatifu penyewe; wote walio wa kiume na wayale, na yawe matakatifu yako.
11
Tena ninakupa wewe na wanao wa kiume na wa kike kuwa vyenu: vipaji vyao vya tambiko, wanavyovitoa vya kunyanyuliwa, navyo vipaji vya tambiko vya wana wa Isiraeli vya kupitishwa motoni viwe vyako; hii na iwe haki yenu ya kale na kale. Kila atakayekuwa nyumbani mwako, akiwa ametakata, na avile.
12
Tena mafuta yote yaliyo mazuri mno nazo mvinyo mbichi zilizo nzuri mno nazo ngano, watakazomtolea Bwana za malimbuko, ninakupa wewe.
13
Nayo mazao yote ya kwanza ya nchi yao, watakayomtolea Bwana, yatakuwa yako; kila atakayekuwa nyumbani mwako, akiwa ametakata, na ayale.
14
Navyo vyo vyote vitakavyotiwa mwiko wa kuwa vyao Waisiraeli vitakuwa vyako.
15
Naye kila mwana wa kwanza wa mama yake, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga, atakuwa wako kwao wote walio wenye miili ya nyama, watu watakaomtolea Bwana, lakini mwana wa mtu utamtoa, akombolewe, vilevile mwana wa nyama aliye mwenye uchafu utamtoa, akombolewe.
16
Akiwa mwenye mwezi mmoja utamtoa, akombolewe kwa hivyo, utakavyompima kiasi chake cha fedha, walipe kama fedha tano, lakini fedha hizo zinazotumika Patakatifu, fedha moja kwa thumuni nane.
17
Lakini wana wa kwanza wa ng'ombe au wa kondoo au wa mbuzi usiwatoe kukombolewa, kwani ndio watakatifu; damu zao sharti uzinyunyizie meza ya kutambikia, nayo mafuta yao sharti uyachome moto kuwa mnuko mzuri wa moto wa kumpendeza Bwana.
18
Lakini nyama zao zitakuwa zako, kama vidari vilivyo vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni au kama mapaja ya kuume yalivyo yako.
19
Tena ninakupa vipaji vitakatifu vyote, wana wa Isiraeli watakavyomtolea Bwana kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa; hivi ninakupa wewe pamoja na wanao wa kiume na wa kike; hii na iwe haki yenu ya kale na kale. Hili sharti liwe agano la kale na kale lisilochujuka kama chumvi, nalo umewekewa wewe pamoja na wanao mbele ya Bwana.
20
Kisha Bwana akamwambia Haroni: Katika nchi yao wewe hutapata fungu la nchi litakalokuwa fungu lako katikati yao; mimi ni fungu lako, utakalolipata kuwa lako katikati ya wana wa Isiraeli.
21
Tena tazama: Wana wa Lawi ninawapa mafungu ya kumi yote yatakayotolewa nao Waisiraeli kuwa fungu lao, ni ujira wa utumishi wao wa kufanya kazi za utumishi wa Hema la Mkutano.
22
Lakini tangu sasa wana wa Isiraeli wasilifikie tena Hema la Mkutano karibu, wasijikoseshe, wakajipatia kufa.
23
Ila Walawi tu na wazifanye kazi za utumishi wa Hema la Mkutano, nao ndio watakaotwikwa manza, watakazozikora. Haya sharti yawe maongozi ya kale na kale ya kuviongoza vizazi vyenu, nanyi hamtapata fungu la nchi kuwa lenu katikati ya wana wa Isiraeli.
24
Kwani ninawapa Walawi mafungu ya kumi, wana wa Isiraeli watakayoyatoa kuwa vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana; haya ninawapa Walawi kuwa fungu lao, kwa hiyo ninawaambia: Hamtapata fungu la nchi kuwa lenu katikati ya wana wa Isiraeli.
25
Bwana akamwambia Mose kwamba:
26
Sema nao Walawi, uwaambie: Mtakapoyachukua mafungu ya kumi kwao wana wa Isiraeli, niliyowapa ninyi kuwa fungu lenu kwao, nanyi sharti mtoe humo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana, navyo sharti viwe fungu la kumi la hayo mafungu ya kumi.
27
Navyo hivyo vpaji vyenu vya tambiko vitawaziwa kuwa ngano zenu za mapurio yenu au mafuriko ya makamulio yenu.
28
Nanyi mtakapovitoa hivyo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana vya mafungu yenu ya kumi, mtakayoyachukua kwa wana wa Isiraeli, sharti m mpe mtambikaji Haroni hivyo vipaji vya tambiko, mtakavyovitoa kwenu vya kumnyanyulia Bwana.
29
Katika vipaji vyote, mtakavyopewa, sharti mtoe vipaji vya tambiko vyote viwapasavyo kuvitoa vya kumnyanyulia Bwana, nanyi sharti mtoe vile vitakavyokuwa vizuri zaidi vinavyopasa kutolewa humo kuwa vipaji vitakatifu.
30
Kwa hiyo uwaambie: Mtakapotoa humo vilivyo vizuri zaidi kuwa vipaji vyenu vya tambiko vya kunyanyuliwa, vitawaziwa kuwa mapato ya Walawi ya mapurio yao na mapato ya makamulio yao.
31
Nanyi na mvile mahali po pote ninyi nao walio wa milango yenu, kwani ni mishahara yenu ya utumishi wenu wa Hema la Mkutano.
32
Mtakapovitoa vilivyo vizuri zaidi katika mapato yenu kuwa vipaji vya tambiko, basi, hamtajikosesha kwa ajili yao, wala hamtavichafua vipaji vitakatifu vya wana wa Isiraeli, msife.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36