bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 29
Numbers 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
1
Siku ya kwanza ya mwezi wa saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi, iwe sikukuu yenu ya Shangwe.
2
Hapo na mtoe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza Bwana: dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
3
Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume la ng'ombe na vibaba sita vya dume la kondoo,
4
na vibaba vitatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
5
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kuwapatia ninyi upozi.
6
Hao na mtoe pamoja na ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima za mwandamo wa mwezi pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao vya tambiko, kama ilivyo desturi yao kuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
7
Siku ya kumi ya mwezi huo wa saba na mkutanie Patakatifu na kujitesa kwa kufunga, msifanye kazi yo yote,
8
ila mtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza: dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
9
Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume la ng'ombe na vibaba sita vya dume moja la kondoo,
10
na vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
11
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya weuo ya sikukuu ya Mapoza na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao ya tambiko.
12
Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi, ila mzile hizo sikukuu za Bwana siku saba.
13
Hapo na mtoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana: madume kumi na matatu ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
14
Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe wa wale madume ya ng'ombe kumi na matatu na vibaba sita vya dume moja la kondoo wa wale madume mawili ya kondoo,
15
na vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo kumi na wanne.
16
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
17
Siku ya pili na mtoe madume kumi na mawili ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
18
Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe navyo vya madume ya kondoo navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
19
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao vya tambiko.
20
Siku ya tatu na mtoe madume kumi na moja ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
21
Navyo vilaji na vinywaji vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
22
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambik ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
23
Siku ya nne na mtoe madume kumi ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
24
Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
25
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
26
Siku ya tano na mtoe madume tisa ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
27
Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
28
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
29
Siku ya sita na mtoe madume manane ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana mbuzi kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
30
Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
31
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
32
Siku ya saba na mtoe madume saba ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
33
Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
34
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
35
Siku ya nane na iwe ya mkutano mkuu kwenu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,
36
ila mtoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana: dume moja la ng'ombe na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
37
Navyo vilaji na vinywaji vyote vya tambiko vya yule dume la ng'ombe, navyo vya yule dume la kondoo, navyo vya wale wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
38
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
39
Hizo ndizo ng'ombe za tambiko, mtakazomtolea Bwana, sikukuu zenu zitakapotimia; tena ziko zile, mtakazozitoa kwa kuapa au kwa kupenda wenyewe kuwa ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima au vilaji au vinywaji vyenu vya tambiko au ng'ombe zenu za tambiko za shukrani.
40
Mose akawaambia wana wa Isiraeli haya yote, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36