bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 15
Numbers 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapoingia katika nchi yenu ya kukaa, ninayotaka kuwapa,
3
hapo mtakapomtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima au za kuchinjwa, kama ni za kuyalipa, mtu aliyoyaapa, au kama ni za kupenda kwa moyo tu, au kama ni za sikukuu zenu, amtengenezee Bwana mnuko wa kumpendeza, kama anatoa ng'ombe au mbuzi au kondoo,
4
basi, huyo mwenye kumtoa na ampelekee Bwana toleo lake pamoja na kilaji cha tambiko, nacho kiwe vibaba vitatu vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na kibaba kimoja cha mafuta,
5
tena kibaba kimoja cha mvinyo kuwa kinywaji cha tambiko, kama ni cha ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, au kama ni ya kuchinjwa, nacho kiwe hivyo cha kila mwana kondoo mmoja.
6
lakini kama ni dume la kondoo, utengeneze kilaji chake cha tambiko kuwa vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na kibaba kimoja na nusu cha mafuta.
7
Nacho kinywaji chake cha tambiko kiwe kibaba kimoja na nusu cha mvinyo; ukimtolea Bwana hivi, vitakuwa mnuko wa kumpendeza.
8
Lakini kama utatengeneza ndama kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima au ya kuchinjwa ya kuyalipa, aliyoyaapa, au ya kumshukuru Bwana,
9
utoe pamoja na ndama kilaji cha tambiko cha vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na vibaba viwili vya mafuta.
10
Tena utoe vibaba viwili vya mvinyo kuwa kinywaji cha tambiko; ukivichoma moto vitakuwa mnuko wa kumpendeza Bwana.
11
Hivi uvitengenezee kila ng'ombe mmoja au kila dume moja la kondoo au kila mwana kondoo au kila mwana mbuzi.
12
Kwa hesabu yao hao, mtakaowatengeneza, kwa hesabu iyo hiyo sharti mmtengenezee kila mmoja kilaji na kinywaji chake cha tambiko.
13
Kila mwenyeji sharti avitengeneze vivyo hivyo akitaka kumtolea Bwana ng'ombe ya tambiko kuwa mnuko wa moto wa kumpendeza.
14
Kama kwenu yuko mgeni au mwingine anayekaa siku zote kwao walio vizazi vyenu, naye akitaka kumtengenezea Bwana ng'ombe ya tambiko kuwa mnuko wa moto wa kumpendeza, na aitengeneze vivyo hivyo, kama ninyi mnavyoitengeneza.
15
Maongozi yawe yayo hayo ya mkutano wote, kama ni ninyi wenyewe au kama ni mgeni akaaye ugenini kwenu; maongozi haya yawe ya kale na kale ya kuviongoza vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo mbele ya Bwana, ndivyo, naye mgeni atakavyokuwa mbele yake.
16
Nayo maonyo na maamuzi yawe yayo hayo ya ninyi wenyewe na ya mgeni atakayekaa ugenini kwenu.
17
Bwana akamwambia Mose kwamba:
18
Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapoingia katika nchi ile, mimi nitakakowaingiza,
19
mtakapokula mikate ya nchi hiyo, sharti mmtolee Bwana vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa.
20
Mlimbuko wa unga wenu wa chengachenga uwe andazi, mtakalolitoa kuwa kipaji cha tambiko cha kunyanyuliwa, nacho mkitoe vivyo hivyo, kama mnavyokitoa kipaji cha tambiko cha kunyanyuliwa kitokacho penye kupuria ngano.
21
Hivyo ndivyo, mtakavyompa Bwana malimbuko ya unga wenu wa chengachenga kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa.
22
Ikiwa kwa kupotelewa, msiyafanye hayo maagizo yote, Bwana aliyomwambia Mose,
23
nayo hayo yote, Bwana aliyowaagiza ninyi kinywani mwa Mose tangu siku ile, Bwana alipoanza kuwaagiza maneno, nayo aliyoyaagiza baadaye kwa vizazi na vizazi,
24
kama ni makosa yaliyofanyika kwa kupotelewa tu, ikiwa wao wa mkutano hawakuyaona, basi, mkutano wote na utengeneze dume moja la ng'ombe aliye kijana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima kuwa mnuko wa kumpendeza Bwana; waitoe pamoja na kilaji na kinywaji chake cha tambiko, kama ilivyo desturi, tena watoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
25
Naye mtambikaji na aupatie upozi mkutano wote wa wana wa Isiraeli, waondolewe hayo makosa, kwani walipotelewa tu. Nao wenyewe na wayapeleke matoleo yao kuwa ng'ombe za tambiko za Bwana za kuteketezwa, nazo ng'ombe za tambiko za weuo wao na wamtolee Bwana usoni pake kwa ajili ya kupotelewa kwao.
26
Hivyo ndivyo, wao wa mkutano wote wa wana wa Isiraeli pamoja na wageni watakaokaa ugenini kwao watakavyoondolewa makosa, kwa kuwa watu wote walikuwa wamepotelewa.
27
Kama mtu mmoja anakosa kwa kupotelewa, na atoe mbuzi jike wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
28
Naye mtambikaji na ampatie upozi mtu huyo aliyepotelewa, akitoa mbele ya Bwana ng'ombe ya tambiko ya kumweua kwa ajili ya kupotelewa kwake; akimpatia upozi hivyo, ataondolewa kosa lake.
29
Kama ni mwenyeji wa wana wa Isiraeli, au kama ni mgeni atakayekaa ugenini kwenu, maongozi yawe yayo hayo ya kuwafanyizia waliokosa kwa kupotelewa.
30
Lakini mtu akikosa kwa kusudi, kama ni mwenyeji, au kama ni mgeni, huyo anamtukana Bwana, kwa hiyo mtu aliye hivyo sharti ang'olewe katikati yao walio ukoo wake,
31
kwani amelibeza Neno la Bwana na kuyavunja maagizo yake. Mtu aliye hivyo hana budi kung'olewa kabisa na kutwikwa manza, alizozikora.
32
Wana wa Isiraeli walipokuwa nyikani waliona mtu, akiokota kuni siku ya mapumziko.
33
Waliomwona, alivyookota kuni, wakampeleka kwa Mose na Haroni na kwa mkutano wote.
34
Wakamweka kifungoni, kwani haijaelekea bado, mtu kama huyu atakayofanyiziwa.
35
Bwana akamwambia Mose: Mtu huyu hana budi kuuawa, wao wote wa mkutano na wampige mawe nje ya makambi.
36
Ndipo, wao wote wa mkutano walipomtoa na kumpeleka nje ya makambi, wakampiga mawe, hata akafa, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
37
Bwana akmwambia Mose kwamba:
38
Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie, wajifanyizie vishada penye ncha za mavazi yao, wao na vizazi vyao, kisha juu ya hivyo vishada watie nyuzi za rangi za nguo za kifalme.
39
Maana ya hivyo vishada vyenu ni hii: mtakapoviona, myakumbuke maagizo yote ya Bwana, myafanye, msizifuate tamaa za mioyo yenu na za macho yenu, kwani mkizifuata hufanya ugoni.
40
Kwa hiyo yakumbukeni maagizo yangu na kuyafanya, mpate kuwa watakatifu wa Mungu wenu.
41
Mimi Bwana ni Mungu wenu aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri, niwe Mungu wenu; kweli mimi Bwana ni Mungu wenu.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36