bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 23
Numbers 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 24 →
1
Bileamu akamwambia Balaka: Nijengee hapa mahali saba pa kutambikia, kisha nipate hapa madume saba ya ng'ombe na madume saba ya kondoo.
2
Balaka akafanya, kama Bileamu alivyosema, kisha Balaka na Bileamu wakatoa kila mahali pa kutambikia ng'ombe mmoja na kondoo mmoja.
3
Naye Bileamu akamwambia Balaka: Simama penye ng'ombe yako ya tambiko! Lakini mimi nitakwenda, labda Bwana atakuja kunikuta; ndipo, nitakapokuambia hilo neno, atakalonionyesha. Kisha akaenda kilimani palipo peupe.
4
Mungu alipokuja kweli kukutana na Bileamu njiani, huyu akamwambia: Nimetengeneza mahali saba pa kutambikia, nikatoa ng'ombe mmoja na kondoo mmoja kila mahali pamoja pa kutambikia.
5
Naye Bwana akampa Bileamu maneno ya kuyasema kwa kinywa chake, kisha akamwambia: Rudi kwa Balaka, uyaseme maneno yayo hayo!
6
Aliporudi kwake akamwona, akisimama penye ng'ombe yake ya tambiko, yeye na wakuu wote wa Moabu.
7
Ndipo, alipoanza kusema maneno yake kwamba: Huko Aramu ndiko, alikonichukua Balaka; mfalme wa Moabu amenitoa milimani upande wa maawioni kwa jua akisema: Njoo, uniapizie Yakobo! Njoo, umchafukie Isiraeli!
8
Lakini, Mungu asiyemwapiza nitamwapizaje? Bwana asiyemchafukia nitamchafukiaje?
9
Hapa juu miambani ninawaona, hapa vilimani ninawachungulia; ndio watu wakaao peke yao, hawajiwazii kuwa sawa na wamizimu.
10
Yuko nani awezaye kuyahesabu mavumbi yake Yakobo au kujua tu hesabu ya fungu la nne la Isiraeli? Kama hawa wanyofu wanavyokufa, ningetaka kufa hivyo, ningependa, mwisho wangu uwe kama mwisho wao.
11
Ndipo, Balaka alipomwambia Bileamu: Umenifanyizia nini? Nimekuchukua, uwaapize adui zangu, kumbe umewabariki!
12
Akajibu kwamba: Hainipasi kuangalia, niyaseme yaleyale, Bwana aliyoyatia kinywani mwangu?
13
Ndipo, Balaka alipomwambia: Nenda pamoja na mimi mahali pengine, utakapowaona wote; sasa unaona mwisho wao tu, huwaoni wote; hapo ndipo, utakaponiapizia watu hawa.
14
Kisha akamchukua, akampeleka juu mlimani kwa Pisiga kulikokuwa uwanda wa wachunguliaji. Huko nako akajenga mahali saba pa kutambikia, kisha akatoa kila mahali pa kutambikia ng'ombe mmoja na kondoo mmoja.
15
Kisha Bileamu akamwambia Balaka: Simama hapa penye ng'ombe yako ya tambiko! Lakini mimi nitakwenda huko kumkuta Bwana.
16
Naye Bwana akaja kweli kumkuta Bileamu, akampa maneno ya kuyasema kwa kinywa chake, kisha akamwambia: Rudi kwa Balaka, uyaseme maneno yayo hayo!
17
Aliporudi kwake akamwona, akisimama penye ng'ombe yake ya tambiko pamoja na wakuu wote wa Moabu. Balaka alipomwuliza: Bwana amesema nini?
18
akaanza kusema maneno yake kwamba: Inuka, Balaka, usikie! Nitegee sikio lako, mwana wa Sipori!
19
Mungu si mtu, aseme uwongo, si mwana wa mtu, ageuze moyo. Yeye aseme neno, asilifanye? Aweke agano, asilitimize?
20
Tazameni! Nimepewa kubariki; napo, alipobariki, siwezi kuyageuza.
21
Hakuna aliyepata kutazama mambo yaliyo ya bure kwake Yakobo, wala hakuna aliyeona masumbuko kwake Isiraeli; Bwana Mungu wake yuko pamoja naye, nayo mashangilio ya mfalme husikilika kwao.
22
Mungu ndiye aliyewatoa Misri, naye anazo nguvu kama za nyati.
23
Kweli hakuna uganga wa kumwangamiza Yakobo, wala hakuna uaguaji wa kumponza Isiraeli, siku zote Yakobo na Isiraeli huambiwa, Mungu anayoyafanya.
24
Na mwone, watu hawa wakiinuka kama simba mke, wakijisimamisha kama simba mume! Halali, mpaka ale nyama zao, aliowararua, mpaka anywe damu zao, aliowaua.
25
Ndipo, Balaka alipomwambia Bileamu: Usipoweza kuwaapiza, uache kuwabariki!
26
Lakini Bileamu akamjibu Balaka kwamba: Sikukuambia kwamba: Yote, Bwana atakayoyasema, nitayafanya?
27
Ndipo, Balaka alipomwambia Bileamu: Njoo, nikupeleke mahali pengine, labda huko utanyoka machoni pake Mungu, ukiniapizia huko watu hawa.
28
Kisha Balaka akamchukua Bileamu, akampeleka juu mlimani kwa Peori kunakoelekea jangwani.
29
Huko Bileamu akamwambia Balaka: Nijengee hapa mahali saba pa kutambikia! Kisha unipatie hapa madume saba ya ng'ombe na madume saba ya kondoo.
30
Balaka akafanya, kama Bileamu alivyosema, akatoa kila mahali pa kutambikia ng'ombe mmoja na kondoo mmoja.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36