bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 24
Numbers 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
1
Bileamu alipoona, ya kuwa imekuwa vema machoni pa Bwana kuwabariki Waisiraeli, hakwenda tena kama mara ya kwanza na mara ya pili kutafuta mambo ya kuagulia, ila akauelekeza uso wake jangwani.
2
Bileamu alipoyainua huko macho yake akawaona Waisiraeli, walivyokaa shina kwa shina; ndipo, roho ya Mungu ilipomjia,
3
akaanza kusema maneno yake kwamba: Hivi ndivyo, asemavyo Bileamu, mwana wa Peori, hivi ndivyo, asemavyo mtu aliyefumbwa macho.
4
Hivi ndivyo, asemavyo aliyesikia maneno ya Mungu, aliyeona maono yake aliye Mwenyezi, aliyefumbuliwa macho alipomwangukia:
5
Mahema yako, Yakobo, ni mema peke yao, nayo makao yako, wewe Isiraeli.
6
Huwa kama mabonde yanayoendelea mbali, huwa kama mashamba yaliyoko kando ya mto, huwa kama misagawi, Bwana aliyoipanda, huwa kama miangati iliyoko kwenye maji!
7
Ndoo zake huchuruzisha maji mengi, nazo mbegu zake hunyweshwa maji mengi. Mfalme wake ni mkuu kuliko Agagi, nao ufalme wake utatukuka sana.
8
Mungu ndiye aliyemtoa Misri, naye anazo nguvu kama za nyati, hula wamizimu wanaomsonga, nayo mifupa yao huipondaponda, akiwaangusha chini kwa mishale yake.
9
Kama simba mume au simba mke anavyootea, ndivyo, anavyolala; yuko nani atakayemwinua? Mwenye kukubariki amekwisha kubarikiwa naye, mwenye kukuapiza amekwisha kuapizwa naye.
10
Ndipo, makali ya Balaka yalipomwakia Bileamu, akayapiga makofi yake, kisha Balaka akamwambia Bileamu: Nimekuita, uwaapize adui zangu, kumbe umewabariki sasa mara ya tatu!
11
Sasa jiendee upesi mahali pako! Nalisema moyoni: Nitakuheshimu sana, lakini tazama, Bwana amekunyima hizo heshima.
12
Naye Bileamu akamwambia Balaka: Je? Wajumbe wako, uliowatuma kwangu, sikuwaambia kwamba:
13
Ijapo Balaka anipe nyumba yake ijaayo fedha na dhahabu, sitaweza kukipita kinywa cha Bwana, nifanye jambo baya au jema, kama moyo wangu unavyotaka; ila Bwana atakaloniambia, ndilo hilo, nitakalolisema?
14
Sasa tazama, ninakwenda zangu kwa watu wa kwetu; lakini kwanza nitakuonyesha, watu wa ukoo huu watakavyowafanyizia watu wako siku zitakazokuja baadaye.
15
Kisha akaanza kusema maneno yake kwamba: Hivi ndivyo, asemavyo Bileamu, mwana wa Peori, hivi ndivyo, asemavyo mtu aliyefumbwa macho.
16
Hivi ndivyo, asemavyo aliyesikia maneno ya Mungu, ajuaye kumtambua Alioko huko juu, aliyeona maono yake aliye Mwenyezi, aliyefumbuliwa macho alipomwangukia:
17
Ninamtazamia, lakini hayuko sasa, ninamchungulia, lakini hayuko karibu. Nyota itatokea kwake Yakobo, nayo bakora ya kifalme itainuka kwake Isiraeli, izivunje pande zote mbili zao Wamoabu na kuwamaliza wana wao wote wapigao vita.
18
Nayo nchi ya Edomu itakuwa yake yeye, nayo ya Seiri itakuwa yake yeye, nayo ndiyo iliyokuwa yao adui zake! Kweli Isiraeli atatenda nguvu.
19
Mwenye kutawala atatoka mwake Yakobo, nao waliokimbia na kutoka mijini atawaangamiza.
20
Alipowaona Waamaleki akaanza kusema maneno yake kwamba: Walio wa kwanza wa wamizimu ndio Waamaleki, lakini mwisho wao utakuwa kuangamia tu.
21
Alipowaona Wakeni akaanza kusema maneno yake kwamba: Kao lako limeshupaa, tundu lako umelijenga mwambani,
22
lakini havikuponyi, Kaini, utateketea, bado kidogo Waasuri watakuteka.
23
Kisha akasema maneno yake mengine kwamba: Hoi! Yuko nani atakayepona, yatakapowapata? Nayo yatawapata hapo, Mungu atakapoyatimiza.
24
Merikebu zitatoka kwao Wakiti, ziwanyenyekeze Waasuri, ziwanyenyekeze hata Waeberi, mpaka waangamie nao.
25
Kisha Bileamu akaondoka kwenda kurudi kwao, naye Balaka akaenda zake.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36