bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Numbers 8
Numbers 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 9 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Sema na Haroni na kuwambia: Utakapoziweka taa juu ya kinara, uangalie, hizi taa zote saba ziangaze mahali pale palipo mbele ya kinara.
3
Haroni akafnya hivyo; alipoziweka hizo taa, huangalia, ziangaze mahali palipo mbele ya kinara, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
4
Nacho kinara kilikuwa kimetengenezwa kwa kufua dhahabu; toka shina lake hata maua yake, yote pia ilikuwa kazi ya kufuafua dhahabu; kama ule mfano ulivyokuwa, Bwana aliomwonyesha Mose, ndivyo, walivyokitengeneza hicho kinara.
5
Bwana akamwambia Mose kwamba:
6
Wachukue Walawi na kuwatoa katikati ya wana wa Isiraeli, upate kuwatakasa.
7
Nawe uwafanyizie hivyo ukiwatakasa: wanyunyizie maji ya weuo, nao na wajinyoe kwa wembe miili yao yote mizima, kisha na wazifue nguo zao, wapate kutakata.
8
Kisha na wachukue dume la ng'ombe aliye kijana bado pamoja na kilaji chake cha tambiko, ndio unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta. Nawe uchukue dume jingine la ng'ombe aliye kijana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
9
Kisha wapeleke Walawi, wafike mbele ya Hema la Mkutano, ukiwakusanya nao wote walio wa mkutano wa wana wa Isiraeli.
10
Kisha watokeze Walawi usoni pa Bwana, wana wa Isiraeli wakiwabandikia Walawi mikono yao.
11
Naye Haroni na awapitishe Walawi mbele ya Bwana huku na huko, wawe kipaji cha tambiko, wana wa Isiraeli walichokitoa cha kupitishwa motoni mbele ya Bwana, wapate kuutumikia utumishi wa Bwana.
12
Kisha Walawi na waibandike mikono yao vichwani pao wale ng'ombe, kisha umtumie mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima, uwapatie Walawi upozi.
13
Kisha wasimamishe Walawi mbele ya Haroni na mabele ya wanawe na kuwapitishwa mbele ya Bwana huku na huko, wawe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
14
Ndivyo, utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katikati ya wana wa Isiraeli, Walawi wapate kuwa wangu.
15
Baadaye Walawi na waingie kulitumikia Hema la Mkutano. Hivyo ndivyo, utakavyowatakasa na kuwapitisha huku na huko mbele ya Bwana, wawe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
16
Kwani hawa ndio niliopewa, watolewe katikati ya wana wa Isiraeli kuwa makombozi ya watoto wote wa kiume watakaozaliwa wa kwanza na mama zao; mahali pao hao wana wote wa kwanza nimewachukua wao kwa wana wa Isiraeli kuwa wangu.
17
Kwani kila mwana wa kwanza kwao wana wa Isiraeli ni wangu, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga tangu siku ile, nilipowapiga wana wa kwanza wote katika nchi ya Misri; ndivyo, nilivyowatakasa, wawe wangu,
18
nikiwachukua Walawi kuwa makombozi ya wana wote wa kwanza kwao wana wa Isiraeli.
19
Nami hawa Walawi nikiwapa Haroni na wanawe, wawe kipaji chao kilichotolewa katikati yao wana wa Isiraeli, wautumikie utumishi wao wana wa Isiraeli wa Hemani mwa Mkutano na kuwapatia wana wa Isiraeli upozi, hao wana wa Isiraeli wasipatwe na pigo lo lote, wao wana wa Isiraeli wakilikaribia Hema la Mkutano.
20
Kwa hiyo Mose na Haroni nao wote waliokuwa wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakawafanyizia Walawi yote sawasawa, kama Bwana alivyomwagiza Mose kuwafanyizia Walawi; hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyowafanyizia.
21
Walawi walipokwisha kujieua na kuzifua nguo zao, Haroni akawapitisha huku na huko mbele ya Bwana, kisha Haroni akawapatia upozi kwa hivyo, alivyowatakasa.
22
Baadaye Walawi wakaingia kuutumikia utumishi wa Hemani mwa Mkutano machoni pa Haroni napo machoni pa wanawe; kama Bwana alivyomwagiza Mose kuwafanyizia Walawi, ndivyo, walivyowafanyizia.
23
Bwana akamwambia Mose kwamba:
24
Hii ndiyo inayowapasa Walawi: tangu hapo, mtu alipopata miaka 25 na zaidi na aingie zamu ya utumishi wa Hemani mwa Mkutano.
25
Lakini tangu hapo, mtu anapopata miaka 50 na atoke katika zamu ya utumishi huo, asiutumikie tena.
26
Wataweza kuwasaidia ndugu zao mle Hemani mwa Mkutano na kulinda ulinzi, lakini kazi za utumishi wasizifanye. Hivyo ndivyo, utakavyowafanyizia Walawi, waziangalie kazi zao.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36