bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 10
Ezekiel 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 11 →
1
Nilipotazama penye ukingo uliokuwa juu ya vichwa vyao Makerubi nikaona kilichokuwa kama kito cha Safiro, kikafanana sura yake kuwa kama kiti cha kifalme, kikaonekana kuwa juu yao.
2
Akamwambia yule mtu aliyevaa vazi la ukonge, akasema: Ingia katikati ya magurudumu yaliyo chini ya Makerubi, uvijaze viganja vyako makaa ya moto yaliyoko katikati ya Makerubi, kisha yamwagie mji huu! Ndipo, alipopaingia machoni pangu.
3
Makerubi yalikuwa yamesimama kuumeni penye hiyo Nyumba, yule mtu alipoingia, nalo lile wingu lilikuwa limeujaza ua wa ndani.
4
Utukufu wa Bwana ukaondoka kwa Makerubi kwenda penye kizingiti cha kuiingilia hiyo Nyumba, hiyo Nyumba ikajazwa na lile wingu, ua nao ukajaa ung'avu wa utukufu wa Bwana.
5
Uvumi wa mabawa ya Makerubi ukasikilika mpaka kwenye ua wa nje, ukawa kama sauti ya Mwenyezi Mungu, akisema.
6
Ikawa, alipomwagiza yule mtu aliyevaa vazi la ukonge kwamba: Chukua moto penye magurudumu katikati ya Makerubi, naye alipoingia na kusimama kando ya gurudumu,
7
ndipo, Kerubi alipokunjua mkono wake kwenye Makerubi na kuupeleka penye moto uliokuwa katikati ya Makerubi, akautwaa, akampa mwenye vazi la ukonge na kuutia katika viganja vyake, naye akauchukua, akatoka.
8
Kisha kukaoneka kwa Makerubi chini ya mabawa yao mfano wa mkono wa mtu.
9
Nilipotazama mara nikaona magurudumu manne kando ya Makerubi, gurudumu moja kando ya Kerubi mmoja, vivyo hivyo gurudumu moja kando ya kila Kerubi mmoja; nilipoyatazama hayo nagurudumu, jinsi yalivyokuwa, yalikuwa kama kito cha Tarsisi.
10
Yote manne mfano wao ulionekana kuwa mmoja, ulikuwa kama gurudumu moja lililomo ndani ya gurudumu lenziwe.
11
Yalipokwenda yalikwenda pande zote nne pasipo kugeuka katika mwendo wao, kwani mahali hapo, kichwa kilipoelekea, ndipo, walipopafuata pasipo kugeuka katika mwendo wao.
12
Nayo miili yao na migongo yao na mikono yao na mabawa yao, nayo magurudumu yalikuwa yamejaa macho po pote, penye magurudumu yote manne vilikuwa hivyo.
13
Hayo magurudumu yakaitwa masikioni pangu Kimbunga.
14
Kila Kerubi mmoja alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa wa Kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mtu, wa tatu ulikuwa wa simba, wa nne ulikuwa wa tai.
15
Kisha Makerubi wakaenda juu. Hawa ndio nyama, niliyemwona kwenye mto wa Kebari.
16
Makerubi walipokwenda, magurudumu yakaenda kando yao; tena Makerubi walipoyakunjua mabawa yao, waondoke katika nchi kwenda juu, magurudumu nayo hayakugeuka kuondoka kando yao.
17
Waliposimama, nayo yakasimama; walipoinuka kwenda juu, nayo yakajiinua kwenda juu pamoja nao, kwani roho ya huyo nyama ilikuwa namo katika hayo magurudumu.
18
Kisha utukufu wa Bwana ukatoka kwenye kizingiti cha kuiingilia hiyo Nyumba, ukasimama juu ya Makerubi.
19
Makerubi wakayakunjua mabawa yao, wakaondoka katika nchi kwenda juu machoni pangu; ndivyo, walivyotoka hapo, hayo magurudumu hayo yakawa kandokando yao; wakasimama tena kwenye lango la Nyumba ya Bwana lielekealo maawioni kwa jua, nao utukufu wa Mungu wa Isiraeli ulikuwa juu yao.
20
Huyo ndiye nyama, niliyemwona chini yake Mungu wa Isiraeli kwenye mto wa Kebari, nikajua, ya kuwa hao ndio Makerubi.
21
Kila mmoja wao alikuwa na nyuso nne, tena kila mmoja alikuwa na mabawa manne, tena iliyofanana na mikono ya watu ilikuwa chini ya mabawa yao.
22
Nazo nyuso zao hao zilikuwa zimefanana na zile nyuso, nilizoziona kwenye mto wa Kebari; ndivyo, zilivyoonekana kuwa, nao wenyewe walikuwa hivyo. Kila mmoja wakaenda na kufuata hapo, uso wake ulipoelekea.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48