bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 24
Ezekiel 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 25 →
1
Neno la Bwana likanijia katika mwaka wa 9 katika mwezi wa kumi siku yake ya kumi kwamba:
2
Mwana wa mtu, jiandikie jina lake siku hii siku hiihii ya leo! Kwani mfalme wa Babeli ameufikia Yerusalemu siku hii ya leo.
3
Nao mlango huu mkatavu uutungie fumbo ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Iteleke nyungu! Ndiyo, iteleke! Kisha itie nayo maji!
4
Tena vikusanye vipande vyake vya kutia ndani, vyote viwe vipande vizuri tu vya paja na vya mkono, ijaze mifupa iliyochaguliwa!
5
Chukua kondoo tu waliochaguliwa kwa uzuri! Tena chini yake hiyo nyungu patupie mifupa, iwe chungu! Zitokose kabisa nyama, nayo mifupa iliyomo sharti ichemke sana.
6
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye damu, u nyungu yenye kutu, nayo kutu yake inakataa kuondoka kwake! Zitoe zile nyama kipande kwa kipande, msizipigie kura!
7
Kwani damu zilizomwagwa mwake zimo bado, ni hapohapo penye mwamba ulio wazi, alipozimiminia, hakuzimwaga penye mchanga, zikafunikwa kwa mavumbi.
8
Kusudi ziyainue makali yangu yenye moto ya kulipiza lipizi, kwa hiyo nimeacha, azimiminie hizo damu penye mwamba ulio wai, zisifunikwe.
9
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye damu, nami nitaupangia chungu kubwa la kuni.
10
Lete kuni nyingi, uwashe moto! Zitokose nyama kabisa na kuziunga kwa viungo! Mifupa na iungue!
11
Nyungu ikiwa tupu, iweke penye makaa yake ya moto, chuma chake kipate moto kabisa, mpaka kiungue, taka zake zilizomo ziyeyuke, kutu nayo iondoke kabisa.
12
Lakini ni kujisumbua bure, kutu haitoki kwake kwa kuwa kutu ni nyingi, namo motoni hiyo kutu yake inakaa.
13
Ni kwa ajili ya uchafu wako wa uzinzi; kwa kuwa nilitaka kukutakasa, ukakataa kutakata uchafu wako ukikutoka, kwa hiyo hutatakata tena, mpaka niyatimize kwako makali yangu yenye moto.
14
Mimi Bwana nimeyasema, kwa hiyo yatakuja nitakayoyafanya. Sitachoka, wala sitakuonea uchungu, nikuhurumie; kwa hivyo, njia zako zilivyo, tena kwa hivyo, nayo matendo yako yalivyo, watakuhukumu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
15
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
16
Mwana wa mtu, tazama, ayapendezaye macho yako nitamchukua kwako kwa mara moja nikimpiga; nawe usimwombolezee, wala usimlilie, machozi yasikutoke machoni!
17
Piga kite usiposikiwa; lakini aliyekufa usimfanyizie matanga! jifunge kilemba chako, kavae viatu miguuni pako! Lakini usiufunike udevu wa midomoni, wala usile chakula, watu watakachokuletea!
18
Asubuhi nilikuwa nikisema na watu, tena jioni mke wangu akafa, kesho yake asubuhi nikafanya nilivyoagizwa.
19
Watu wakaniuliza: Mbona hutuelezi yatakayokuwa kwetu, wewe ukifanya hivyo?
20
Nikawaambia: Neno la Bwana limenijia la kwamba:
21
Uambie mlango wa Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikipapatia uchafu Patakatifu pangu palipo majivuno yenu makuu na tamaa ya macho yenu na upendeleo wa roho zenu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike, mliowaacha, wataangushwa kwa panga.
22
Ndipo, mtakapofanya, mimi nilivyofanya: Hamtazifunika ndevu za midomoni, wala hamtakula chakula, mtakacholetewa na watu.
23
Navyo vilemba vyenu vitakuwa vichwani penu, navyo viatu miguuni penu; hamtaomboleza, wala hamtalia machozi, ila kwa manza zetu, mlizozikora, mtayeyuka, tena mtapigiana kite kila mtu na ndugu yake.
24
Naye Ezekieli atawawia kielekezo, nanyi myafanye yote, aliyoyafanya yeye, yatakapotimia. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
25
Nawe mwana wa mtu, isiwe hivyo? Siku, nitakapoyachukua kwao yaliyowapa nguvu, yaliyokuwa furaha yao kwa kuwapa utukufu, macho yaliyoyatamani, yaliyowashika mioyo yao wana wao wa kiume na wa kike,
26
siku ile atakuja kwako mtu aliyekimbia, ayasimulie masikioni pako.
27
Siku ile kinywa chako kitafumbuliwa papo hapo, yule mtoro atakapofika kwako, useme, usinyamaze tena; ndipo, utakapowawia kielekezo, nao watajua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48