bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 40
Ezekiel 40
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 41 →
1
Ikawa katika mwaka wa 25 wa kuhamishwa kwetu, mwaka ulipoanza, siku ya kumi ya mwezi, nao ulikuwa mwaka wa 14 wa kutekwa kwa huo mji, siku ileile ndipo, mkono wa Bwana uliponishika, ukanipeleka huko.
2
Katika maono ya Kimungu akanipeleka katika nchi ya Waisiraeli, akaniweka katika mlima mrefu sana, nitulie huko; upande wake wa kusini kulikuwako yaliyofanana na majengo ya mji.
3
Alipokwisha kunipeleka huko, mara nikaona mtu, akaonekana kuwa kama wa shaba, mkononi mwake alishika kamba ya katani na mwanzi wa kupimia, naye alikuwa amesimama langoni.
4
Akaniambia yule mtu: Mwana wa mtu, tazama kwa macho yako, tena sikiliza kwa masikio yako! Nao moyo wako uuelekeze kuyaangalia yote, nitakayokuonyesha! Kwani umeletwa huku, kusudi uonyeshwe mambo; yote, utakayoyaona huku, uwatangazie walio ukoo wa Isiraeli!
5
Nikaona ukuta wa nje ulioizunguka Nyumba pande zote pia. Nao mwanzi wa kupimia ulikuwa mkononi mwake yule mtu, ulikuwa wa mikono sita kama mkono wa mtu na upana wa shubiri moja; akaupima upana wa ukuta, ulikuwa mwanzi mmoja, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mwanzi mmoja.
6
Kisha akaenda kwenye jengo la lango lililoelekea maawioni kwa jua, akavipanda vipago vyake, akakipima kizingiti cha jengo la lango, upana wake ulikuwa mwanzi mmoja; kizingiti hiki kimoja kilikuwa kwa upana mwanzi mmoja.
7
Nacho chumba kimoja urefu wake ulikuwa mwanzi mmoja nao upana wake vilevile mwanzi mmoja, tena katikati ya vyumba kulikuwa mikono mitano. Kizingiti cha jengo la lango lililokuwa penye ukumbi, lililoelekea nyumbani, kilikuwa nacho mwanzi mmoja.
8
Akaupima ukumbi wa lile jengo la lango wa upande wa nyumbani, nao ulikuwa mwanzi mmoja.
9
Akaupima nao ukumbi wa lile jengo la lango wa upande wa mbele, nao ulikuwa mikono minane, nayo miimo yake ilikuwa mikono miwili, nao lukumbi huo ulikuwa upande wa nyumbani.
10
Navyo vyumba vya jengo la lango hili lililoelekea maawioni kwa jua vilikuwa vitatu upande wa huku, tena vitatu upande wa huko, kipimo cha hivi vitatu kilikuwa hicho kimoja, hata kipimo cha miimo ya huku na ya huko kilikuwa hicho kimoja.
11
Akaupima upana wa hapo pa kuingia, langoni nao ulikuwa mikono kumi, urefu wa lile lango ulikuwa mikono kumi na mitatu.
12
Mbele ya vile vyumba palikuwa pamekatwa mipaka, urefu wao wa juu upande wa huku mkono mmoja, nao upande wa huko vilevile mkono mmoja; kila chumba kilikuwa mikono sita upande wa huku na mikono sita upande wa huko.
13
Kisha akalipima jengo la lango toka dari la chumba hata dari la lchumba cha ng'ambo mikono ishirini na mitano, mlango ukiuelekea mlango wenziwe.
14
Akafanya nguzo za mikono sitini; penye hizo nguzo ua ulilizunguka jengo la lango pande zote.
15
Toka hapo pa kuingia langoni mpaka upande wa mbele wa ukumbi wa lango la ndani ilikuwa mikono hamsini.
16
Madirisha yenye vyuma yalikuwa kwenye vyumba na kwenye miimo upande wa ndani wa hilo jengo la lango po pote; nao ukumbi ulikuwa na madirisha po pote yaliyoelekea ndani. Penye nguzo palikuwa pamechorwa mitende.
17
Kisha akanipeleka katika ua wa nje, nikaona huko vyumba, tena chini palikuwa pametengenezwa sakafu kuzunguka pande zote uani; hapo penye sakafu palikuwa na vile vyumba, navyo vilikuwa thelathini.
18
Hiyo sakafu ilikuwa kando penye malango, ikalingana na urefu wa majengo ya malango, ndiyo sakafu ya ua wa chini.
19
Akaupima upana toka upande wa ndani wa jengo la lango la ua wa chini mpaka upande wa mbele wa jengo la lango la ua wa ndani mikono mia; vilikuwa hivyo upande wa maawioni kwa jua na upande wa kaskazini.
20
Nalo jengo la lango la ua wa nje lililoelekea kaskazini akalipima urefu wake na upana wake.
21
Vyumba vyake vilikuwa vitatu upande wa huku, tena vitatu upande wa huko; nazo nguzo zake na ukumbi wake kipimo chao kilikuwa kilekile cha jengo la mlango la kwanza. Urefu wake ulikuwa mikono hamsini, nao upana wake ulikuwa mikono ishirini na mitano.
22
Madirisha yake na ukumbi wake na machoro ya mitende kipimo chao kilikuwa kilekile cha jengo la lango lililoelekea maawioni kwa jua; kwa vipago saba watu wakalipandia, kisha ukumbi wake ulikuwa mbele yao.
23
Tena kulikuwako jengo la lango la ua wa ndani lililoelekea sawasawa jengo la lango la upande wa kaskazini na jengo la lango la upande wa maawioni kwa jua, akapima toka lango hata lango mikono mia.
24
Akaniongoza njia ya kwenda kusini, nikaona, hata katika hiyo njia ya kwenda kusini kulikuwako jengo la lango, akazipima nguzo zake na ukumbi wake, kipimo chao kilikuwa kilekile.
25
Hata madirisha yalilizunguka hilo jengo la lango na ukumbi wake pande zote, kama yale madirisha mengine yalivyokuwa, nao urefu ulikuwa mikono hamsini, nao upana ulikuwa mikono ishirini na mitano.
26
Napo hapo palikuwa na vipago saba vya kupapandia, nao ukumbi wake ulikuwa mbele yao, nao ulikuwa na machoro ya mitende kwenye nguzo zake upande wa huku na upande wa huko.
27
Tena kulikuwako hata jengo la lango la ua wa ndani katika hiyo njia ya kwenda kusini, akapima toka lango hata lango katika hiyo njia ya kwenda kusini mikono mia.
28
Akanipeleka katika ua wa ndani kwenye njia ya kwenda kusini, akalipima hilo jengo la lango la kusini, vipimo vyake vilikuwa vile vile,
29
Navyo vyumba vyake na nguzo zake na ukumbi wake vipimo vyao vilikuwa vilevile. Hata madirisha yalilizunguka hilo jengo la lango na ukumbi wake pande zote; nao urefu ulikuwa mikono hamsini, nao upana ulikuwa mikono ishirini na mitano.
30
Pande zote palikuwa na vyumba, urefu ulikuwa mikono ishirini na mitano, nao upana ulikuwa mikono mitano.
31
Ukumbi wake uliuelekea ua wa nje, nayo machoro ya mitende yalikuwa penye nguzo zake, tena hapo palikuwa na vipago vinane vya kupapandia.
32
Kisha akanipeleka katika ua wa ndani penye njia ya maawioni kwa jua, akalipima jengo la lango vipimo vyake vilikuwa vilevile.
33
Navyo vyumba vyake na nguzo zake na ukumbi wake vilikuwa vilevile. Hata madirisha yalilizunguka hilo jengo la lango na ukumbi wake pande zote. Urefu ulikuwa mikono hamsini, nao upana ukikuwa mikono ishirini na mitano.
34
Ukumbi wake uliuelekea ua wa nje, nayo machoro ya mitende yalikuwa penye nguzo zake upande wa huku na upande wa huko, napo hapo palikuwa na vipago vinane vya kupapandia.
35
Kisha akanipeleka penye jengo la lango la kaskazini, akalipima, vipimo vyake vilikuwa vilevile.
36
Vyumba vyake na nguzo zake na ukumbi wake ni vivyo hivyo, nayo madirisha yalilizunguka pande zote; urefu ulikuwa mikono hamsini, nao upana ulikuwa mikono ishirini na mitano.
37
Ukumbi wake uliuelekea ua wa nje, nayo machoro ya mitende yalikuwa penye nguzo zake upande wa huku na wa huko, napo hapo palikuwa na vipago vinane vya kupapandia.
38
Hapo palikuwa na chumba, pake pa kuingilia palikuwa ukumbini mwa hayo malango, ndimo walimozisafishia nyama za kuteketezwa nzima za tambiko.
39
Mle ukumbini mwa jengo la lango mlikuwa na meza mbili upande wa huku, tena meza mbili upande wa huko; ndipo, walipoziandalia ng'ombe za tambiko zilizochinjwa za kuteketezwa nzima nazo za weuo nazo za upozi.
40
Tena upande wa nje pa kupandia napo pa kuliingilia jengo la lango la kaskazini palikuwa na meza mbili, nao upande mwingine wa ukumbi wa hilo jengo la lango palikuwa na meza mbili tena.
41
Pamoja zilikuwa meza nne upande wa huku na meza nne upande wa huko kando ya hilo jengo la lango, zote pamoja zilikuwa meza nane; ndipo, walipoziandalia nyama zilizochinjwa.
42
Tena palikuwa na meza nne za nyama za tambiko zilizoteketezwa nzima, zilijengwa kwa mawe yaliyochongwa, urefu wao ulikuwa mkono mmoja na nusu nao upana ulikuwa mkono mmoja na nusu, nao urefu wa kwenda juu ulikuwa mkono mmoja; ndipo, walipoviweka vyombo vya kuchinjia nyama wa kuteketezwa nzima na nyama wengine wa tambiko.
43
Upande wao wa ndani palikuwa pametiwa mambo, urefu wao shibiri moja pande zote; hizo meza zilikuwa za kuwekea nyama, walizomtolea Mungu.
44
Upande wa nje wa kila jengo la lango la ndani palikuwa na vyumba vya waimbaji katika ua wa ndani, kimoja kando ya jengo la lango la kaskazini kilielekea kusini, kimoja kilikuwa kando yake jengo la lango la maawioni kwa jua, nacho kilielekea kaskazini.
45
Akaniambia: Hiki chumba kinachoelekea kusini ni cha watambikaji wanaongoja zamu humu Nyumbani.
46
Nacho chumba kinachoelekea kaskazini ni cha watambikaji wanaongoja zamu mezani pa kutambikia, ndio wana wa Sadoki, ndio wanaomkaribia Bwana peke yao katika wana wa Lawi, wamtumikie.
47
Akaupima huo ua ulikuwa wenye pembe nne, urefu wake ulikuwa mikono mia, nao upana wake ulikuwa mikono mia. Nayo meza ya kutambikia ilikuwa mbele ya Nyumba.
48
Akanipeleka penye ukumbi wa Nyumba, akaupima unene wa miimo ya huo ukumbi, ulikuwa mikono mitano upande wa huku, tena mikono mitano upande wa huko, nao upana wa lango ulikuwa mikono kumi na minne, nazo kuta za kando ya jengo la lango upande wa ndani zilikuwa mikono mitatu upande wa huku na mikono mitatu upande wa huko.
49
Urefu wa ukumbi ulikuwa mikono ishirini, nao upana wake mikono kumi na miwili, tena hapo palikuwa na vipago vya kupapandia, tena penye miimo palikuwa na nguzo, moja upande wa huku na moja upande wa huko.
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48