bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 30
Ezekiel 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 31 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, fumbua yatakayokuwa, ukisema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Pigeni vilio kwamba: Ni siku gani hii?
3
Kwani siku iko karibu, kweli siku ya Bwana iko karibu! ni siku yenye mawingu, itakuwa wakati wa wamizimu.
4
Panga zitaingia Misri, nayo nchi ya Nubi itatetemeka, watu waliopigwa kwa panga wakianguka huko Misri, wengine wakizichukua mali zao, tena wakiibomoa misingi yao.
5
Wanubi na Waputi na Waludi nao wote waliochanganyika nao na Wakubu na wenyeji wa nchi, waliofanya maagano nao, wote pia watauawa kwa panga.
6
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nao walioiegemea nchi ya Misri wataangushwa, majivuno ya nguvu zake yakinyenyekezwa; kuanzia Migidoli kufikisha Siwene watauawa kwao kwa panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
7
Nchi zao zitakuwa peke yao katikati ya nchi nyingine zilizo peke yao nazo, nayo miji yao itakuwa vivyo hivyo katikati ya miji iliyo mabomoko tu.
8
Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana; nitakapowasha moto katika Misri, nao wasaidiaji wake wote watavunjwa.
9
Siku ile watatoka kwangu wajumbe kwenda katika merikebu kuwastusha nao Wanubi wakaao na kutulia; ndipo, watakapotetemeka, ile siku ya Misri itakapokuja, kwani wataiona, inavyokuja.
10
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitawakomesha wale watu wengi wa Misri kwa mkono wa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli.
11
Yeye na watu wake, alio nao, ni wakali kuliko mataifa mengine; watapelekwa kuiangamiza hiyo nchi, watazichomoa panga zao kuwapiga Wamisri, waijaze hiyo nchi watu walioumizwa na panga.
12
Nayo majito yake nitayakausha, nayo nchi hiyo nitaiuza mikononi mwa watu wabaya, niiangamize kwa mikono ya wageni pamoja nayo yote yaliyomo. Mimi Bwana nimeyasema.
13
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitayapoteza magogo ya kutambikia mle Nofu, hata vinyago nitavikomesha, pasiwe tena mkuu atokaye katika nchi ya Misri, tena nitaitisha nchi ya Misri.
14
Patirosi nitaigeuza kuwa mapori tu, mle Soani nitawasha moto, namo No nitawahukumu waliomo.
15
Mji wa Sini ulio boma lake Misri nitaumwagia makali yangu yenye moto, nao watu wengi waliomo No nitawaangamiza.
16
Nitawasha moto katika Misri: Sini utaona machungu makuu, No utavunjwa kwa kubomolewa, Nofu utapata wanaousonga mchana.
17
Vijana wa Oni na wa Pi-Beseti watauawa kwa panga, watu wao wengine watatekwa na kuhamishwa.
18
Namo Tehafunesi mchana utageuka kuwa giza, nitakapozivunja mle bakora za kifalme za Misri; namo ndimo, nitakamoyakomesha majivuno ya nguvu zao; mji wenyewe wingu litaufunika, navyo vijiji vyake vya shambani vitatekwa na kuhamishwa.
19
Hivyo ndivyo, nitakavyokata mashauri huko Misri; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
20
Ikawa katika mwaka wa 11 siku ya saba ya mwezi wa kwanza, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
21
Mwana wa mtu, mkono wa Farao, mfalme wa Misri, nimeuvunja, lakini tazama, haukufungwa, upate kupona, hawakuutakia kitambaa tu, kwamba waufunge, wautie nguvu tena, upate kushika upanga.
22
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikimjia Farao, mfalme wa Misri, nitaivunja mikono yake, ule ulio na nguvu bado nao ule uliokwisha kuvunjika, niuangushe upanga chini uliomo mkononi mwake.
23
Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika hizo nchi.
24
Lakini mikono ya mfalme wa Babeli nitaitia nguvu, nao upanga wangu nitampa mkononi mwake, niivunje mikono ya Farao, ampigie yeye kite kama mtu mwenye vidonda.
25
Mikono ya mfalme wa Babeli nitaitia nguvu, lakini mikono ya Farao itaanguka; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapompa mfalme wa Babeli upanga wangu mkononi mwake, aichomolee nchi ya Misri.
26
Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika hizo nchi. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48