bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 42
Ezekiel 42
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 43 →
1
Kisha akanipeleka katika ua wa nje penye njia ya kwenda kaskazini, akanipeleka penye vyumba vilivyopaelekea hapo palipokatazwa watu, tena vililielekea jengo lililoko upande wa kaskazini.
2
Upande wa mbele urefu wake ulikuwa mikono mia hapo pa kuingia upande wa kaskazini, nao upana wake ulikuwa mikono hamsini.
3
Kuielekea ile mikono ishirini ya ua wa ndani, tena kuielekea sakafu ya mawe ya ua wa nje palikuwa na baraza juu ya baraza penye madari matatu.
4
Mbele ya hivyo vyumba palikuwa pa kupitia palipouelekea ua wa ndani; upana wake ulikuwa mikono kumi, nao urefu wake hiyo njia ulikuwa mikono mia moja, nayo milango ya zile baraza ilielekea kaskazini.
5
Navyo vyumba vya juu vilikuwa vimekatwa kidogo kwa upana wao, kwani zilipunguzwa na zile baraza zilizopita mbele yao, vilikuwa vifupi kuliko vile vya chini na vya kati vya hilo jengo.
6
Kwani vilikuwa vya madari matatu, nayo yalikuwa hayana nguzo kama nguzo za uani; kwa hiyo lvya juu vilipunguzwa upana toka chini kuliko vya chini na vya katikati.
7
Tena palikuwa na kitalu nje kilichokwenda sawasawa na vile vyumba upande wa ua wa nje mbele ya vyumba, urefu wake ulikuwa mikono hamsini.
8
Kwani urefu wa vyumba vilivyokuwa upande wa ua wa nje ulikuwa mikono hamsini, lakini vile vilivyokuwa upande wa Patakatifu urefu wao ulikuwa mikono mia.
9
Chini yao hivyo vyumba palikuwa pa kuingia upande wa maawioni kwa jua, mtu akitoka katika ua wa nje.
10
Sawasawa na hicho kitalu kilichokuwa hapo uani, lakini upande wa kusini, palikuwa na vyumba vilivyopaelekea hapo palipokatazwa watu na hapo penye jengo lile.
11
Mbele yao palikuwa pa kupitia; ukipatazama, palikuwa na vyumba kama vile vya upande wa kaskazini, urefu wao na upana wao ni uleule, nazo njia zao zote za kutoka na mambo mengine yalikuwa yaleyale. Nayo milango yao
12
ilikuwa kama milango ya vyumba vilivyoelekea kusini; pa kuingia palikuwa pembeni pa njia iliyokwenda mbele ya kitalu kilichokuwa sawa kama kile cha upande wa kaskazini, mtu akiishika ile njia ya upande wa maawioni kwa jua, afike hapo.
13
Kisha akaniambia: Vyumba vya upande wa kaskazini, hata vyumba vya upande wa kusini vilivyopaelekea palipokatazwa watu, ndivyo vyumba vitakatifu; ndimo, watambikaji watakamokula vyakula vitakatifu vyenyewe, tena ndimo, watakamoviweka vipaji vitakatifu vyenyewe, vilaji vya tambiko na nyama za ng'ombe za tambiko za weuo nazo zao za upozi, kwani ndivyo vyumba vitakatifu.
14
Watambikaji wakitaka kuingia humo, wasitoke Patakatifu na kupitia penye ua wa nje! Humo ndimo, wayaweke mavazi yao waliyoyavaa wakimtumikia Mungu, kwani nayo ni matakatifu. Sharti wavae mavazi mengine, kisha wapakaribie, watu walipo!
15
Alipokwisha kuipima Nyumba upande wa ndani, akanitoa humo na kunipeleka nje penye jengo la lango lililoelekea maawioni kwa jua, akaipima pande zote kuizunguka.
16
Akaupima upande wa maawioni kwa jua kwa ule mwanzi wa kupimia, nao ulikuwa wote pia mianzi mia tano kwa kupima na ule mwanzi.
17
Akaupima upande wa kaskazini, nao ulikuwa wote pia mianzi mia tano kwa kupima na ule mwanzi.
18
Akaupima upande wa kusini, nao ulikuwa mianzi mia tano kwa kupima na ule mwanzi.
19
Akazunguka penye upande wa baharini, akaupima, nao ulikuwa mianzi mia tano kwa kupima na ule mwanzi.
20
Alipopapima pande zote nne penye ukuta uliopazunguka, urefu wake ulikuwa po pote mia tano, nao upana wake ulikuwa mia tano kupatenga Patakatifu napo penye watu.
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 43 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48