bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 27
Ezekiel 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 28 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Wewe mwana wa mtu, utungie mji wa Tiro ombolezo!
3
Uambie Tiro: Wewe ulikaa paingiapo bahari, ukachuuza katika nchi nyingi za baharini; hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe Tiro ulisema: Mimi nimetimiza uzuri wote.
4
Kweli mipaka yako imo baharini ndani, nao waliokujenga walikutengeneza kuwa chombo chenye uzuri wote.
5
Walikujenga pande zote mbili kwa mbao za mivinje ya Seniri, wakachukua mwangati huko Libanoni wa kukutengenezea mlingoti.
6
Mivule ya Basani waliitumia ya kukufanyizia makasia, vyumba vyako walivifanya kwa mbao za misagawi zilizopangiliwa kwa meno ya tembo, zilizotoka visiwani kwa Wakiti.
7
Nguo za rangi zilizotoka Misri zilikuwa tanga lako zikawa hata bendera yako. Nguo za kifalme nyeusi na nyekundu zilizotokavisiwa vya Elisa zilikuwa chandalua chako cha kujifunika juu.
8
Waliokaa Sidoni na Arwadi walikuwa mabaharia wako, nao werevu wa kweli wa kwako, Tiro, ndio waliokuwa waelekeza chombo.
9
Wazee wa Gebali na mafundi wake walikuwa kwako wa kuziziba nyufa zako. Merikebu zote za baharini zikafika kwako na mabaharia wao, wakauziana na wewe.
10
Wapersia na Waludi na Waputi walikuwamo katika vikosi vyako vya askari wa kukupigia vita vyako; walipotundika ngao na kofia kwako waliuongea utukufu wako.
11
Wana wa Arwadi na askari wako walizunguka penye kuta zako za boma, tena Wagamadi walikuwa katika minara yako; walipozitundika ngao zao po pote katika kuta zako, waliutimiza uzuri wako.
12
Watarsisi wakaja kuchuuza kwako kwa ajili ya wingi wa vitu vya kwako, wakazinunua bidhaa zako kwa fedha na kwa vyuma na kwa bati na kwa risasi.
13
Wagriki na Watubali na Wameseki walikuwa wachuuzi wako, wakatoa watumwa na vyombo vya shaba, wapate vitu vya kwako.
14
Walio wa mlango wa Togarma walitoa farasi na farasi wa vita na nyumbu, wapate bidhaa zako.
15
Wana wa Dedani walikuwa wachuuzi wako, watu wa nchi nyingi za baharini wakaja kuchuuza mikononi mwako: walikuletea meno ya tembo na mipingo kuwa malipo yao.
16
Washami nao wakaja kuchuuza kwako kwa ajili ya wingi wa kazi zako, wakazinunua bidhaa zako kwa vito vyekundu na kwa nguo za kifalme na kwa nguo za rangi na kwa bafta nzuri na kwa marijani na kwa vijiwe vya yaspi.
17
Wayuda nao wa nchi ya Isiraeli walikuwa wachuuzi wako, wakanunua vitu vya kwako kwa ngano za Miniti na kwa vikate vitamu na kwa asali na kwa mafuta na kwa uvumba.
18
Wadamasko wakaja kuchuuza kwako kwa ajili ya wingi wa kazi zako na kwa ajili ya wingi wa mali, wakaleta mvinyo za Helboni na manyoya meupe sana ya kondoo.
19
Wawedani na Wayawani walijipatia bidhaa zako na kuleta toka Uzali vyuma vilivyofuliwa vema, hata dalasini na vichiri vilikuwa malipo yao ya kukulipa.
20
Wadedani walikuwa wachuuzi wako, wakanunua vyako kwa nguo nzuri za kuweka chini ya matandiko.
21
Waarabu na wakuu wote wa Kedari nao wakaja kuchuuza mikononi mwako, wakanunua kwako kwa wana kondoo na kwa madume ya kondoo na kwa mbuzi.
22
Wachuuzi wa Saba na wa Raama nao walikuwa wachuuzi wako, wakazinunua bidhaa zako kwa manukato mazuri mno kupita yote mengine na kwa vito vya namna zote vyenye kiasi kikubwa na kwa dhahabu.
23
Waharani na Wakane na Waedeni, nao wachuuzi wa Saba na Waasuri na Wakilmadi walikuwa wachuuzi wako.
24
Hao walifanya biashara na wewe wakiuza nguo za urembo kama mablanketi makubwa ya kifalme yenye rangi nzuri na mazulia yenye machorochoro yaliyofungwa vema kwa kamba katika sanduku za miangati, wakanunua vitu vilivyouzwa kwako.
25
Merikebu za Tarsisi zilikuwa kama wapangazi wako wa kupeleka vitu vya kwako, ukafurikiwa, ukatukuka sana huko ndani baharini.
26
Wavutao makasia wakikupeleka kwenye vilindi vya maji, lakini upepo utokao maawioni kwa jua utakuvunja baharini kati.
27
Ndipo, mali zako na bidhaa zako na vitu vya kwako na mabaharia wako na waelekeza chombo nao wazibao nyufa zako nao wachuuzi waliovichuuzia vya kwako nao wote, ulio nao wa kukupigia vita vyako, pamoja na mkutano wote wa watu wako waliomo mwako watakapoanguka kule baharini kati; itakuwa siku ile, utakapoangamizwa.
28
Kwa sauti za makelele ya waelekeza vyombo vyako vitatetemeka viunga vyako.
29
Ndipo, wote wavutao makasia watakaposhuka na kutoka merikebuni mwao mabaharia nao wote waelekezao vyombo baharini wasimame pwani,
30
wakupalizie sauti zao na kukulilia kwa uchungu; watajitupia mavumbi vichwani pao na kujigaagaza majivuni.
31
Watajikata nywele kwa ajili yako, vichwa viwe vyenye vipara, kisha watajifunga magunia, wakulilie kwa uchungu wa roho zao na kukuombolezea kwa kuliwa na uchungu.
32
Watakapokulilia watakutungia ombolezo, wakuombolezee kwamba: Pako mahali gani panaponyamaza kimya kama Tiro ulioko baharini kati?
33
Bidhaa zako zilipotoka baharini ulishibisha makabila mengi ya watu, kwa wingi wa mali zako na wa vitu vya kwako uliwapatia wafalme wa nchi mali nyingi.
34
Lakini sasa umevunjwa, utoweke baharini kwa kutoswa vilindini penye maji mengi, navyo vitu vya kwako vya kuuza nao mkutano wa watu wako waliokuwamo mwako wamezama.
35
Kwa hiyo wote wakaao kwenye bahari wanakustukia wafalme wao wakapigwa na bumbuazi, nazo nyuso zao zikatetemeka.
36
Wachuuzi walioko kwenye makabila ya watu hukuzomea, kwa kuwa umegunduliwa na maangamizo, wala hutakuwapo tena kale na kale.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48