bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 31
Ezekiel 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 32 →
1
Ikawa katika mwaka wa 11 siku ya kwanza ya mwezi wa tatu, ndipo neno la Bwana liliponijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, mwambie Farao, mfalme wa Misri, nao watu wake walio wengi: kwa ukuu wako unafanana na nani?
3
Tazama, Mwasuri alikuwa mwangati wa Libanoni ulio mzuri kwa matawi yake yaliyo yenye majani mengi yenye kivuli, tena ni mrefu kwa kimo chake, kilele chake huyapita majani mengine ya miti iliyoko.
4
Maji ndiyo yaliyoukuza hivyo, vilindi vya chini ndivyo vilivyouendesha juu, mito yao ikapitia po pote ulipopandwa, kisha vikavipeleka vijitojito vyao penye miti yote ya shambani.
5
Kwa hiyo ulikua kuwa mrefu kwa kimo chake kuliko miti yote ya kondeni, matawi yake yakawa mengi, nayo machipuko yake yakawa marefu, ukiweza kuyachipuza vema kwa hayo maji mengi.
6
Ndege wote wa angani walijenga matundu yao katika matawi yake, hapo chini ya machipuko yake wakazaa nyama wo wote wa porini, napo kivulini pake wakakaa mataifa mengi na mengi.
7
Hivyo ulikuwa mzuri kwa ukubwa wake na kwa urefu wa matawi yake, kwani mizizi yake iko kwenye maji mengi.
8
Katika bustani ya Mungu haukuwako mwangati ulioupita, wala mivinje haikufanana nao kwa matawi yao, wala migude haikuwa yenye machipuko kama huo; miti yote iliyoko bustanini kwake Mungu haikufanana nao kwa uzuri wake.
9
Niliutengeneza kuwa mzuri kwa wingi wa matawi yake, kwa hiyo miti iliyoko Edeni bustanini kwake Mungu iliuonea wivu.
10
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Kwa kuwa ulikuwa mrefu kwa kimo chake, kilele chake kikayapita majani ya miti iliyoko, ukajiwazia moyoni mwake kuwa mkuu kwa urefu wake.
11
Lakini nitamtia mikononi mwake aliye peke yake mkuu wa mataifa, aufanyizie ayatakayo; kwa uovu wake nimekwisha kuutupa.
12
Ndipo, wageni walio wakali kuliko mataifa mengine walipoukata, wakaubwaga, matawi yake yaanguke milimani na mabondeni po pote, nayo machipuko yake yakavunjika, yakawa katika makorongo yote ya nchi, nayo makabila yote ya nchi yakaondoka kivulini pake, wakauacha tu.
13
Juu ya gogo lake lililoanguka watakaa ndege wote wa angani, nako kwenye machipuko yake watakuwako nyama wote wa porini.
14
Itakuwa hivyo, kusudi miti yote iliyoko kwenye maji isijikuze, wala isipeleke vilele vyao juu kabisa kupita miti mingine yenye majani mengi, wala ile yenye nguvu isisimame kwa urefu wao na kuishinda yote mingine inyweshwayo, kwani yote imewekewa kufa, ifike mahali palipo chini ya nchi kwenye watu walioshuka shimoni.
15
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Siku ile, uliposhuka kuzimuni, naliviombolezesha vilindi vya maji vilivyoko ndani ya nchi nikivifunika kwa ajili yake huo, tena nikiizuia mito yao, yale maji mengi yakomeshwe, nayo milima ya Libanoni naliivika mavazi ya matanga, nayo miti yote ya kondeni ikazimia.
16
Kwa uvumi wa kuanguka kwake nikayatetemesha mataifa, nilipoushusha kuzimuni pamoja nao washukao shimoni; ndipo, miti yote ya Edeni ilipotulizana pale mahali palipo chini ya nchi, ni ile miti ya Libanoni iliyochaguliwa kwa uzuri, ile yote iliyonyweshwa maji.
17
Hii nayo ilishuka pamoja nao kuzimuni kwao waliouawa kwa panga, ndio waliokuwa mkono wake walipokaa kivulini pake katikati ya mataifa.
18
Kwa hiyo umefanana na nani kwa utukufu na kwa ukuu kwenye miti ya Edeni? Pamoja na miti hii ya Edeni nawe utashushwa pale mahali palipo chini ya nchi, ulale kwao wasiotahiriwa pamoja nao waliouawa kwa panga. Huo ndio Farao na watu wake wote walio wengi. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48