bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 43
Ezekiel 43
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 44 →
1
Akaniongoza tena kwenda penye lile lango lililoielekea njia ya maawioni kwa jua.
2
Nilipotazama mara nikaona, utukufu wa Mungu wa Isiraeli ukija katika njia itokayo maawioni kwa jua, nao uvumi wake ulikuwa kama uvumi wa maji mengi, nayo nchi iliangaza kwa utukufu wake.
3
Ulionekana kuwa kama lile ono, nililoliona, ulikuwa kweli kama lile ono, nililoliona nilipokuja kuuangamiza huo mji; tena ulionekana kuwa kama lile ono, nililoliona huko kwenye mto wa Kebari, nikaanguka kifudifudi.
4
Nao utukufu wa Bwana ukaja kuingia humo Nyumbani katika njia ya lango lililoielekea hiyo njia ya maawioni kwa jua.
5
Ndipo, roho iliponichukua, ikanipeleka katika ua wa ndani, mara nikaona, utukufu wa Bwana ulivyoijaza Nyumba.
6
Nikasikia aliyesema na mimi toka mle Nyumbani, tena kulikuwako mtu aliyesimama hapo, nilipokuwa.
7
Akaniambia: Mwana wa mtu, hapa ndipo penye kiti changu cha kifalme napo penye nyayo za miguu yangu; ndipo, nitakapokaa kale na kale katikati ya wana wa Isiraeli. Walio wa mlango wa Isiraeli hawatalipatia tena Jina langu takatifu uchafu, wala wenyewe, wala wafalme wao, wala kwa ugoni wao, wala kwa mizoga ya wafalme wao watakapokufa,
8
wakiviweka vizingiti vyao penye kizingiti changu nayo miimo yao kandokando penye miimo yangu, pakawa ukuta tu uliopatenga pangu na pao, wakalipatia Jina langu takatifu uchafu kwa machukizo yao, waliyoyafanya; ndipo, nilipowamaliza kwa makali yangu.
9
Sasa ugoni wao watauondoa pangu pamoja na mizoga ya wafalme wao, nipate kukaa katikati yao kale na kale.
10
Wewe mwana wa mtu, walio mlango wa Isiraeli uwapashe habari za Nyumba hii, wapatwe na soni, wayaache maovu yao, waliyoyafanya, kisha waupime vema ulinganifu wake.
11
Nao watakapopatwa na soni, wayaache yale yote, waliyoyafanya, ndipo, utakapowajulisha umbo lake Nyumba hii, ilivyolinganywa, napo pa kuitokea napo pa kuiingilia, jinsi umbo lake lote pia lilivyo! Tena uwajulishe maongozi yalipasayo umbo lake lote na maonyo yake yote ukiyaandika machoni pao, waliangalie umbo lake lote na maongozi yote yalipasayo, wayafanye!
12
Haya ndiyo maonyo yaipasayo hii Nyumba: Po pote penye mipaka yake izungukayo huku milimani juu ndipo Patakatifu penyewe. Yaangalieni haya maonyo yaipasayo Nyumba hii!
13
Hivi ndivyo vipimo vyake pa kumtambikia Bwana vya kupapima kwa mikono, mkono ukiwa mkono wa mtu na upana wa shibiri: msingi ni mkono mmoja, nao upana wake ni mkono mmoja, tena pembeni pake panazunguka kitalu, urefu wake ni shibiri moja. Nao huu ndio urefu wa juu wa hapo pa kutambikia:
14
toka msingi ulioko mchangani mpaka daraja ya chini ni mikono miwili, nao upana wake mkono mmoja; tena toka daraja hili dogo mpaka daraja kubwa ni mikono minne, nao upana wake mkono mmoja.
15
Kisha kilima cha Mungu ni mikono minne, tena hapo jikoni pa Mungu palikuwa na pembe nne zilizoelekea juu.
16
Nalo jiko la Mungu ni mikono kumi na miwili urefu wake, nao upana wake ni mikono kumi na miwili, pande zake nne ni sawa, zenye pembe nne.
17
Lile daraja kubwa urefu wake ni mikono kumi na minne, nao upana wake ni mikono kumi na minne, pande zake nne ni sawa; nacho kitalu kinacholizunguka ni nusu ya mkono, nao msingi wake po pote ni mkono mmoja; navyo vipago vya kupapandia viko upande wa maawioni kwa jua.
18
Kisha akaniambia: Mwana wa mtu, hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu: Haya ndiyo, ninayokuagiza kuyafanya siku ile, hapo pa kunitambikia patakapokwisha kutengenezwa, watoe juu yake ng'ombe za tambiko pamoja na kupanyunyizia damu.
19
Ndipo, utakapotoa ndama ya ng'ombe ya kiume kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, uwape watambikaji wa Kilawi walio wa uzao wa Sadoki, maana ndio wanaonikaribia na kunitumikia; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
20
Kisha sharti uchote damu katika damu yake, uinyunyizie pembe zake nne napo penye zile pembe nne za daraja napo penye kitalu kipazungukacho! Ndivyo, utakavyopaeua pamoja na kupapatia upozi.
21
Kisha umchukue huyo ndama atakayekuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, umteketeze penye Nyumba hii hapo panapoitumikia kazi hii upande wa nje wa hapo Patakatifu.
22
Siku ya pili sharti upeleke dume la mbuzi asiye na kilema, wapaeue hapo pa kutambikia kama walivyopaeua na kumtoa yule ndama.
23
Utakapokwisha kupaeua, sharti upeleke ndama ya ng'ombe ya kiume asiye na kilema na dume la kondoo asiye na kilema.
24
Hao uwapeleke wa kuwatoa usoni pa Bwana, kisha watambikaji wawamwagie chumvi na kumtolea Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
25
Sharti ufanye hivyo siku saba, wakitoa kila siku dume la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ndama ya ng'ombe ya kiume na dume la kondoo; hao wote, watakaowatoa, sharti wawe nyama pasipo kilema.
26
Sharti siku saba wapapoze hapo pa kutambikia na kupaeua hivyo. Ndivyo, watakavyopatakasa, pawe patakatifu.
27
Watakapozimaliza hizo siku, basi, siku ya nane nazo siku zitakazokuwa zote watambikaji watolee hapo pa kutambikia ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima nazo za kushukuru; ndipo, nitakapopendezwa nanyi; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 44 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48