bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 37
Ezekiel 37
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 38 →
1
Mkono wa Bwana ukanishika, Bwana akanitoa kirohoroho, akanipeleka na kuniweka katikati ya hilo bonde, nalo lilikuwa limejaa mifupa.
2
Akanipitisha po pote pande zote, ilipokuwa, nikaiona kuwa mingi sana humo bondeni juu ya mchanga, nami nikaiona kuwa mikavu sana.
3
Akaniuliza: Mwana wa mtu, inakuwaje? Mifupa hii itaweza kuwa yenye uzima tena? Nikajibu: Bwana Mungu wewe unajua.
4
Akaniambia: Ifumbulie mifupa hii yatakayokuwa! Iambie: Ninyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana!
5
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyoiambia mifupa hii: Tazameni, nitawaletea pumzi ndani yenu, mpate kuwa wenye uzima tena.
6
Nitatia mishipa juu yenu, tena nitaotesha nyama juu yenu, nitawafunika kwa ngozi, kisha nitawatia pumzi; ndipo, mtakapokuwa watu wazima, mtajua, ya kuwa mimi ni Bwana.
7
Nikafumbua, kama nilivyoagizwa; ikawa, sauti ya kufumbua kwangu iliposikilika, pakawa na vishindoshindo, mifupa ikarudiana kila mfupa kwa mfupa mwenziwe.
8
Nilipotazama, nikaona kwao mishipa, nazo nyama zikaja kuwa juu yao, kisha ngozi zikazifunika pande za juu, lakini pumzi hazikuwamo mwao.
9
Akaniambia: Ufumbulie upepo! Fumbua, mwana wa mtu, ukiuambia upepo: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe upepo njoo na kutoka pande zote nne za upepo, uwapuzie hawa waliouawa, wapate kuwa wazima tena!
10
Nikafumbua, kama nilivyoagizwa; ndipo, pumzi zilipowaingia, wakawa wazima, wakasimama kwa miguu yao, wakawa kikosi kikubwa sanasana.
11
Akaniambia: Mwana wa mtu, mifupa hii ndiyo mlango wote wa Isiraeli. Tazama, husema: Mifupa yetu imekauka, kingojeo chetu kimepotea, tumekatwa roho.
12
Kwa hiyo wafumbulie ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiyafunua makaburi yenu, niwatoe mle makaburini mwenu ninyi mlio ukoo wangu! Kisha nitawapeleka katika nchi ya Isiraeli.
13
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa mle makaburini mwenu ninyi mlio ukoo wangu.
14
Nitawatia Roho yangu, mpate kuwa wazima tena, kisha nitawapeleka katika nchi yenu, mtulie huko; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, niliyoyasema ninayafanya; ndivyo, asemavyo Bwana.
15
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
16
Mwana wa mtu, jipatie kijiti kimoja, ukiandike: Cha Yuda na cha wana wa Isiraeli walio wenziwe! Kisha jipatie kijiti kingine, ukiandike: Cha Yosefu! maana ni kijiti cha Efuraimu na cha mlango wa Isiraeli walio wenziwe!
17
Kisha vibandike kimoja kwa mwenziwe, vishikamane kuwa kwako kijiti kimoja tu, hivyo viwili viwe kimoja kabisa mkononi mwako!
18
Kama wana wao walio ukoo wako watakuuliza kwamba: Hutuambii maana yao hayo, uliyo nayo?
19
waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona mimi, nikikichukua kijiti cha Yosefu kilichomo mkononi mwa Efuraimu nayo makabila ya Waisiraeli walio wenziwe, niwatie pamoja na kijiti cha Yuda, niwafanye kuwa kijiti kimoja tu; ndipo, watakapokuwa kimoja mkononi mwangu.
20
Navyo vijiti, ulivyoviandika, sharti viwe mkononi mwako machoni pao.
21
Kisha uwaambie: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiwachukua wana wa Isiraeli kwenye wamizimu, walikopelekwa, niwakusanye na kuwatoa pande zote; kisha nitawapeleka katika nchi yao.
22
Huko nitawafanya kuwa kabila moja katika nchi hiyo kwenye milima ya Isiraeli. Naye mfalme wao wote atakuwa mmoja tu, hawatakuwa tena makabila mawili, wala hawatagawanyika tena kuwa nchi mbili zenye wafalme.
23
Wala hawatajipatia uchafu tena kwa kuyatambikia yale magogo yao wala kwa kuyafanya machukizo yao na mapotovu yao yote; nami nitawaokoa na kuwatoa mahali pao pote palipowakosesha, niwatakase; ndipo, watakapokuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
24
Naye mtumishi wangu Dawidi atakuwa mfalme wao, yeye peke yake atakuwa mchungaji wao wote; ndipo, watakapoyafuata mashauri yangu na kuyashika maongozi yangu, wayafanye.
25
Hivyo watakaa katika nchi hiyo, niliyompa mtumishi wangu Yakobo, waliyoikaa baba zenu; ndiko, watakakokaa wao na wana wao na wajukuu wao kale na kale, naye mtumishi wangu Dawidi atakuwa mfalme wao kale na kale.
26
Nitafanya nao agano la kuwapa utengemano, nalo litakuwa la kale na kale kwao; nami nitawapa kukaa na kuwa wengi, hata Patakatifu pangu nitapaweka, pawe katikati yao kale na kale.
27
Hapo patakuwa Kao langu la kwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa ukoo wangu.
28
Ndipo, wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi Bwana ndiye anayewatakasa Waisiraeli, Patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao kale na kale.
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 38 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48