bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 11
Ezekiel 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 12 →
1
Roho ikanichukua, ikanipeleka kwenye lango la Nyumba ya Bwana la mashariki lielekealo maawioni kwa jua. Hapo pa kulilingilia lile lango nikapaona waume 25; katikati yao nikamwona Yazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, walio wakuu wa ukoo huu.
2
Akaniambia: Mwana wa mtu, hawa waume ndio wanaowaza yaliyomaovu na kuwapigia watu mashauri mabaya humu mjini.
3
Ndio wanaosema: Kujenga nyumba siko karibu; mji huu ndio nyungu, nasi ndio nyama.
4
Kwa hiyo wafumbulie yatakayokuwa! Wafumbulie, mwana wa mtu!
5
Ndipo, Roho ya Bwana iliponiangukia, ikaniambia: Sema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ndivyo, mlivyosema, mlio wa mlango wa Isiraeli, nayo mawazo yainukayo rohoni mwenu mimi nimeyajua.
6
Wenzenu, mliowaua humu mjini, ni wengi, mkajaza barabara za mji mizoga yao.
7
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wenzenu, mliowaua na kuwalaza humu mjini, hao ndio nyama, nao mji huu ndio nyungu, lakini ninyi watawatoa humu mjini.
8
Panga mnaziogopa, lakini nitawaletea panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
9
Kisha nitawatoa humu mjini, niwatie mikononi mwa wageni; ndipo, nitakapowakatia mashauri.
10
Mtauawa kwa panga, kwenye mipaka ya Isiraeli ndiko, nitakakowapatiliza; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
11
Mji huu hautakuwa nyungu yenu, mkiwa nyama humu mjini, ila kwenye mipaka ya Isiraeli ndiko, nitakakowapatiliza.
12
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana; hamkuyafuata maongozi yangu, wala hamkuyafanya mashauri yangu, ila mmefanya, kama wamizimu wawazungukao wanavyopiga mashauri.
13
Ikawa, nilipowafumbulia haya, ndipo, Pelatia, mwana wa Benaya, alipokufa; nikaanguka kifudifudi na kulia kwa sauti kuu nikisema: E Bwana Mungu, wewe utalimaliza sao lake Isiraeli!
14
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
15
Mwana wa mtu, ndugu zako, hawa ndugu zako, ambao mlitekwa pamoja nao, hata mlango wote wa Isiraeli, hawa wote ndio, wenyeji wa Yerusalemu waliowaambia: Nendeni mbali mkitoka kwake Bwana! Sisi tumepewa nchi hii, iwe yetu!
16
Kwa hiyo sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema kwamba: Kweli nimewapeleka mbali kwenye wamizimu na kuwatawanya katika hizo nchi siku hizi zilizo chache, nikawa mwenyewe patakatifu pao katika nchi hizo, walikopelewa.
17
Kwa hiyo sema: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Nitawakusanya ninyi na kuwatoa katika hayo makabila, kweli nitawaunganisha ninyi na kuwatoa katika nchi hizo, nilikowatawanya, niwape ninyi nchi ya Isiraeli.
18
Napo watakapoiingia watayaondoa huko matapisho yake yote na machukizo yake yote.
19
Nami nitawapa kuwa moyo mmoja, tena nitatia roho moja mioyoni mwao; namo miilini mwao nitaitoa mioyo iliyo migumu kama mawe nikiwatia mioyo inayolegea kama nyama.
20
Ndivyo, watakavyoyafuata maongozi yangu na kuyashika mashauri yangu, wayafanye. Watakuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
21
Lakini wenye mioyo iyaelekeayo matapisho yao na machukizo yao, mioyo yao ikayafuata, basi, nitawapatilizia njia zao vichwani pao.
22
Ndipo, Makerubi walipoyakunjua mabawa yao, nayo magurudumu yakawa kando yao, nao utukufu wa Mungu wa Isiraeli ukawa juu yao.
23
Kisha utukufu wa Bwana ukapanda ukiondoka mle mjini katikati, ukasimama juu ya mlima ulioko karibu ya mji upande wa maawioni kwa jua.
24
Roho ikanichukua, ikanipeleka katika nchi ya Wakasidi kwenye mateka kwa nguvu ya hayo maono ya Roho ya Mungu. Kisha hayo maono, niliyoyaona, yakaniondokea.
25
Nikawaambia waliotekwa mambo yote ya Bwana, aliyonionyesha.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48