bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 25
Ezekiel 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 26 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, waelekezee wana wa Amoni uso wako, uwafumbulie yatakayokuwa!
3
Waambie wana wa Amoni: Lisikieni neno la Bwana Mungu! Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa ulipazomea Patakatifu pangu, palipotiwa uchafu, kwa kuwa uliizomea nayo nchi ya Isiraeli, ilipoangamizwa, ukawagutia nao walio mlango wa Yuda, walipotekwa na kuhamishwa,
4
kwa hiyo utaniona, nikikutia mikononi mwao watakao maawioni kwa jua, waichukue nchi yako, iwe yao, wayapige mahema yao kwako, waitumie nchi yako kuwa makao yao; hao ndio watakaoyala matunda yako, tena ndio watakaoyanywa maziwa yako.
5
Nao mji wa Raba nitautoa kuwa malisho ya ngamia, navyo vijiji vya wana wa Amoni vitakuwa matulio ya makundi ya mbuzi na kondoo. Ndipo mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
6
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa ulipiga makofi pamoja na kupiga shindo kwa miguu yako, ukafurahi kwa moyo wako wote ulio wenye mabezo kwa ajili ya nchi ya Isiraeli,
7
kwa hiyo utaniona, nikikukunjulia mkono wangu, nikutolee mataifa mengine, wakunyang'anye, kisha nitakuangamiza kwenye makabila ya watu, nikupoteze na kukutowesha katika nchi hizi. Ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
8
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa Wamoabu na Waseiri husema: Tazameni, mlango wa Yuda unafanyiziwa kama mataifa yote,
9
kwa hiyo mtaniona, nikiufunua ubavu wake Moabu kuanzia kwenye miji, kwenye ile miji yake iliyoko mipakani, iliyokuwa urembo wa nchi, kama Beti-Yesimoti na Baali-Meoni na Kiriataimu.
10
Nchi yao nitaitoa nayo yao wana wa Amoni, niwape watokao maawioni kwa jua, iwe yao, kusudi wana wa Amoni wasikumbukwe tena kwenye mataifa.
11
Wamoabu nao nitawahukumu; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana
12
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa Waedomu walijilipiza kwao wa mlango wa Yuda na kuwatoza malipizi, wamekora manza papo hapo, walipojilipiza kwao.
13
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Nitaikunjulia nchi ya Waedomu mkono wangu niangamize kwake watu na nyama, niigeuze kuwa mabomoko tu, kuanzia Temani mpaka Dedani watu watauawa kwa panga.
14
Nami nitawatia mikononi mwao walio ukoo wangu wa Isiraeli, wawatoze malipizi, niyatakayo, wakiwafanyizia Waedomu mambo, machafuko yangu makali yenye moto yanayoyataka, wapate kujua, ya kuwa lipizi ni langu mimi; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu
15
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa Wafilisti waliendelea kujilipiza, wakijilipiza na kutoza malipizi kwa mioyo yenye mabezo, wakayazidisha mabaya yao kwa kushika machukio ya kale na kale,
16
kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Mtaniona, nikiwakunjulia Wafilisti mkono wangu, niwaangamize hao Wakreta na kuyapoteza masao yao yaliyoko pwani kwenye bahari.
17
Nami nitawatoza malipizi makubwa na kuwapiga kwa makali yenye moto. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapowatoza malipizi yangu.
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48