bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 3
Ezekiel 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 4 →
1
Akaniambia: Mwana wa mtu, utakachokiona, kile! Ukile kitabu hiki kilichozingwa! Kisha nenda kusema na mlango wa Isiraeli!
2
Nikakifunua kinywa changu, akanilisha hicho kitabu cha kuzingwa.
3
Akaniambia: Mwana wa mtu, lilishe tumbo lako, uyajaze matumbo yake hiki kitabu cha kuzingwa, mimi ninachokupa! Basi, nikakila, kikawa kitamu kinywani mwangu kama asali.
4
Akaniambia: Mwana wa mtu, nenda, ufike kwao wa mlango wa Isiraeli, uwaambie niliyokuambia!
5
Kwani wewe hutumwi kwa kabila lenye msemo mgumu na ndimi nzito, ila kwa mlango wa Isiraeli.
6
Hutumwi kwa makabila mengi yenye misemo migeni na ndimi nzito, usizozisikia; kama ningekutuma kwao hao wangekusikia.
7
Lakini hawa wa mlango wa Isiraeli watakataa kukusikia, kwani hawataki kunisika mimi, kwani mlango wote wa Isiraeli ndio wenye mapaji mashupavu na wenye mioyo migumu.
8
Tazama: Nao uso wako nitaushupaza kuwa sawasawa kama zao, nalo paji lako nitalishupaza kuwa sawasawa kama yao.
9
Kama almasi inavyoshupaa kuliko mwamba, ndivyo, nilivyolipa paji lako kuwa. Usiwaogope, wala usizistuke nyuso zao! Kwani ndio mlango mkatavu.
10
Akaniambia: Mwana wa mtu, maneno yangu yote, nitakayokuambia, yaweke moyoni mwako ukiyasikia kwa masikio yako!
11
Kisha nenda ufike kwao waliotekwa na kuhamishwa, walio wana wa ukoo wako, useme nao na kuwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema. Ikiwa wanasikia, au ikiwa wanaacha kusikia, basi.
12
Upepo ukanichukua, nikasikia nyuma yangu sauti ya uvumi mkubwa wa kwamba: Utukufu wa Bwana na utukuzwe hapo, alipo!
13
Kukasikilika nako kuvuma kwa mabawa ya wale nyama, wakigusana na kuvuma, na kuvuma kwa yale magurudumu yaliyokuwako kwao, zikawa sauti za uvumi mkubwa.
14
Upepo ukanichukua, ukanipeleka; nami nikaenda kwa uchungu wa kukasirika rohoni mwangu, nao mkono wa Bwana ulikuwa ukinishika kwa nguvu.
15
Hivyo ndivyo, nilivyokuja Teli-Abibu kwao waliotekwa na kuhamishwa, waliokaa kwenye mto wa Kebari; huko walikokaa hao, ndiko, nilikokaa nami siku saba nikiwa kimya katikati yao kwa kushangaa.
16
Hizo siku saba zilipopita, neno la Bwana likanijia la kwamba:
17
Mwana wa mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa mlango wa Isiraeli. Hapo, utakaposikia neno kinywani mwangu, sharti uwaonye, wanisikie.
18
Ninapomwambia mtu asiyenicha: Utakufa, nawe usipomwonya, usiposema naye yeye asiyenicha, kwamba umwonye, aiache njia yake, umpatie kuwapo uzimani, basi, yeye asiyenicha atakufa kwa manza zake, alizozikora, lakini damu yake nitakulipisha, kwani itakuwa imeishika mikono yako.
19
Lakini wewe unapomwonya asiyenicha, naye asipoyaacha mapotovu yake, asiporudi katika njia yake ipotokayo, basi, yeye atakufa kwa manza zake, alizozikora, nawe wewe utakuwa umeiokoa roho yako.
20
Tena mwongofu anapouacha wongofu wake, afanye mapotovu, nitaweka mbele yake pa kujikwalia, naye atakufa. Ikiwa hukumwonya, atakufa kwa makosa yake, nayo maongofu yake, aliyoyafanya, hayatakumbukwa, lakini damu yake nitakulipisha, kwani itakuwa imeishika mikono yako.
21
Lakini wewe unapomwonya mwongofu, asikose kwa kuwa mwongofu, naye akaacha kukosa, basi, atakaa uzimani, kwani ameonyeka, nawe utakuwa umeiokoa roho yako.
22
Ndipo, mkono wa Bwana ulipokuja kuwa juu yangu, akaniambia: Ondoka kwenda kwenye mbuga iliyoko bondeni! Ndiko, nitakakosema na wewe.
23
Nikaondoka kwenda kwenye mbuga iliyoko bondeni, mara nikauona utukufu wa Bwana, ukisimama hapo, ulikuwa kama ule utukufu, niliouona kwenye mto wa Kebari, nikaanguka kifudifudi.
24
Kisha roho ikanijia, ikanipa kusimama kwa miguu yangu. Akasema na mimi, akaniambia: Ingia nyumbani mwako, ufungiwe humo!
25
Nawe mwana wa mtu, utaona, wakikutia kamba, wakufunge nazo, usiweze kutoka katikati yao.
26
Nao ulimi wako nitaugandamanisha na ufizi wako, uwe bubu, usiweze tena kuwaonya, kwani ndio mlango mkatavu.
27
Lakini hapo, nitakaposema na wewe, nitakifumbua kinywa chako, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema. Mwenye kusikia atasikia; lakini mwenye kukataa atakataa vilevile, kwani ndio mlango mkatavu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48