bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 26
Ezekiel 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 27 →
1
Ikawa katika mwaka wa 11 siku ya kwanza ya mwezi, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, Watiro waliuzomea Yerusalemu kwamba: Aha! umevunjika uliokuwa umeingiwa na makabila ya watu! Sasa watageuka, waje kwangu! Bado kidogo nitafurikiwa, kwa kuwa umebomoka!
3
Kwa sababu hii Bwana Mungu anasema hivi: Utaniona, nikikujia, wewe Tiro! Nitaleta mataifa mengi, wakupige, kama bahari inavyoleta mawimbi kwa mawimbi.
4
Wataziangusha kuta za boma lake Tiro na kuibomoa minara yake nami nitauparapara mchanga wake, upatoke, mpaka nipageuze mahali pake kuwa mwamba mtupu.
5
Hivyo patakuwa tu pa kuanikia nyavu katikati ya bahari, kwani mimi nimeyasema; nayo mataifa watapanyang'anyiana; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
6
Navyo vijiji vyake ulivyovijenga mrimani, watu wao watauawa kwa panga; ndipo watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
7
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikimleta Nebukadiresari, mfalme wa Babeli, aliye mfalme wa wafalme, aujie mji wa Tiro na kutoka kaskazini na kuleta farasi na magari ya watu wapandao farasi na vikosi vingi vya makabila ya watu.
8
Waliomo katika vijiji vyako vya mrimani atawaua kwa panga; kisha atakujengea minara ya vita, tena atakuzungushia ukingo wa mchanga na kukujengea hapohapo vibanda kuwa ngao zao.
9
Kisha atazipiga kuta za boma lako kwa vyombo vyake vya kubomolea, nayo minara yako ataivunja kwa vyuma vyake.
10
Kwa kuwa na farasi wengi mavumbi yao yatakufunika, kwa mashindo ya wapanda farasi na za magurudumu na za magari kuta zako zitatetemeka, atakapoingia katika malango yako, kama watu wanavyoingia katika mji uliovunjwa kwa nguvu.
11
Kwa kwato za farasi wake atazipondaponda barabara zako zote za mjini, walio ukoo wako atawaua kwa panga, nazo nguvu za vinyago vyako zitaangushwa chini.
12
Vilimbiko vyako watavinyang'anya, nazo mali zako za kuchuuzia wataziteka, kuta zako za boma watazibomoa, majumba yako, uliyoyatamani kwa uzuri wao, watayavunja, kisha watayatupa baharini mawe yako na miti yako na mavumbi yako.
13
Ndipo, nitakapozikomesha shangwe za nyimbo zako, zisisikiwe tena sauti za mazeze yako.
14
Hivyo nitakugeuza kuwa mwamba mtupu, uwe mahali pa kuanikia nyavu, hutajengwa tena, kwani mimi Bwana nimeyasema; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
15
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema kwa ajili ya Tiro: Je? Kwa uvumi wa anguko lako, kwa mauguzi yao walioumizwa na kuuawa kabisa kwa panga mjini mwako nchi za pwani zisitikisike?
16
Wafalme wote wa nchi zilizoko baharini watashuka katika viti vyao vya kifalme wakiziondoa kanzu zao za urembo na kuzivua nazo nguo zao za rangi, kisha watajivika mastuko na kukaa chini, wakistuka mara kwa mara kwa kupigwa na bumbuazi kwa ajili yako.
17
Kisha watakutungia ombolezo la kukulilia kwamba: kumbe umeangamia uliokaa baharini, uliokuwa mji wa kusifiwa tu kwa kukaa na nguvu zake baharini, huo wenyewe na watu wake waliokuwamo waliowatisha wote waliokaa pwani kwao!
18
Siku hiyo, utakapoangushwa, nchi zilizoko baharini zitakuwa zimestuka, navyo visiwa vilivyomo baharini vitakuwa vimetishika sana kwa kutoweka kwako.
19
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitakapokutoa kuwa mji uliobomolewa, kuwa kama miji mingine isiyokaa watu, nitakapokupandishia mawimbi ya bahari, maji yao mengi yakufunike,
20
ndipo, nitakapokusukuma, ushuke kwao walioshuka shimoni, kwao watu wa kale, ndipo nitakapokukalisha kuzimuni chini ya nchi kwenye mabomoko ya kale kwao washukao shimoni, kusudi watu wasikae mwako tena. Lakini nchi yao walio wazima nitaipitia urembo mwingine.
21
Nitakapokutisha, utakuwa umetoweka, usioneke tena kale na kale, ijapo watu wakutafute; ndivyo asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48